Hussein Bashe Historia itakuandika

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
May 24, 2008
10,942
428
Moja ya sifa waliyonayo baadhi ya viongozi na wanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM) ,ni tabia mbaya ya unafiki.


Tabia ya Unafiki ni mbaya na inakera sana ,kwa sababu mtu mnafiki anaweza akaja nyumbani kwako akakusalimu huku akiwa na uso wenye tabasamu lakini moyoni mwake anatamani hata asikuone au wakati mwingine aitoe roho yako.

Mifano ya tabia hiyo ndani ya ccm ni mingi mno ,lakini leo ni vema tukaangalia vitendo vya kinafiki vinavyoendelea kutokea kwenye majukwaa ya kampeni ya chama hicho katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu

Sote tunakumbuka jinsi mchakato wa kura za maoni ndani ya ccm ulivyofanyika nchi nzima ambapo kulikuwa na vilio vya watu kuchezeana rafu za kisiasa ,rushwa ,kadi feki na mambo mengine mengi.

Baada ya mchakato huo ambao kwa wagombea wengine ulikuwa mchungu ,Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Ilikutana dodoma na kupitisha majina ya wagombea wa udiwani ,ubunge na wale wa ngazi ya kitaifa

Maamuzi ya NEC Dodoma kwa kiasi kikubwa yalizingatia na kuheshimu maamuzi ya wanachama walioshiriki kwenye kupiga kura za maoni ,kwa sababu wengi walioshinda kwenye kura hizo ,ndio waliopitishwa kupeperusha bendera za chama hicho.

Lakini kwenye kikao hicho hicho cha Dodoma baadhi ya wagombea walioshinda kwenye kura za maoni majina yao yaliondilewa na nafasi yao yaliondolewa na nafasi za ugombea wakapewa walioshindwa ,tena wengine walishindwa kwa aibu kubwa

Ni dhairi kabisa kuwa maamuzi hayo ya NEC yamekitia dosari kubwa sana chama hicho katika maeneo husika ,na zaidi yamepandikiza chuki kubwa miongoni mwa wanachama wake ,kwa sasa wanalazimishwa wawapigie kura watu wasiowahitaji kuwaongoza.

Kutokana na hilo ,kuna matukio ambayo yametokea katika majimbo mawili ya uchaguzi ,matukio ambayo yamenisukuma na kuandika ,majimbo yenyewe ni Nzega mkoani Tabora,na Iringa mjini mkoani Iringa

Iringa mjini aliyeibuka na ushindi ni Fredrick Mwakalebela,lakini NEC wakaondoa jina lake kwa madi kuwa anakabiliwa na kesi ya rushwa anayodaiwa kutoa wakati wa kura za maoni

sababu zilizotolewa na NEC dhidi ya mwakalebela ukiziangalia kwa umakini ,hazikuwa na mantiki na kilichoonekana ni kuwa wakubwa walimtaka monika mbega na si vinginevyo.

Kwa sababu kama suala ni tuhuma za rushwa kwenye kura za maoni ,naamini zaidi ya nusu ya wagombea wangeenguliwa wakiwamo mawaziri

Au kama suala ni kesi iliyokuwa katika hatua za mwisho kabla ya kupelekwa mahakamani kuna Bail mramba, Andrew chenge ,amaye ana kesi nzito mahakamani la kulitia Taifa hasara kubwa ,lakini mbona wao wameachwa wagombee.

Lakini pamoja na kufanyiwa yale yote aliyofanyiwa Mwakalebela ameamua kuwa mnafiki ,na akakubali kupanda jukwaani na kushiriki kumnadi monica mbega.

Ni vigumu kwa mtu yoyote mwenye akili timamu kuamini kama lile cheko na tabasamu la mwakalebela pale jukwaani kama ni la dhati na linatoka moyoni .pia hata wale waliompigia kura za maoni,katika hali ya kawaida watakuwa wanamuona kama kamanda msaliti ambaye amewageuka wapiganaji.

Kwa sababu kama ccm walikuona kuwa hufai ,wakaliondoa jina lako ,lazima ujiulize kuwa kumetokea nini ,na sasa wanakuona kuwa wewe ni mtu muhimu kiasi cha kukupandisha jukwaani na kukumwagia sifa lukuki ambazo hazikusaidii kitu chochote

Kwani siku ile pale Iringa mjini alipofika jk ,mwakalebela ungeamua kubaki nyumbani unakunywa kahawa yako ,ni nini kingetokea?na kwa kufanya hivyo heshima yako miongoni mwa wapenzi wako ingekuwa kubwa sana kuliko ilivyo sasa.

Mwakalebela unapaswa kufahamu kitu kimoja kikubwa katika maisha, destinity ya mtu yoyote ipo mikononi mwa mungu pekee, si kwa mtu wala chama au taasisi yoyote ile,kwahiyo unafiki haupaswi kuwa na nafasi katika maisha ya mtu yoyote makini na asiyependa mzaha.

Binafsi simfahamu mwakalebela au mhe mbega ,laakini naamini wote wawili ni wakubwa kiumri kwa mjumbe wa baraza la utekelezaji la umoja wa vijana wa CCM Ridhwan kikwete,pia mama mbega ni mkuu wa mkoa ,au kwa lugha raisi ni kiongozi mkubwa wa serikali.

Sasa inapofika kwa wawili hao kukalishwa chini kupatanishwa na Ridhwan .ni kichekesho cha mwaka na zaidi ni kujidhalilisha mbele ya wapiga kura.

Tukirudi jimboni nzega, nako kikao cha NEC dodoma kilimfanyia uhuni na kumuengua mginbea aliyeshinda kwenye kura za maoni ,tena kwa kura nyingi mno kulinganisha na mgombea aliyepitishwa

Husei Bahe alipata kura 14,422 ,dhidi ya kura 1.566 alizopata kigwangala ,ambaye alipitishwa kugombea ,uamuzi ambao ni sawa na tusi kwa wana ccm wa Nzega

Kwa mujibu kwa katibu mwenezi wa ccm Taifa john chilagati Bashe alienguliwa kutokana na kutokuwa na uraia wa Tanzania ,jambo ambalo siku chache baadae serikali ya ccm ikautangazia umma wa watanzania kuwa Bashe ni raia ,tena uraia wake hauna shaka yoyote

kimsingi ccm walichokifanya dodoma ni fitina na uhuni ,lengo likiwa ni kumfuraisha Ridwan kikwete

Pamoja na yote hayo kufanyika lakini Bashe aliweka bayana msimamo wake kuwa atabaki kuwa mwanachama mwaminifu wa CCM ,hatakiama chama hicho ,na ahadi alizotoa kwa wapiga kura wa Nzega atazitimiza

Lakini Kikubwa Zaidi ambacho kinapaswa kuigwa na wana CCM ambao wamedhulumiwa haki yao ya kugombea kama Bashe ,ni kitendo chake cha kukataa kuwa mnafiki kama ilivyokuwa kwa mwakalebela

Bashe alihudhuria mkutano wa jk nzega lakinini alisimamia kile anachokiamini ,na kamwe hakuruhusu unafiki kwa kujibaraguza na kupanda jukwaani kumnadi kigwangala

Kutokana na uamuzi huo makini na adimu ndani ya CCM ,Bashe ameudhirishia umma wa wana Nzega na Tanzania kuwa ni mtu mwenye msimamo ,haterereki ,si mwoga na ushaidi tosha kuwa bunge lijalo litakosa mchango wa mwanasiasa kijana asiyetikisika ,
 
Tungemshangaa kama angelikuwa mnafiki mbele ya kiongozi aliyepigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la uteuzi wa Bashe. Tutawashangaa pia wana Nzega iwapo wataamua kumpa kura zao JK ambaye ndiye haswa aliyemuumiza Bashe kwa sababu majina ya wawania ugombea yalifikishwa kwake hata kabla ya kikao cha uteuzi, iweje ashindwe kutumia vyombo vinavyohusika kuweza kupata uhakika wa uraia wa Bashe kabla hajamhukumu kwa kumuonea na kumdhalilisha? Kuna uvumi kwamba kulikuwa na 'mkono' wa Ridhwani kwenye Bashe kunyimwa nafasi ya kuwa mgombea. Kama hivyo ndivyo naona Tanzania sasa inatawaliwa kifalme na labda tusema ki-chifu!!
 
Sijaelewa! alivyoonyesha ukamovu, kwa kuhudhuria mkutano lakini asiongee au hakuhudhuria kabisa? fungueni tafadhali
 
huyo mwakalebela ni mganga njaa ndo maana kakubali kuwa ndio mzee, labda kuna kitu kaahidiwa. Hongera kwa bashe
 
JK kwa kinywa chake alitamka kuwa Bashe sio raia kisa ana bifu na mtoto wake
 
Naona huelewi kilichojiri pale Nzega siku Jk anahutubia,kwanza alipanda Huyo Mgombea wa sasa,umati ukanonekana haumkubali.........toka wanaingia kiwanjani vijana wengi walikuwa wakiimba jina na BASHE ,hivyo Jk akaona ataunguza karata kwa kumpandisha Bashe JUkwaani,huko kwingine hali ilikuwa nzuri ndo maana waliitwa.
Bashe si ametumiwa barua ya Kushiriki kampeni za Nzega za Ubunge na yeye amekubali kukisaidia chama chake na alisema hana kinyongo ..........kampeni zinaendela na Ngoja uone utabaini.
 
Jamani mnamsema Mwakalebela yupi? yule aliyetoa rushwa kubwa zaidi kuliko ya Monica?
Haaaaaaaa huyo hakupanda jukwaani kwa mapenzi. Anaogopa kitanzi cha rushwa kilicho mbele yake na kwa hilo kajisalimisha kama kondoo wa kafara. hahahahahahahahaha
 
Back
Top Bottom