Huruma ya CC ndiyo pona ya Chiligati na Nape

Kwani kama walienda mikoani kusemea yale waliokubaliana kuna ubaya gani? Basi kama wanastahili kuondolewa basi na mwenyekiti nae hafai kuongoza chama na yote kwa yote huo ulikuwa ni utetezi wa Edo, kumbuka hii ni kama mchezo wa karata 3......hivyo kugeuziwa kibao ni kawaida ila ni wakati muafaka sasa wa chama kuachana na sera za kujivua gamba na ijulikana kwamba chama hiki kiko kwa ajili ya matajiri na wafanya biashara kwani ile kusema ni chama cha wakulima na wafanya kazi inanipa walakini....na hiyo kauli mbiu vyema ikabadilika na itafutwe kauli mbiu nyingine itakayoendana na chama jinsi kilivyo kwa sasa. Maamuzi magumu yanahitaji mioyo migumu pia! Hebu sasa ifanyeni mioyo yenu kuwa migumu kwani ndo mtaweza kufanya maamuzi magumu.....Ah..wacha nichukue nafasi hii kuwapongeza ANC..juu ya Malema (wameweza).
 
Kuna mchangiaji mmoja kasema you sound like him, huwezi mlinganisha Nape na Zitto wala Lissu, tunajua Zitto alivyotetea maslahi ya taifa tuambie toka Nape awe vuvuzela amelisaidia nini taifa zaidi ya m/kiti wake? usichanganye mambo ya kitaifa na kichama, Nape kapewa cheo (miezi kama 8) lakini muda wote kautumia kupambana na Chadema na kuchonganisha wanachama wenzake sasa mtu kama huyu utamfananisha na Zitto au hata Mnyika mara kumi useme hata January kajaribu kutetea kwenye kamati ya nishati.
 
JohnShaaban kuna wengine huwa ni wasema kweli, Nape hana kosa lolote kuzunguka na kueneza yaliyokubaliwa na NEC (kama yapo) lakini kaponzwa na ujinga wake narudia ujinga wake wa kutokubali ushauri alokuwa anapewa kuwa amewekwa pale kama chambo la wakubwa kutimiza malengo yao baadae atatupwa. Lakini sina tatizo kama alikuwa najua mwisho wake utakuwa huu.
 
kwa sarakasi zilizopo ndani ya magamba, hakuna kitu ambacho tunaweza kuwaamini. Nape sasa sijui atakuwa nakisemea chama gani. maana huko aliko amezodolewa na kupgwa masinge ya nguvu.
 
Nape kaponza na kutumiwa na watu wenye interest ya urais 2015,kwakuwa yeye upeo wake mdogo wa kusoma mambo akajikuta anakurupuka,ni bora angebaki na CCJ kama mwaasisi na kukipigania chama chake kikapata usajili wa kudumu kuliko kufanya mazingaombwe yaliyo mgharimu.CCM ina wenyewe na wenyewe wameshamgeuka kilichobaki sasa ni visasi.Ushauri wa bure kwa Nape na mwenzake Chiligati,ni wakati wao sasa nao kumgeuka m/kiti na kuweka mambo hadharani.Kila mtu anajua kuwa m/kiti ndiye aliyemtuma sasa anakana ili tumueleweje?Chenge alisema wakimwaga mboga yeye anamwaga ugali,sasa wamemwaga mboga na ugali Nape na Chilligati watamwaga nini?Kumbe gamba lililokuwa linasubiriwa ni Nape?Yuko wapi Makongoro Nyerere,mbona amenyamza kimya ilihali chama kinachezewa?

Nafikiri ni wakati mwafaka kwa chama kutoa maamuzi magumu kwa mwenyekiti wake kuupotosha umma ilihali akijua kuwa yeye ndiyo gamba lililokuwa linastahili kuvuliwa.tunachosubiri ni CCM kuacha unafiki na kumvua kofia mwenyekiti kwa kushindwa kukiongoza chama na kuendeleza majungu na magawanyo wa kimakundi ndani ya chama.Aliwahi kutamka kuwa anayoyasema Nape yana baraka zake kama m/kiti na baraka za chama sasa leo anaposema chama hakikumtuma anamaanisha nini?Na kwa wadhifa wake ilitosha kumwita Nape nakumuuliza haya mambo ya kuchafua watu unayapata wapi,ikibidi na kuwaadhibu kwa mujibu wa kanuni za chama.

Ili CCM ipone 2015 lazima JK awajibishwe,angalau wananchi tutakuwa na imani na CCM.Kama ndiyo staili ya funika kombe mwanaharamu apite mmekwisha,mnatakiwa kusoma alama za nyakati bila kujali nani ni nani.Ninapozungumzia m/kiti kushindwa majukumu yake ni kwamba akiwa rais na m/kiti wa baraza la mawaziri ameshindwa kudhibiti mfumuko wa bei kwa kipindi chake chote alichopo madarakani lakini si hilo tuu,kama m/kiti wa chama anashangaa serikali anayoiongoza kushindwa kuwadhibitiwa wafanyabiashara kwa kupandisha bei za mafuta,hivi kama kweli huu si usanii nini?Yawezekana hajui majukumu yake!
 
Mnaomtetea nape hamjajua tatizo lake. Kwanzaa yeye indoo amesababisha tote Hays yakampata! Kikubwa Hana msimamo , juzi kaitisha wanahabari akijipinga yeye mwenyewe hajawahi kuwataja kama wao ni wahusika wakujivua Gambia. Haya Akane na huko! Inamaana anawaogopa NA sio mpambanaji
 
... Na nikweli kuwa kabla Nape na Chilgati hawajachukuliwa hatua ... Mwenyekiti wao aliyeasisi mchakato huo je yeye atakuwa kwenye nafasi gani?


mnachanganya mambo vijana hali ni tete kwa lowassa ndio maana analia lia apate wa kufa nae,kiufupi yeye lengo lake lilikua suala hilo la kujivua gamba lizikwe na nec ambako aliamini na ana wafuasi wengi,wapinzani wake hawakutaka nec ishughulike na suala hilo bali walitaka nec itoe kibali kwa kamati kuu kushughulika na hilo ambako huyo nape na chiligati ni wajumbe,lowassa hayumo kwenye kamati kuu na pia hana ushawishi,na kwa kuwakumbusha zaidi chiligati pia ni mjumbe wa kamatia ya maadili pia!



Kamati ya Maadili ina wajumbe wazito, baadhi yao ni: Mwenyekiti Kikwete, Makamu wenyeviti, Pius Msekwa na Amani Karume, Makamu wa Pili wa SMZ, Balozi Seif Iddi,Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Katibu Mkuu, Wilson Mukama na Manaibu Katibu Mkuu, Kapteni mstaafu John Chiligati na Vuai Ali Vuai.

Hawa ndio watakaomshughulikia Lowassa!!!!
 

hebu acha tabia ya kuropoka. hujui nini kinaendelea . hivi unafikiri nape anaweza kuzunguka nchi nzima na kuwalaani mafisadi bila baraka za mwenyekiti wake? au umeamua kuropoka tu kwa sababu umepewa mdomo wa kuongea.acha ushabiki wa kijinga.
 
hebu acha tabia ya kuropoka.hujui nini kinaendelea. hivi unafikiri nape anaweza kuzunguka nchi nzima na kuwalaani mafisadi bila baraka za mwenyekiti wake wa chama? au umeamua kuropoka tu kwa sababu umepewa mdomo wa kuongea. acha ushabiki wa kijinga. hujui unaongea nini wewe.hivi unafikiri kikwete yeye ni mjinga wa kukubali toka mwanzo ripoti ile ya richmond kusomwa hadharani wakati yeye alikuwa anajua fika kuwa lowasa amehusika kwenye mchezo mzima?jk angeweza kukataa ripoti ile isisomwe pale bungeni, lakini kwa sababu alijua lowasa ni mwizi ndio akaamua kumuumbua pale kwa staili ile ya kusomwa ripoti. na kwa taarifa yako lowasa atamalizwa keshokutwa kwenye kikao cha cc. acha kutetea ujinga ambao utakugharim hata wewe filipo.acha mawazo ya kitoto. haihitaji ufike udsm kutambua haya ninayokueleza filipo.lowasa, chenge na rostam wote ni wezi wakubwa.
 
Ni kweli Nape na Chiligati walizunguka nchi nzima wakitaja majina ya wanaotakiwa kujiondoa CCM bila kutumwa na mtu? Inawezekana kweli hii?
 

Mimi ndio niliyetoa kauli hiyo.
Kama utakuwa makini na kupitia thread yake kwa umakini.utaweza gundua ni jinsi gani anavyojitaidi kujifananishe yeye(DSN=NAPE) na viongozi fulalanifulani wa CDM.
Kwa mlinganisho huo wa ndugu DSN utaweza gundua yeye ni nani(kwa nature yake).
 

pole sana endelea kuota mchana!
 
kuna mtu humu jamvini aliwahi sema kuwa JK anamtumia huyu dogo!! tukamporomoshea maneno! sasa tumeona jinsi alivyomkana!!
JK NOMA JAMANI!!
 
Dunia haitabiriki, CCM haitabiriki chochote chaweza tokea wakati wowote; aliyekuwa anataka kuwavuwa wenzake gamba sasa anakaribia kuvuliwa yeye!!
 


Unawafahamu wajumbe wa kamati ya nidhamu ya CC ya CCM? Kama unawafahamu basi tafuta majina yao kisha ufanye tafakuri!!
 
Ni vigumu sana kufanya kazi katika mazingira yasiyofuata misingi. Chama kinaendeshwa kwa kufuata utashi na hisia za viongozi hasa mwenyekiti ndio matokeo yake. Kwa hili namlaumu Nyerere na kauli mbiu iliyorindima kila kona ya nchi ya "ZIDUMU FIKRA SAHIHI ZA MWENYEKITI WA CCM".Hivi Nape na Chiligati wasingekua "mediocres" si wangeweza hata kujiuzulu pale pale mwenyekiti alipomjibu Sumaye kwamba watachukuliwa hatua kwa kumwita Lowasa Gamba? Du nimekubali "kumvua Kobe gamba inahitaji timing".
 



Mkuu,
Natambua ufisadi wa EL na pia simkubali kabisa. Natambua uwezo mdogo wa huyo M/kiti wa ccm. Nilichochangia hapa ni kujaribu kuonesha sympath niliyonayo kwa Nape maana kinachoonekana ni kwamba mambo yamemgeukia. Leo yeye ndiye anayetakiwa kuvuliwa gamba na kuwaacha wale aliokuwa anahubiri nchi nzima kwamba lazima waondoke. That was my concern!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…