Humphrey Polepole, ni lini na kwa lipi CCM imewahi kuyakumbuka maslahi na haki za akina mama hapa nchini?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Humphrey Polepole, ni lini na kwa lipi CCM imewahi kuyakumbuka maslahi na haki za akina mama hapa nchini?

Pamoja na hawa akina mama kuwa mtaji wa CCM kuendelea kuwepo madarakani tangu Uhuru, cha kushangaza, Serikali yenu ya CCM imewanyima maji safi na salama.

Aidha, Serikali yenu ya CCM imeshindwa kabisa kuwarahisishia hawa akina mama hali ngumu za maisha wanazokabiliana nazo huku mitaani na majumbani.

Leo unavyowapaka mafuta hapa kwa mgongo wa chupa, Sukari inakaribia kufika Shilingi 3,000/= kwa Kilo moja. Mafuta ya kula ndio usiseme maana ni aibu ya mwaka.

CCM na Dola yenu mnawezaje kusimamia haki za akina mama wa nchi hii ili hali mwanadada Aquiline Akwilina ambaye kesho angeitwa mama fulani, ameuawa bila hatia akiwa safarini na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya wahusika.

Hawa akina mama hawataki kwamba haki na maslahi yao iwe ni hisani ya CCM na Serikali yake.

Badala yake wanataka uwaambie ilipo Rasmu ya Jaji Waryoba maana wanaamini haki na maslahi yao chini ya Katiba Mpya iliyo bora, hakuna hisani ya CCM na Serikali yake.

Na hiki ndio kilio chao kikuu leo mpaka kesho.
 
Kina mama ni watu rahisi sana kushawishika kwa vitu vidogo xna bt huwa wanaji sahau kuangalia mbele yao kuna nini,hebu angalia Leo watapata shida na kulaumu kila siku mtaani lakn ikifika wakt wa kampeni kwa kitenge cha kijani pa1 na kubebwa kwenye FUSO wana sahau matatiz yote haya kina MAMA mungu anawaona
 
Back
Top Bottom