Huruma yenu wana JF iwe msaada! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huruma yenu wana JF iwe msaada!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by wiseboy, Apr 26, 2011.

 1. wiseboy

  wiseboy JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,713
  Likes Received: 1,893
  Trophy Points: 280
  hongereni kwa kuivuka pasaka tukiwa na uhai. (TUMSHUKURU ADENAI). Ni tumaini langu kuwa hapa jf ni kama chungu kilichobeba kila aina ya watu, wakubwa, watoto, wafanyakazi, wanafunzi n.k. Tatizo ni kwamba hapa mtaani kwetu kuna binti kanitia huruma na sina uwezo wa kumsaidia bnafsi ndo maana nimeamua kuleta hapa suala lake mnisaidie tatizo lake. Huyu binti alifiwa na mama yake akiwa na miaka 6. baada ya .hapo amelelewa na baba ake mzazi hadi alipofika kidato cha 4 mwaka jana. Akiwa kwenye mitihania kwa bahati mbaya baba ake naye akafariki kwa ajali ya gari, baada ya matokeo mwaka huu hakubahatika kufaulu kwenda 4m 5. Kusema ukweli ana maisha magumu sana na hana wa kumsaidia, hvyo amekuja kwangu na kuniomba nimsaidie sehemu angalau ya kupata kibarua, ki ukweli uso wake unatia huruma na mm bdo mwanafunzi na sina chanel ya vibarua, kama kuna m2 anachanel ya kazi naomba msaada wake. Nategemea msaada wenu tumsaidie yatima huyu anayekata tamaa ya kuishi. KARIBUNI
   
 2. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...dah, hii inasikitisha sana.
  Vipi Wajomba zake, shangazi, mama wadoko kwa wakubwa, baba wadogo/wakubwa?
  hana kaka wala dada?...msaada wa maana hapo ni kumuendeleza kielimu. Angalau ajue hata ku type kwa computer (secretarial courses)

  Mw'mungu amuepushie wataotaka kumfanya house girl!
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  Maisha ya sasa na ya Zamani ni tofauti sana, kama zamani kweli tungezungumza la kutafuta ndugu zake, lakini hilo la kwenda kwa ndugu miaka hii ataishia kuuza vitumbua na kuwapikia watoto wa ndugu zake wao wakiwa shule

  nadhani cha muhimu ni kama kuna mtu mwenye uwezo hamsaidie tu
   
 4. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Pole sana ndio mtihani huo, ni PM details zifuatazo:

  1. Form Four amepata division gani?
  2. Form Four amemaliza shule gani?
  3. Mtaa, wilaya na Mkoa alipo?
  4. Kwasasa anaishi na nani!
  5. Wewe unahusiano gani nae?
  6. Kabla ya kukuomba msaada amewai kuomba wapi zaidi?
  7. Ana umri gani?
  8. Kabila lake?
  9. Mawasiliano ya Ndugu wa karibu upande wa Baba na Mama yake
  10. Anaishi na nani kwasasa, jina na mawasiliano yake.
  Ukileta hizo taarifa mapema nitamsaidia zaidi ya upeo wa macho yako.
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,802
  Likes Received: 83,175
  Trophy Points: 280

  Nakubaliana nawe Mkuu Mbu, inasikitisha sana kusema kweli.
   
 6. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,056
  Likes Received: 24,060
  Trophy Points: 280
  Mkuu, nakuombea kwa Mungu uendelee kuwa na moyo wa upendo.....ila hapo kwenye kabila...... linaweza kuwa kikwazo? Kimefikia kipindi tunataka tusaidiane kwa kuzingatia kabila?
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  mKUU,
  Ubarikiwe sana endapo Mungu atakufanikisha kwa hili la msaada kwa yatima huyu!
  Naamini maswali haya yote yana nia ya kumjua vizuri mtu huyu, na hayana nia mbaya!
   
 8. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Mkuu Mungu akubariki na akuzidishie katika kila jambo na katika kila utakuwa unalolifanya
   
 9. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2011
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ha ha ha!
  HOMEBOY NIMEKUSTUKIA

  ha ha ha ha ha ha!

  sichangii kwenye hii sredi
   
 10. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Ma hg wengine wanalipwa kima cha chini kabisa wala usimkatishe tamaa mbu, anaweza fanya hiyo huku anaenda shule pia
   
 11. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #11
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Nashuruku sana kwa wote walionipa likes nakuniombea kwa Mola juu ya huyu yatima, shukrani za pekee ziwaendee wale walifahamu na kutambua umuhimu wa maswali yote yaliyoulizwa hasa lile la kabila ambalo linaonekana kama halikueleweka vyema kwa wote.

  Niseme tu swali la 'wewe ni kabila gani?' kwa kifupi ni la muhimu sana na halitakuja kufutika kwa haraka hasa kwa nchni changa kama zetu za africa! ni swali la msingi sana linaweza kuzaa maswali mengi sana juu yako hasa pale linapotokea matatizo baadae, hata hivyo kwa jamii nyingi za kiafrica kabila bado ni utambulisho muhimu na alama muhimu tusilipuuze hilo swali lina maana sana.

  Vyema tu nieleweke kuwa Mungu akikupa moyo wa kusaidia, haijalishi kabila, maana ni Mungu anakutumia tu! Ila kiukweli anayesaisia ni Mungu mwenyewe siku zote,na kumbuka kuwa Mungu hana kabila!

  Wana JF wote wanapaswa kujua kuwa wanao uwezo ndani yao ya kusaidia, kinachopungua ni utashi, na mara zote utashi utoka kwa mola, maana kila utakachotoa lazima atarudisha mara dufu! Kama huamini jaribu siku moja, cha muhimu ni kumjua unaye msaidia kinagaubaga maana mungu apendi kumsaidia hasiye na shida! Pia kumjua unayemsaidia inakupa nafasi ya kujua aina ya mstaada unaomfaa maana pia Mungu hapendi kumsaidia mtu kitu kisicho na manufaa kwake. hata kama ndicho anachokuomba!

  Mfano: Nikikuomba unisaidie bia mbili, hata kama ni kweli sina hizo bia mbili na nikweli nina hamu na kiu ya hizo bia mbili na kuwa ndio chaguo langu mimi binafsi muombaji kuwa nataka bia mbili, la hasa naamini huo msaada hauto funguliwa milango kwa Mungu.
   
 12. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #12
  Apr 27, 2011
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mbona mtoa mada kaingia mintini, nahisi kama anaweza kuwa bf wake...sorry, lakini hebu aje ajibu maswala ya muhimu hapo na dio tutajua tufanyeje.
   
 13. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #13
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,259
  Trophy Points: 280
  <p>
  </p>
  <p>&nbsp;</p>
  kuna mtoto mwingine kwa kumpa kazi kama hgeli pia ni njia ya kumsaidia kama mtu hawezi kuenda extra mile.hii itamhakikishia mahali pa kulala,kula na walau matibabu na faraja za kibinadamu bila kusahau kipato kidogo.manake mwisho wa siku wa siku atakosa pa kulala na kula aishie mikononi mwa wakware ambao watamtumia kimapenzii na kumharibia maisha jumla.isitoshe baada ya muda anakuwa na nafasi hata ya kusoma QT,mbona tunasomesha cherehani bana na kuwafanyia vicheni party wapate vyombo vya kuanzia maisha?tusitoe limits kwa msaada...
   
 14. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #14
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Umeenda mbali sana hadi katika kisogo cha kichwa changu! ila yawezekana ni katika kukusanya taarifa ili akirudi awe kamili au uhaba wa mtandano ndani ya Bongo!.

  "your speculations can tail the results of question 4 and 5; hence leads into biases!" anyway I appreciate your hypothesising.
   
 15. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #15
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Unaonaje ukitufumbua macho wote, maana ndio JF yenye kupeana elimu, sisi hatuja mstukia wala kung'amua lolote!tufumbue tafadhali.
   
 16. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #16
  Apr 27, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hommie ndo unataka kusema??????????????
   
 17. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #17
  Apr 27, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ama kweli dunia duara!!!
   
 18. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #18
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,259
  Trophy Points: 280
  sasa teamo bin shikh yahya nae kapotea!au ndo wanajadiliana na hommie wake watoke vipi ili wagawane hili dili?
  :lying: :shocked:
   
 19. wiseboy

  wiseboy JF-Expert Member

  #19
  Apr 27, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,713
  Likes Received: 1,893
  Trophy Points: 280
  asanteni kwa michango yenu, sory kwa kuchelewa kuwajb coz nipo shule na nilikosa mda kufungua net. kwa yule aliye taka ni Pm nitafanya hvyo soon ngoja nifanye mawasiliano na huyu yatima. ila kwa wale wanao apply utani ktk hili mara ni gf wangu, namuomba mungu awaepushe na awape upeo wa kujua tatizo la mwingine.
   
 20. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #20
  Apr 27, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Pole sana yatima kufiwa na wazazi jamani sio mchezo, tulipita hukohuko utafanikiwa ukiamini hivo
   
Loading...