wasaimon
R I P
- Oct 6, 2010
- 220
- 45
Kwani kama walienda mikoani kusemea yale waliokubaliana kuna ubaya gani? Basi kama wanastahili kuondolewa basi na mwenyekiti nae hafai kuongoza chama na yote kwa yote huo ulikuwa ni utetezi wa Edo, kumbuka hii ni kama mchezo wa karata 3......hivyo kugeuziwa kibao ni kawaida ila ni wakati muafaka sasa wa chama kuachana na sera za kujivua gamba na ijulikana kwamba chama hiki kiko kwa ajili ya matajiri na wafanya biashara kwani ile kusema ni chama cha wakulima na wafanya kazi inanipa walakini....na hiyo kauli mbiu vyema ikabadilika na itafutwe kauli mbiu nyingine itakayoendana na chama jinsi kilivyo kwa sasa. Maamuzi magumu yanahitaji mioyo migumu pia! Hebu sasa ifanyeni mioyo yenu kuwa migumu kwani ndo mtaweza kufanya maamuzi magumu.....Ah..wacha nichukue nafasi hii kuwapongeza ANC..juu ya Malema (wameweza).