Huruma ya CC ndiyo pona ya Chiligati na Nape

Huruma ya CC ndiyo pona ya Chiligati na Nape

CCM nufanya maamuzi kwa kustukizana hawawezi kufanya maamuzi kwa msingi wa kweli
 
pole sana endelea kuota mchana!

Bashe na wenzake waitwa kuhojiwa
Kati ya wanaotajwa kuitwa mbele ya Kamati ya Maadili Jumapili iliyopita ni Hussein Bashe, mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana. Ukiacha nafasi hiyo ndani ya UVCCM, Bashe ni mwajiriwa wa kampuni ya magazeti ya New Habari inayomilikiwa na mfanyabiashara Rostam Aziz na mbunge wa zamani wa Igunga aliyejiondoa katika siasa miezi kadhaa iliyopita akidai amechoshwa na siasa chafu. Bashe ni mtendaji mkuu katika kampuni hiyo ya Rostam.
Kama walivyo Lowassa na Chenge, Rostam naye alikuwa akituhumiwa na chama chake kuwa kwa matendo yake na kutajwa sana katika matukio ya ufisadi; ya kampuni iliyochota fedha Benki Kuu ya Kagoda na kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond, anakikosesha mvuto mbele ya jamii jambo ambalo lilichangia kupungua kwa kura za mgombea wa CCM wa nafasi ya rais, Kikwete, ambaye aliporomoka hadi kufikia kura asilimia 61 katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kutoka katika asilimia 82 za mwaka 2005.
Bashe amekuwa akidaiwa kwamba alitoa matamshi mabaya dhidi ya chama chake akiwa wilayani Nzega alipoashiria kudai kwamba CCM isingeshinda katika uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi ya Rostam, Igunga, na hiyo ingesaidia kuweka heshima.
Imefahamika kwamba kamati hiyo pia ilimwita Katibu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kirumbe Ng’enda, ambaye anatuhumiwa kusababisha mtafaruku katika zoezi la kura za maoni kiasi cha kumshusha mmoja wa wagombea nafasi za udiwani wa viti maalumu vya wanawake kutoka nafasi ya juu hadi ya chini katika mazingira yanayoashiria ufisadi.
Kamati ya Maadili ina wajumbe wazito, baadhi yao ni: Mwenyekiti Kikwete, Makamu wenyeviti, Pius Msekwa na Amani Karume, Makamu wa Pili wa SMZ, Balozi Seif Iddi,Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Katibu Mkuu, Wilson Mukama na Manaibu Katibu Mkuu, Kapteni mstaafu John Chiligati na Vuai Ali Vuai.
Hakuna taarifa zilizokuwa zimepatikana kuhusiana na hatima ya Bashe na Ng’enda na baadhi ya wanachama wa UVCCM wanaodaiwa kutoa matamshi ya kashfa kwa Mwenyekiti ambao nao waliitwa.
Kwa kawaida, kamati hiyo ina mamlaka ya kuchukua hatua, lakini pia inaweza kupendekeza hatua za kuchukuliwa na vikao vya juu zaidi, yaani Kamati Kuu ambayo sehemu ya wajumbe wake ni haohao wa kwenye Kamati ya Maadili na NEC.

"Kilumbe Ng'enda amevuliwa Ukatibu wa Mkoa wa Dar es Salaam (CCM) kwa kosa la kutenda maamuzi binafsi kinyume na maamuzi ya vikao halali vya chama.

Taarifa tulizo nazo zinazidi kueleza kuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar naye yupo kwenye hatihati. Nyeti nyingine zinadai kuwa kutokana na EL kujaza watu wake Dodoma ili wafanye fujo basi huenda yeye na Chenge wakaachwa na maamuzi yakatolewa ghafla baada ya mkutano huko Dodoma.

Nape kasema nafasi hiyo imeondolewa mikononi mwa Ng'enda na atapangiwa nafasi nyingine"

SASA WE KURUPUKA TU KIJANA.....ENDELEA KUFIKIRIA MAMBO NDIO YAMEISHA!

U sound like him.

Dude in My Ancenstor's and Mwalimu Julias Kambarage Nyerere's grave I dont Know Any one among.But I speak as a normal Tanzania with fear of GOD,of which many Leaders of our nation has no that fear on them.Believe in Me am just a local Tanzania like You.
 
Kutokana na maamuzi ya mkutano uliomalizika jana mjini dodoma,na kutokana na Utetezi wa Lowasa,na kuhoji uhalali wa wawili hawa kuzunguka nchi nzima wakimtukana kwa kutumia pesa ya chama icho,je Nape na Chiligati wanalipi watakalokwepa?

Ngoja tuwe wazi,Nape na Chiligati hawana walilobakiza katika ccm(kwa mtazamo wangu) na iwekwe kwenye record humu jamvini kuwa cc itawaondoa kwa tuhuma izo haiwezi wabakiza.

Nawasilisha.

Lazima watimuliwe...
Huwezi kujishaua kupita kila kona kumchafua MUHESHIMIWA Lowassa.

Lowassa ni chaguo la Allah.
 
Bashe na wenzake waitwa kuhojiwa
Kati ya wanaotajwa kuitwa mbele ya Kamati ya Maadili Jumapili iliyopita ni Hussein Bashe, mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana. Ukiacha nafasi hiyo ndani ya UVCCM, Bashe ni mwajiriwa wa kampuni ya magazeti ya New Habari inayomilikiwa na mfanyabiashara Rostam Aziz na mbunge wa zamani wa Igunga aliyejiondoa katika siasa miezi kadhaa iliyopita akidai amechoshwa na siasa chafu. Bashe ni mtendaji mkuu katika kampuni hiyo ya Rostam.
Kama walivyo Lowassa na Chenge, Rostam naye alikuwa akituhumiwa na chama chake kuwa kwa matendo yake na kutajwa sana katika matukio ya ufisadi; ya kampuni iliyochota fedha Benki Kuu ya Kagoda na kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond, anakikosesha mvuto mbele ya jamii jambo ambalo lilichangia kupungua kwa kura za mgombea wa CCM wa nafasi ya rais, Kikwete, ambaye aliporomoka hadi kufikia kura asilimia 61 katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kutoka katika asilimia 82 za mwaka 2005.
Bashe amekuwa akidaiwa kwamba alitoa matamshi mabaya dhidi ya chama chake akiwa wilayani Nzega alipoashiria kudai kwamba CCM isingeshinda katika uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi ya Rostam, Igunga, na hiyo ingesaidia kuweka heshima.
Imefahamika kwamba kamati hiyo pia ilimwita Katibu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kirumbe Ng’enda, ambaye anatuhumiwa kusababisha mtafaruku katika zoezi la kura za maoni kiasi cha kumshusha mmoja wa wagombea nafasi za udiwani wa viti maalumu vya wanawake kutoka nafasi ya juu hadi ya chini katika mazingira yanayoashiria ufisadi.
Kamati ya Maadili ina wajumbe wazito, baadhi yao ni: Mwenyekiti Kikwete, Makamu wenyeviti, Pius Msekwa na Amani Karume, Makamu wa Pili wa SMZ, Balozi Seif Iddi,Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Katibu Mkuu, Wilson Mukama na Manaibu Katibu Mkuu, Kapteni mstaafu John Chiligati na Vuai Ali Vuai.
Hakuna taarifa zilizokuwa zimepatikana kuhusiana na hatima ya Bashe na Ng’enda na baadhi ya wanachama wa UVCCM wanaodaiwa kutoa matamshi ya kashfa kwa Mwenyekiti ambao nao waliitwa.
Kwa kawaida, kamati hiyo ina mamlaka ya kuchukua hatua, lakini pia inaweza kupendekeza hatua za kuchukuliwa na vikao vya juu zaidi, yaani Kamati Kuu ambayo sehemu ya wajumbe wake ni haohao wa kwenye Kamati ya Maadili na NEC.

"Kilumbe Ng'enda amevuliwa Ukatibu wa Mkoa wa Dar es Salaam (CCM) kwa kosa la kutenda maamuzi binafsi kinyume na maamuzi ya vikao halali vya chama.

Taarifa tulizo nazo zinazidi kueleza kuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar naye yupo kwenye hatihati. Nyeti nyingine zinadai kuwa kutokana na EL kujaza watu wake Dodoma ili wafanye fujo basi huenda yeye na Chenge wakaachwa na maamuzi yakatolewa ghafla baada ya mkutano huko Dodoma.

Nape kasema nafasi hiyo imeondolewa mikononi mwa Ng'enda na atapangiwa nafasi nyingine"

SASA WE KURUPUKA TU KIJANA.....ENDELEA KUFIKIRIA MAMBO NDIO YAMEISHA!

Usikurupuke...
Wa kumtoa CCM Muheshimiwa Lowassa ni nani??
 
Kuna mchangiaji mmoja kasema you sound like him, huwezi mlinganisha Nape na Zitto wala Lissu, tunajua Zitto alivyotetea maslahi ya taifa tuambie toka Nape awe vuvuzela amelisaidia nini taifa zaidi ya m/kiti wake? usichanganye mambo ya kitaifa na kichama, Nape kapewa cheo (miezi kama 8) lakini muda wote kautumia kupambana na Chadema na kuchonganisha wanachama wenzake sasa mtu kama huyu utamfananisha na Zitto au hata Mnyika mara kumi useme hata January kajaribu kutetea kwenye kamati ya nishati.

Rejea kwani kazi ya Nape nini kwa Chama chake,Kwani ameweka ili awasidie chadema washindea uchaguzi au wakubalike kwa Wananchi au amewekwa ili ajenge mikakati ya kuifanya Chadema ionekanae si lolote mbele ya Umma wa Watanzania kwa niaba ya Chama chake..

Nafasi ya Nape [Zamani ilijulikana kama Propaganda lakini kwa kizazi cha sasa matumizi ya neno Propaganda inabeba nafasi ya ubabe na dhuluma hivyo a modern way ni kuita kitengo cha Mahusiano ya Umma [Public Relation]uku kikiwa na mbinu za zinazoendana na mazingira ya sasa ya ushawishi kwa umma kwa njia ya makubaliano yenye kubeba uungwana na mapokeo ya pande mbili kuafikiana kwa nioa njema.

Hivyo basi kutaka kulinganisha faida na sio Umuhimu wa Nape dhidi ya umuhimu wa Zitto au LIssu dhidi ya Wapenzi wa Chadema ni kushabikia Obama kuwa kiongozi wa Rebuplican.Tufike hatua Mnyonge Mnyongeni lakini haki yake Mpeni.

Vyama vya siasa kazi yake ni kupigania nafasi ya kuaminika kwa jamii ilai kupewa RIDHAA YA WANANCHI ILI KUPEWA DOLA NA KUTAWALA UMMA KUPITIA DOLA.Hivyo sio Zitto wala TINDU LISSU watakao itakia Mema CCM ili ifanye mazuri kwa umma,kisha wao wakae Benchi ili iweje wakati ni jukumu la NAPE kuakikisha kuwa CHADEMA inaenda chini ili wao waendelee kauminika kwenye TAIFA na kupewa dhamana na TAIFA YA KUTAWALA.

Mbona swala hili la Kazi ya NAPE liko wazi kwa Mtu yoyote yule mwenye upeo na ufahamu wa kitu kinaitwa siasa na Maisha yetu katika mifumo ya uendeshaji Serikali duniani kote.

Hivyo Nape kuchukiwa na Wapenzi wa Chadema au Mashabiki wake mbona ni kitu cha kawaida kama ambavyp Rais JK alivyopata kusema ni heri ya SLAA awe RAIS kuliko TINDU LISSU kuwa Mbunge.Hizo zote ni mbinu za Wanasiasa kuwekeana vizingiti na mikwamo ili mmoja ashindea kumthibiti mwingine.

Hakika wana CHADEMA kumbe NAPE anawapata HEADACHE.
 
Lazima watimuliwe...
Huwezi kujishaua kupita kila kona kumchafua MUHESHIMIWA Lowassa.

Lowassa ni chaguo la Allah.

Lowasa ni chaguo la Allah!? My foot! Labda sio Allah ninayemjua! Mungu wangu hawezi kunichagulia Fisadi, Mla rushwa, Mwizi, Mlafi asiyeshiba, mwenye uchu wa madaraka aniongoze. Ndio maana alimkataa JK lakini nec na tiss wakamweka. Talk to Allah He'll show your right leader!
 
Usikurupuke.
Allah unamjuwa wewe?
Hebu tueleze anafananaje...
Then kama Muheshimiwa Lowassa ni mwizi, fisadi, mla rushwa nakushauri utafute mawakili na ukamfungulie kesi ili afungwe.
Hayo mambo ya kuja kuleta chuki zenu binafsi na porojo hapa JF ni wazi kuwa mmekosa hoja sasa mwaja na vioja.

LA MWISHO...
Muheshimiwa Lowassa hana uchu wa Madaraka, ila kwa hali iliyopo sasa ni wazi kuwa anapata msukumo toka kwa Mungu ili aje aliokoe Taifa hili.

Tuseme inshaalah
 
Ngoja nivute kikombe kingine cha kahawa .movie hii magamba part II naona Kama star wake Nape anakaribia kuuwawa ingawa sterling uwa hafi. Hii move chiboko sana uwezi Predict mwisho wake. Haya movie inaendelea..... Naona pale EL amechukua... bastola take toka kwenye safe yake, amevaa barbiturate.......
 
Back
Top Bottom