Naona ama kweli kumbe Nape ni tishio la wapenzi wa Chadema walioko humu ndani jamvini,Reality na sio facts wakimfukuza NAPE kwa na sio LOWASA kwa sasa CCM inavunjika kuliko angeondoka Lowasa japo Ukweli wa RICHMOND unaanza kuwa wazi,lakini sioo kuwa unamuondolea kitanzi cha lawama.Lakini kwa waelevu inaleta hoja kubwa zaidi ya kwani kama sifa hizo za utendaji wenye kubeba sifa ya kujiudhuru kulinda kitu ambacho kimekuja kuwa ni donda la AIBU YA TAIFA.Je kuna stahiki yoyote ya kuaminiwa tena.
Kama kuna mpango wowote kumuondoa kijana NAPE,ambae kwa namna fulani amesaidia sana kubadilisha UPEPO wa mwelekeo wa SIASA za CCM hakika toka kipande kile CHADEMA na watanzania wako kwenye pick ya kulalama UKAIBUKA mpango wa kuijvua gamba ambao ulipigiwa chepuo na vinala kibao kisha mbele ya safari wengineo wote walijitoa akabaki kijana Nape ambae spirit yake inanguvu kwa kuwa na sifa kubwa mbili moja ni UJANA na ya PILI,ni aina sahihi ya kizazi cha nyakati [Generation Era]. Hakika nyuma ya NAPE kuna watu makini [NJE YA MAFISADI] watakaoibuka ambao wamekaa pembeni wakiangalia SYNTHESIS ambayo inajaribu kutafuta JIBU LA KWELI NA KUIBUKA KWA DHANA MPYA KAMA CCM IFE AU CCM IZALIWE UPYA.
1: CCM IFE [kama itaendelea kuwabeba watuhumiwa na wale wote jamii inayowapigia kelele kuwa hawatakiwi ndani ya CCM NA SERIKALI]
2: CCM IZALIWE UPYA-[Kuwaondoa viongozi wote watuhumiwa wa UFISADI na ikibidi kuwafukuza ndani ya chama na kuwekwa kwa kanuni mpya ikiwemo kuanzishwa kwa sheria za wafanyabiashara kutokupewa madaraka ndani ya CCM huku wakiwa ni washriki wa biashara zao na kuweka wazi masharti na kanuni zenye kutoa haki sawa kwa mwanachama yoyote kuwa na ushiriki wa haki na sio wa rushwa kwenye chaguzi na maamuzi ya chama.
Nape ni kizazi cha upambandaji wa kijamii dhidi ya kinanchopaswa kuondoka na kinachotegemea kubaki na kuendeleza maisha kwa miaka 30 mpaka 50 ijayo.Nape ni kizazi cha kushinda na wakina ZITO,TINDU LISSU na wengineo kwa mujibu wa ITIKADI za vyama vyao.Hivyo CCM kukaa na kuanza kupoteza muda wa kujadili POSITIVE efforts za kuhujumu bidii za NAPE ambazo kwa ukweli ndizo REALITY [Hata kwa favour ya nature na spiritual wise] ambayo ni sawa na kumzuia LISSU au ZITTO kuwakilisha hoja yayote ya msingi dhidi ya TAIFA,basi nikushindana na NATURE na mwisho wake ni AIBU mara dufu.
Hivi rudi nyuma enzi ya ZITTO alipokuwa akipambana na WALAJI WA KEKI YA TAIFA, kuna mambo yalipita mengi sana dhidi yake lakini kwa kuwa asilia [nature] inamsimamia kwa mujibu ya dhana ya kizazi kipya na zama ya wengi, baadhi ya watu waliumia na nguvu iliyokuwa nyuma ya ZITTO ambayo ni umma,baada ya kuibuka kutaka kumnyamazisha,asizungumze ukweli kwa niaba ya kizazi kilichopo na kijacho.
Leo hii kwenye upinzani nguvu hiyo unaweza kuiona kwa TINDU LISSU,na kwa CCM nguvu hiyo iko kwa NAPE,kwa wanaojua how nature works na wenye kuheshimu uwepo wa Mungu wanajua nguvu hizo,hivyo sio za kupingana nazo bali kuzifuata vinginevyo ni kuzalishwa kwa aibu na majanga yasioweza kuelezeka kwa binadamu wasio tambua kuwa kuna nguvu za MUNGU zinaojua HILA [UONGO] na UKWELI unaozalishwa na sisi binadamu,kwa nia na makusudio na faida binafsi.
Na mbaya zaidi nyuma ya nguvu hiyo watu hawa wanakuwa walishaanza mapambano toka kwenye damu za mama na baba zao.LEO hii wakati nguvu ya LOWASA ni moja kuwa yeye ndiye uzao wa kwanza kwenye madaraka ya CCM kwa nguvu hiyo.NAPE na MAKONGORO kila mmoja ana nguvu mbili mpaka tatu za ziada kutokana na kuwa imekua hivyo ndani ya toka kwa wazazi.Na ndio maana Makongoro aliweza kusema yale ambayo ndani ya CCM wengine hawakuweza kusema kwa kumwambia Mwenyekiti wake Taarifa kutoka SITE [KWA WATANZANIA] juu ya RACHEL.Ile dare au uthubutu hauji hivi hivi uko ndani ya damu na uthubutu huo ndio huo wa wa NAPE.
Na hakika kama kweli wamempeleka kwenye CC,ni kualika Majanga ya ndani ya CCM na SERIKALI yake kwa kuwa muda huo ungetumika kuzungumzia madhara ya UFISADI ndani CCM na taarifa nyingine za msingi za kuludisha matumaini ya Watanzania ya kuichoka CCM,na nini kifanywe kuludisha Mapenzi hayo kwa Umma.
Yakiendelea hapo mtoto wa muhasisi wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere,aliposimama akamuuliza Mwenyekiti wake kuwa alipowainua mikono RACHEL wakati wa uchaguzi 2010,Wananchi walisema HII NDIYO NINI?Basi wajue Swali lile bado Wananchi awajajibiwa hivyo wasikimbie kuzima moto kwa
Mtungi wa Gasi ya Kupikia,badala ya kutumia Fire Extinguisher.
View attachment 42074Hakika Picha uongea Mara 1000.Unaweza kuona Nguvu ya Dogo,ukitaka kuijua NGUVU hiyo Mwangalie Gwiji anavyomwangalia Dogo Pata Picha Kichwani mwake yanayoendelea.Sifa kubwa ya Mungu ni pale anapomkabidhi adui aliyeshindikana kusulubiwa na kajitu kadogo [Daudi na Goliath].Kwa kawaida kanuni hii wengi hawaijui kuwa ipo na ufanya kazi katika mazingira gani.Mioyoni mwa watu hawa wanaosalimiana na NAPE wanapata shida sana inakuaje na bidii zote hizo za wakubwa dogo anadunda, tena dogo with a GENEUINE SMILE and not the FAKE ONE.Muache Mungu aitwe Mungu dakika za Mwisho asie amini MUNGU [ATHEIST] ataita Mapadre KUTHIBITISHA KUWA ANAMWAMINI MUNGU.