Humphrey Polepole: Mshahara wangu ni tzs 1,000,000 tu

Humphrey Polepole: Mshahara wangu ni tzs 1,000,000 tu

Mshahara siyo pesa anayolipwa mtu moja kwa moja tu. Yapo mengi katika malipo ambayo hayatajwi hasa katika mtazamo finyu.
Hata MAUTI na UZIMA WA MILELE ni mishahara ambayo huwezi kuithaminisha kifedha.
 
Kama kupokea mshahara milioni moja ni uzalendo,wazalendo wa ukweli ni watumishi wa umma ambao wengi wao wanapokea mshahara robo ya milioni.

Wazalendo halisi walikuwa kina Kikwete walipomaliza vyuo mshahara kwa mwezi Tshs 500( mia tano) ilikuwa siyo zaidi ya 650!! Mkuu wa mkoa enzi hizo shs 500 na PhD yake!!!!(Dr Cleruu)!Waliokuwa wanajifanya wajanja walikimbilia Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo walikuwa wanalipwa hela ndefu kwa Pound Sterling kwa mwezi ila ndo hao sasa wanaandamana kudai mafao yao ya tangu 1977 hawajalipwa!!wale waliopata shida kwa kuishi na mishahara midogo wakavumilia serikalini ndo wenye raha(Presidents Ministers, Directors)!
 
Kama analipwa chini ya milioni moja kwanini kakimbia kule bahari beach alipokuwa anakaa kwa shemeji yake? Kipindi bado mwanaharakati alikuwa na kiduka cha tigopesa/m-pesa pale Bahari beach -Burget.ila kawaachia wadogo zake waendeshe yeye kakimbilia kuishi nyumba na kulipiwa kodi na serikali,gari gharama za serikali etc.
 
Kwahiyo kulipwa milioni moja ndio kipimo cha uzalendo? Unajua posho na marupurupu anayopata? Hivi unajua kuna kazi posho na marurupu hupita mshahara kwa mbali sana na inawezekana akapewa posho na marupu rupu ya siku moja tu ambayo ni zaidi ya huo mshahara. Huyo anapewa nyumba, gari, wasaidizi na hata ulinzi, matibabu na kila anapotoka analipwa. Lakini kuna mtumishi wa serikali anapata si zaidi ya shilingi laki 5 lakini usafiri, chakula, malazi na taka taka nyingine zote ni juu yake. Huyo utamwita nani sasa ni fisadi? Kama ungeambiwa Posho na marupu rupu anayolipwa rais kwa ziara zake hizi hizi za ndani ndio ungejua kuwa mshahara ni bosheni tu! Ndio maana wanataja mishahara lakini hawataji marupurupu mengine. Sasa rais kwa mfano chakula kwake na familia yake ni bure, malazi ni bure, mavazi ni bure, ulinzi ni bure, usafiri ni bure, wasaidizi kibao ni bure sasa huyo hata asipopata mshahara si anaishi tu?
Analipwa mshahara kidogo Ila marupurupu mengi ili kukwepa kulipa Kodi.Maana sidhani kama posho Huwa zinalipiwa Kodi.Kwa hiyo Polepole ni mkwepa Kodi tu
 
Mshahara siyo pesa anayolipwa mtu moja kwa moja tu. Yapo mengi katika malipo ambayo hayatajwi hasa katika mtazamo finyu.
Hata MAUTI na UZIMA WA MILELE ni mishahara ambayo huwezi kuithaminisha kifedha.
N
 
"Mshahara wangu kama katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha CCM ni chini ya million moja(1,000,000)." - Polepole abainisha.

Hakika huo ni uzalendo kwa chama na Taifa kwa ujumla , CCM ni kisima cha viongozi bora kabisa! Sasa na upinzani watuambie wanalipwa kiasi gani ?"

Anauliza Pole Pole

View attachment 860506

Source:EATV
Anaona rahisi kutaja mshahara, ataje na marupurupu!
 
Kwanza hiyo pesa anayo lipwa ni pesa nyingi sana. kwa sababu hamna kazi anayo fanya.
 
"Mshahara wangu kama katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha CCM ni chini ya million moja(1,000,000)." - Polepole abainisha.

Hakika huo ni uzalendo kwa chama na Taifa kwa ujumla , CCM ni kisima cha viongozi bora kabisa! Sasa na upinzani watuambie wanalipwa kiasi gani ?"

Anauliza Pole Pole

View attachment 860506

Source:EATV
Unafahamu posho yake kwa mwezi? Unajuwa posho yake ya safari? Unaijuwa posho yake ya nyumba? Unaijuwa posho yake ya communication? Unsijuwa posho yake ya mafuta kwa mwezi?
Mwisho lile fuko la manunuzi ya wabunge na madiwani unajuwa alipewa kiasi gani?

Wewe jijaze ujinga tu.
 
"Mshahara wangu kama katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha CCM ni chini ya million moja(1,000,000)." - Polepole abainisha.

Hakika huo ni uzalendo kwa chama na Taifa kwa ujumla , CCM ni kisima cha viongozi bora kabisa! Sasa na upinzani watuambie wanalipwa kiasi gani ?"

Anauliza Pole Pole

View attachment 860506

Source:EATV
Hebu leten na salary slip yake kabisa ili to prove!

Je, hana posho?
Hana gari lakupewa na mafuta

Ngoja niishie hapo tu!
 
Sasa hiyo ni ndogo ukilinganisha na upuuzi wake anaofanya mi hata buku nisingempa
 
Back
Top Bottom