Zanzibar 2020 Hussein Mwinyi na CCM wana faida gani kwa Wazanzibari?

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
Viongozi wa CCM Tanganyika walipomchagua Hassan Mwinyi ili aje kuwa Rais wa Zanzibar, miongoni mwa sifa waliziompa ni mtu mpole na mkimya. Lakini hebu tujiulize sisi Wazanzibari huu upole wake utatusaidia nini!? Na huu ukimya wake wa kusema mengine na akayatenda mengine, tutanufaika nini?

Yeye mwenyewe amejinasibu na kujisifu kuwa atatuletea Maendeleo, atadumisha Amani, na ataondosha Upemba na Uunguja, na ataondosha matabaka. La kustaajabisha ni kwamba hivi sasa yeye bado ni kiongozi wa chama ambacho bado kipo madarakani, sasa kwanini asiyafanye haya kwa kutuonyesha mfano!? Lukuvi, Gwajima, Samwel Sitta, Ali kessy, na viongozi wengine wa CCM waliizungumza vibaya Zanzibar na kutukejeli Wazanzibari, na pia walitukashifu Waisilamu na kutudhalilisha, lakini mbona aliamuwa kuufyata na kuendelea kupiga makofi tu Bungeni?

Hassan Mwinyi amekuwa kiongozi ndani ya serikali ya CCM kwa miaka mingi sana mpaka leo, je ameinufaisha nini Zanzibar kupitia uongozi wake? Amewasaidia nini Wazanzibari tokea alipochaguliwa mpaka leo hii? Kipindi chote cha Ubunge wake na Uwaziri mbona hatujamsikia kuitetea Zanzibar wala kuwatetea Wazanzibari?

Hawa viongozi wa CCM wanapita wakihubiri amani, hali ya kuwa wanajua kwamba bila ya haki na usawa haiwezi kupatikana Amani. Huwezi kuwasikia wakihubiri haki na usawa kwa sababu wao ndio wanaoleta dhulma na maonevu kwa Wazanzibari, kila wanachokitenda hutazama maslahi yao na CCM wanzao tu. Kwenye majukwaa wanahubiria Amani Amani Amani, hali kuwa vitendo vyao ni vya uvunjifu wa Amani, kauli zao na matendo yao ni vitu viwili tofauti.

Hawa viongozi wa CCM ndio walioanzisha matabaka baina ya Wazanzibari, pamoja na ubaguzi wa Upemba na Uunguja. Halafu leo anataka kutudanganya, eti akiwa Rais atayaondosha haya yote! Lakini na yeye pia ni mmoja kati ya viongozi wa Serikali ya CCM kwa miaka mingi sana na wala hatujaiona juhudi yake ya kuhubiri haki wala usawa! Je, anataka kutufanya sisi ni watoto wadogo?

Hassan Mwinyi, katika Bunge la Katiba, yeye alikuwa ni mmoja kati ya walioikandamiza Zanzibar kwa kuipinga katiba mpya, bali alionekanwa wazi kuiunga mkono CCM kwa maslahi yake na waliomtuma. Kama kweli ana nia njema na Zanzibar, basi tungelimuona siku ile angeliitetea Zanzibar kwa kupatikana katiba mpya ili ipatikane Haki na Usawa, badala yake alituonyesha kibri na jeuri, halafu sasa anajaribu kutufanya sisi ni watoto wadogo.

Kwa miaka mingi sana Serikali ya Muungano imekuwa ikiizuilia Zanzibar mikopo na misaada, na huyu bwana ni waziri ndani ya Serikali hiyo, na hajapatapo kuonyesha msimamo wake kwa Zanzibar, halafu leo anajinasibu kwa sifa za kutaka kuleta maendeleo na kuikwamua kiuchumi Zanzibar! Hapa yapo masuali mengi ya kujiuliza maana huyu mtu ametumwa ili aje kuimaliza Zanzibar.

Kama kweli ana nia njema na Zanzibar; kwanini kwenye majukwaa yake hazisemei rasilmali na mafuta ya Zanzibar kuwa ni vya Wazanzibari!? Serikali ya Muungano inasema kwamba mafuta, madini, na rasilmali zote zilizokuwepo Zanzibar ni mali ya Muungano, wakati sisi Wazanzibari hatufaidiki chochote katika almasi ya Tanganyika, wala madini yao mengine, wala rasilmali zao, leo iweje chetu kiwe chao na cho kiwe chao!? Na nyinyi CCM-Zanzibar munalifurahia hilo na kuliunga mkono!

Hassan Mwinyi kwanini hazizungumzii kero za Muungano na madhila yanayoletwa na Muungano huu dhidi ya Zanzibar? Zanzibar miaka ya nyuma ilikuwa ni nchi bora tena ni tajiri, Amani na Usalama vilikuwa ndio desturi za Mzanzibari. Lakini Ali Hassan Mwinyi alipokuwa madarakani ndie alieziondosha nguvu za zanzibari, na akaipa mamlaka Tanganyika ya kuitawala Zanzibar. Leo hii SMZ ni sawa na Halmashauri ya Mkuranga!

Hassan Mwinyi pamoja na waliomtuma, sera yao kuu ni kuudumisha Muungano na kuyaenzi Mapinduzi. Sisi tunajua kwamba Mapinduzi 1964 waliuliwa Wazanzibari wengi sana kwa sababu tu hawakuwa ni wenye kuiunga mkono ASP, na huu Muungano ndio sababu kuu ya kuiua Zanzibar kiuchumi na kimaendeleo. Ni wazi kwamba hawa CCM hawana nia njema na Zanzibar na wala hawatujali Wazanzibari, ndio maana wakatuletea mtu kutoka Mkuranga ili aje kututawala kwa mkono wa chuma, halafu aikabidhishe rasmi Zanzibar iwe chini ya Mtawala Tanganyika kwa makubaliano ya kutiliana saini, hapo iwe ndio mwisho wa SMZ, mwisho wa Zanzibar.

Tazama namna gani CCM-Zanzibar walivyowakamata Masheikh wetu wakawapeleka Tanganyika ili wafungwe kifungo cha maisha bila kuhukumiwa, bila ya kupewa haki zao za kibinaadamu. Kosa la Masheikh hawa ni kuupinga udhalimu na hujuma zinazotokana na Muungano dhidi ya Zanzibar, kuyakemea vikali maonevu na dhulma zinazoletwa na CCM, pamoja na kutoyaunga mkono mauaji ya 1964. Kama kweli Hassan Mwinyi ni mtu mwema mpenda amani, mbona hajawahi hata siku moja kuwatetea Masheikh hawa, wala hajawahi kuonyesha nia ya kweli ya kuwaondoshea dhulma na maonevu yanayowapata?

Sisi Wazanzibari hatumhitaji Hassan Mwinyi wala CCM, wala hatuna ulazima wa kudumisha Muungano na kuyaenzi Mapinduzi, bali tunataka uhuru wa kujitawala utakaotuletea furaha na mapenzi, yaliyobakia yatakuja wenyewe. Haki na usawa ndio ndio sababu ya Amani katika nchi: "Tunataka nchi yetu sasa tumechoka".

Tokea 1995, CCM haijawahi kushinda Zanzibar, na hili analijua fika kila CCM, bali wanajitia ubabaifu tu. Wao wenyewe wanajua kwamba kinachowaweka madarakani ni mabavu ya ZEC pamoja na nguvu za vyombo vya Dola tu. Ama kwa mwaka huu na iwe basi, mumeshatusukuma mpaka tushafika ukingoni.

Wazanzibari tushikamane tuwe kitu kimoja, khofu na woga tuondoshae, kwa uwezo wa Allah tutashinda tu. La muhimu ni kujitahidi kumuomba Allah Subhaanahu waTaala ili atufanikishe tufanikiwe, atulinde na atuhifadhi. Nguvu za Allah Subhaanahu waTaala ndizo zitakazoiangamiza CCM na shari zao.

Nilikuwa UVCCM
 
Zanzibar ni tatizo mlipasa muwe mkoa tu yani just RC tu aje aongoze huo mkoa
 
Mkuu Kakke, kama hoja hii ni kweli, then hii inamaanisha kuna sababu! Je, mmeishawahi kufanya tathmini ni kwanini?
Kama hanjafanya tathmini, then endeleeni kujifurahisha!.

Iwapo CCM itashindwa Zanzibar, Nini Majaaliwa ya Muungano?

Kufuatia hoja za bandiko hili nililokuwekea, inabidi tuu lazima CCM ishinde Zanzibar.

P
Wewe nawe UNAJIDHALILISHA mtu wangu. Ni bora ukakaa kimya tu sio kuyashupalia MAMBO YASIO KUHUSUU.

wewe unaisemea Zanzibar kama nani!
 
Acha porojo utaona manufaa akiwa rais kwa sasa wewe kampigie kura ya ndio halafu jiandae kula mema ya nchi.
 
Mkuu Kakke, kama hoja hii ni kweli, then hii inamaanisha kuna sababu! Je, mmeishawahi kufanya tathmini ni kwanini?
Kama hanjafanya tathmini, then endeleeni kujifurahisha!

Iwapo CCM itashindwa Zanzibar, Nini Majaaliwa ya Muungano?

Kufuatia hoja za bandiko hili nililokuwekea, inabidi tuu lazima CCM ishinde Zanzibar.

P
Mimi ni mwumini wa "UMOJA NI NGUVU" ila kwa tofauti ya mitazamo ya Wanzibari na Watanzania Bara, kama itatokea Zanzibar kuchagua upinzani, hasa chama cha Maalim Seif, nadiriki kusema kuwa muungano utavunjika.

Uwezekano wa Maalim kushinda umeongezewa nguvu na ropoka ropoka ya Lissu leo Unguja. INAFIKIRISHA lakini naamini CCM imejipanga kukabili vuguvugu hizo kulinda muungano wa kihistoria wa Serikali moja ya muungano wa nchi mbili hadi hapo tutakapokuwa tayari kuunda Serikali ya nchi moja.
 
“Upole na ukimya” wake ndio wanachotaka CCM Bara ili waendelee kumbulldose na kumuamuru cha kufanya bila hofu ya kuhojiwa au kubishiwa
 
Huna mapenzi na Zanzibar wewe, hata hizo nyuzi zako tuu zinaonesha wazi kabisa..

Mapenzi ya kuiombea Zanzibar ifutike ndio mapenzi gani hayo kwa Zanzibar!!? Hivi Unaweza kuenda Zanzibar mbele za watu ukayasema maneno hayo!?

Kuiombea Zanzibar ifutike hayo ni mapenzi au UNAFIKI !!?
 
Back
Top Bottom