Hussein Bashe afanya ziara ya ghafla katika hospitali ya wilaya ya Nzega

jamaa babaishaji balaa,naambiwa yupo kwenye Finance committee hata soksi hajafaa.muulizeni mipaka ya mamlaka yake inaishia wapi,yeye yupo kwenye baraza la mji mdogo na hospital ipo halmashauri ya wilaya.kwa kifupi alikuwa anawahi kushtukiza ili kumuwahi kigwangala
kabisa mkuu
 
Hivi hawa wanaojiita viongozi hawajui kuwa hospital zote nchini za serikali zina hali moja, hizo ziara za kushitukizana zinasaidia nini sasa!?
Mi nahisi wanakwenda kwa mara ya kwanza kujionea hali za hospital zetu maana wao hawajawahi kwenda kutibiwa
 
Nini maana ya kukurupuka??? Kukurupuka inatumika kama unatoa habari hasi kwa mhusika, lakini idara ya habari inaelekea ilikuwa inaripoti habari chanya za mbunge. Je Kichwa cha habari kililenga kuwavutia wasomaji wengi ili waone ujinga au uzoba wa mbunge, au idara haikuelewa maana na impact ya neno walilotumia?? Naomba maelezo tafadhari.

kwanini huwa hamchelewi?
 
No. 7 nina wasiwasi je atawezaje kuhamasisha wananchi kutoa damu salama kama anatoa amri hivyo? Au atawalaghai wanafunzi wa sekondari na vyuo ambao lishe yao ni hafifu waje kuchangia damu? Hivi Mbunge ana ruhusa ya kupiga marufuku kitu chochote au yeye ni diwani anayependekeza na watekelezaji wanakuwa wengine?
 
Kigwangala amekaa miaka mitano,Bashe llazima afanye ziara ya kushitukiza maana ni mgeni hapo nzega,wananzega uchaguzi umeisha na msimu wa maembe umeisha,kazi kwenu.
 
mbunge wa nzega mjini mhe. Hussein bashe amefanya ziara ya ghafla katika hospitali ya wilaya ya nzega leo tarehe 12.12.2015 na kubaini mapungufu makubwa katika utoaji wa huduma za afya.


Mbunge wa jimbo la nzega mjini mhe. Hussein mohamed bashe majira ya saa tano na nusu asubuhi leo jumamosi tarehe 12.12.2015 amefanya ziara ya ghafla katika hospitali ya nzega mjini na kubaini mapungufu makubwa katika utoaji wa huduma za afya kama ifuatavyo.


1) upungufu mkubwa wa vifaa tiba hasa vifaa vya kujifungulia kwa wakina mama wajawazito.

2) ikiwa ni pamoja na uhaba wa vitanda vya wogonjwa hasa wodi ya wototo ambayo haina vitanda mahususi kwa ajili ya watoto. Uhaba wa matandiko kwenye vitanda, uhaba wa neti za mbu na ukosefu wa taa kubwa kwa ajili ya kumulika ndani ya wodi ya watoto, wanawake na wajawazito ili kufanikisha kazi ya kutafuta mishipa ya damu nyakati za usiku.

3) upungufu wa vifaa vya kujifungulia yaani delivery pack, pia amebaini uchakavu wa vifaa ndani ya chumba cha kuzalisha wajawazito ikiwa ni pamoja na uwepo wa mikasi yenye kutu.

4) uhaba wa mashine ya oxygen katika wodi ya wazazi na chumba cha kuzalishia wajawazito

5) uhaba wa damu salama kwa ajili ya matumizi ya kitabibu.

6) ubovu wa mashine ya kuulia vijidudu kama bakteria kwenye vyombo vyenye asili ya chuma yaani sterilizer inayotumika katika chumba cha kuzalishia wajawazito

7) malimbikizo makubwa ya madeni ya posho za watumishi wa hospitali kama vile on call allowance, on duty allowance, post-mortem allowance na posho za kujikimu kwa watumishi wapya walioajiriwa hivi karibuni.

8) karibuni asilimia 85 ya watumishi wote katika hospitali ya wilaya ya nzega hawajapandishwa vyeo kwa mujibu wa sheria na taratibu za utumishi.

9) hospitali inakabiliwa na uhaba mkubwa wa watumishi yaani madaktari na manesi.

10) tozo za ushuru wa maegesho ya baiskeli zinatozwa kwa wananchi wanaoenda hospitalini hapo.

11) uhaba wa majengo kama vile wodi ya wanawake ambayo inapokea wagonjwa wengi kuzidi uwezo wake.

12) uwezo mdogo wa hospitali kuhudumia jenereta hasa nyakati ambazo umeme unakatika mara kwa mara.

13) kutokutumika kwa jengo jipya la upasuaji (theatre) ambalo ujenzi wake umekamilika.

14) kutokufika kwa wakati kwa vifaa na madawa ya kufanikisha zoezi la upasuaji katika chumba cha upasuaji.

15) madaktari kutopita round kuangalia hali za wagonjwa kwa mfano wakati wa ziara katika wodi ya wazazi mbunge alikuta daktari hajapita round siku nzima, jambo ambalo linachangiwa na uhaba wa madaktari lakini pia uwajibikaji hafifu wa watumishi.

16) uzembe wa baadhi ya manesi kutowahudumia wagonjwa ipasavyo na kwa wakati, mfano mbunge alikuta mgonjwa aliyemaliza dripu tangu siku iliyopita saa mbili usiku na sindano ya dripu hiyo haikuondolewa mkononi mwake na dripu ikining?inia mkononi mpaka baada ya ndugu za mgonjwa huyo kulalamika mbele ya mbunge, hivyo nesi akalazimika kuichomoa.

17) malalamiko ya uwepo wa rushwa ili kuharakisha huduma za afya kwa wagonjwa hasa katika huduma za uzazi.

18) afisa afya wa wilaya ambaye yupo likizo ya masomo, amelalamikiwa na madaktari mara kwa mara kutoka likizo na kuja kugawa fedha za oc kisha anarudi masomoni.

Hatua alizozichukua mbunge.

1) mbunge amepiga marufuku hospitali ya wilaya ya nzega kutoza ushuru wa shilingi mia mbili kwa wananchi wanaoegesha baiskeli zao pindi wanapoingia ndani ya hospitali hiyo.

2) mbunge amedhamiria kushughulikia suala la utumishi wa hospitali ya nzega kwa kuhakikisha dmo (district medical officer-afisa afya wa wilaya) daktari mkuu wa wilaya ya nzega anahamishwa kituo cha kazi kutokana kushindwa kushughulikia kero za watumishi wa hospitali ya nzega na kutosimamia ipasavyo utolewaji wa huduma za afya hospitalini hapo.

3) mbunge amemtaka ded asiruhusu dmo arudi kazini ili tufanye uchunguzi wa oc na atafutiwe kazi sehemu nyingine na sio nzega kwa sababu hawezi kazi.

4) mbunge atahakikisha madai yote ya madeni ya posho za watumishi wa hospitali ya nzega mjini yanalipwa na halmashauri ya mji wa nzega haraka sana na kuahidi kuwasilisha madai hayo mbele ya kikao cha halmashauri ya mji wa nzega inayowajibika kulipa stahiki za watumishi hao.

5) mbuge atahakikisha ufumbuzi wa haraka unapatikana katika masuala yote ya upungufu wa vifaa tiba ikiwamo vifaa vya maabara, oxygen, vitanda kwenye wodi za watoto , wazazi na wanawake.

6) mbunge ameadhamiria kuhakikisha wananchi wengi zaidi wa jimbo la nzega mjini wanajiunga na mfuko wa afya ya jamii yaani [community health fund] au maarufu kama chf.

7) mbunge anakusudia kushughulikia suala la upatikanaji wa damu salama katika hospitali ya wilaya ya nzega.

8) mbunge ameahidi kushughulikia upatikanaji wa dawa nyakati zote katika hospitali ya wilaya ya nzega kwa kuhakikisha kuwa duka la bohari ya dawa yaani msd linafunguliwa katika hospitali ya wilaya ya nzega haraka iwezekanavyo.

9) aidha mbunge ameagiza apatiwe taarifa kamili ya kiasi cha malimbikizo ya madeni yanayodaiwa na watumishi wa hospitali ya wilaya ya nzega, ali kila mtumishi anayedai apewe stahiki zake haraka iwezekanavyo.

10) mbunge amewaelekeza wananchi kutoa taarifa za uwepo wa rushwa haraka sana kupita dirisha maalumu la malalamiko lililopo hospitalini hapo. Pia ameagiza uongozi wa hospitali kutoa elimu ya kutosha ya jinsi ya kuwasaidia wananchi kutoa malalamiko.

11) mbunge ameahidi kuisimamia halmashauri ya mji wa nzega ili iweze kumudu kuchangia gharama za kuendesha jenerata ya hosptali ili ikitokea umeme umezimika hospitalini huduma muhimu ziendelee.



Imetolewa na;
idara ya habari na mawasiliano
ofisi ya mbunge wa nzega mjini



amekurupuka!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Haingii huko yeye ni mwanasiasa na mbunge tu. Majukumu yake ni kuwasemea wananchi na wala si kuwajibisha viongozi. Hawezi kumtaka DED na hapa nadhani tujue mipaka ya kazi kati ya mihimili mitatu ya nchi i.e. mahakama, bunge na serikali.

Kaazi kweli kweli! Yaani Mimi ningekua DED ningempuuza mbunge huyo! Haelewi majukumu yake.
 
Hivi ziara za ghafla ni mahospitalini tu? na hakuna strategy nyingine zaidi ya ghafla ghafla?
 
Mkoa wa Tabora kwa ujumla bado una safari ndefu kufikia maendeleo ya kweli. Kwa mfano wakati wilaya ya HAI inapanga kuvuna maji ya mvua msimu mzima ili kuwawezesha kulima kilimo cha umwagiliaji mwaka mzima - kuna wilaya nchini bado zimo kwenye dimbwi la umasikini kwa mfano wilaya za Sikonge, Urambo, Nzega, Igunga zinatia huruma, yaani zimetapakaa kwenye dimbwi la umasikini uliokithiri - Barabara hakuna, Shule hazina madawati walimu hali mbaya , Hakuna kabisa maji safi, Elimu duni, Zahanati zipo mochwari

Kila mwaka wao ni kurudia rudia makosa tu - utafikiri wameshafunga ndoa ya kikirsito ya CCM. (No taraka)

Hawa si wa kusikitikia hata kidogo....
 
you are light???? ulitaka kumaanisha nini mkuu...yaani jamaa ni mwanga ama wewe ni kayumba product

kwanini husiongee kiswahili ukaeleweshwa kuliko kuandika kiingereza kibovu hivi jaman watanzania???/
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom