Humphrey Polepole: Rais Magufuli hafurahishwi na mjadala wa kuongezewa miaka ya Urais kutoka 5 hadi 7

mara nyingi ishu ya kuongezewa muda huwa inakua kwenye muhula wa mwisho sio sasa hivi,kwa sababu anajua akisema sasa hivi hali itakua si shwari,subiri muhula wa pili ndio mtapata majibu
Ngoja nikuweke kwenye Hansard zangu hapa, najua JF itakuwepo na tutafukua makaburi, INSHALLAH!
 
hawa ccm wa chini chini hujaribu kutafuta kila namna wakihisi wanamfurahisha na kumpaisha mkuu wao., na kule Zanzibar wako pia ccm ambao wametaka rais aongezewe mda na wengine wamesema sheria zibadilike sasa kwamba katika uchaguzi chama cha mapinduzi ndio watoe mgombea urais asiwe na mpinzani, wapinzani wasimamishe wabunge na wawakilishi tu kwenye uchaguzi.
 
Inawezeka ujio wa polepole umechangia polepole kuongelea maswala ya kuongoze muda wa uraia?au wananchi wanaandaliwa kisaikolojia kuwa likija kutokea huku mbeleni ionekane ni wananchi wenyewe wanataka rais aongezewe muda na sio rais anataka?
Una akili sana mkuu. Ni style ya PK kwamba aje aseme wananchi wamemuomba aongeze muda. Na ndo ajenda nafikiri ktk ugeni huu. Wanataka kuyapanga maana bado mpaka sasa hajafanikiwa.
Walianza wale wa "Magufuli baki"...wakazimwa. Akaletwa "Juma Nkamia " kiaina ...naye akazimwa. Wakaipeleka kwenye baraza la wawakilishi Zenji ili ipitie mlango wa nyuma....napo ikazimika fyuu..
Sasa ni wkt wa PK kumpa mbinu. Hatari sana.

Sasa jiulize leo inakuwa ndo coincidence Polepole kuliongelea. Ili kesho magazeti yaandike. Anafunika ujio wa PK na mambo ya uchaguz mdogo..
 
Magu angewaachia CDM wapate hata kitu kimoja cha kuongelea, Sasa anawakata mdomo wasiwe na chochote cha kulalamikia kama ada yao
 
You guys mpoje??? Hii nayo inatolewa press na ikulu??? Mambo ya kiccm mnatuletea hovyo kabisa

Hizi nii propaganda za kishenxx za CCM kuzima HABARI ZA CHAGUZI NDOGO uliofanyika leo baada ya UPINZANI KUSUSIA na hivo Wapiga kura wachache sana kujitokeza!!!!!!
AIBU YAO CCM.......!!!!!!!!
 
nitashangaa wazee wa chama, system na mkuu wa majeshi wakibariki kile kinacho itwa kuongezewa muda ili apambane kutuletea maendeleo zaidi.
nitashangaa sana.
 
Aliyeanzisha hii kitu ya seven yrs sijui anajisikia vipi sasa hivi. BIG UP MR PRESIDENT.....tunakuombea maisha marefu
 
Ukijiona unawaamini viongozi wa CCM basi utakuwa na mpumbavu wa kutupwa.
 
Uwa siamini wanasiasa hasa JPM kuna wakati akiwa zanzibar aliwai kusema hatateuwa mpinzani ata mmoja
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom