Humphrey Polepole: Mshahara wangu ni tzs 1,000,000 tu

Humphrey Polepole: Mshahara wangu ni tzs 1,000,000 tu

"Mshahara wangu kama katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha CCM ni chini ya million moja(1,000,000)." - Polepole abainisha.

Hakika huo ni uzalendo kwa chama na Taifa kwa ujumla , CCM ni kisima cha viongozi bora kabisa! Sasa na upinzani watuambie wanalipwa kiasi gani ?"

Anauliza Pole Pole

View attachment 860506

Source:EATV
Marupurupu yake je ni shs. Ngapi? Atuambie complete package na sio kudanganya watu !
 
Wakati fulani YM akiwa KM wa CCM, wasaidizi wk walikuwa Nape na Mtanda pale Ofisi ndogo! Siku niliojua posho zao, nilitamani ile Kazi!
 
Kama mshahara wako milioni 1 tu yakiwemo na marupurupu pamoja na fringe benefits zako basi utakuwa MWIZI!
 
Mnawaamini wanasiasa? Huyu take home kwa mwezi haipungui
10m. asitudanganye
 
Kwahiyo kulipwa milioni moja ndio kipimo cha uzalendo? Unajua posho na marupurupu anayopata? Hivi unajua kuna kazi posho na marurupu hupita mshahara kwa mbali sana na inawezekana akapewa posho na marupu rupu ya siku moja tu ambayo ni zaidi ya huo mshahara. Huyo anapewa nyumba, gari, wasaidizi na hata ulinzi, matibabu na kila anapotoka analipwa. Lakini kuna mtumishi wa serikali anapata si zaidi ya shilingi laki 5 lakini usafiri, chakula, malazi na taka taka nyingine zote ni juu yake. Huyo utamwita nani sasa ni fisadi? Kama ungeambiwa Posho na marupu rupu anayolipwa rais kwa ziara zake hizi hizi za ndani ndio ungejua kuwa mshahara ni bosheni tu! Ndio maana wanataja mishahara lakini hawataji marupurupu mengine. Sasa rais kwa mfano chakula kwake na familia yake ni bure, malazi ni bure, mavazi ni bure, ulinzi ni bure, usafiri ni bure, wasaidizi kibao ni bure sasa huyo hata asipopata mshahara si anaishi tu?
Kwa hii CCM mpya uzalendo ni kuwa mjinga-mjinga.

Umasikini umefanywa kuwa joho la kajivunia.
 
"Mshahara wangu kama katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha CCM ni chini ya million moja(1,000,000)." - Polepole abainisha.

Hakika huo ni uzalendo kwa chama na Taifa kwa ujumla , CCM ni kisima cha viongozi bora kabisa! Sasa na upinzani watuambie wanalipwa kiasi gani ?"

Anauliza Pole Pole

View attachment 860506

Source:EATV
Pumba! Ukilipwa ml 1 ndio uzalendo?
 
ni mwendawazimu tu atakayeuamini uqongo huu.tatizo la wanasiasa wanaamini watu wote ni mbumbumbu.
 
ndio maana ufisadi hautaisha! mtu anaendeshwa na V8 halafu aseme mshahara chin ya 1M
matumiz ya gari na dereva tu yanaweza kuwa mara tano ya huo mshahara! uongooooooo
 
"Mshahara wangu kama katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha CCM ni chini ya million moja(1,000,000)." - Polepole abainisha.

Hakika huo ni uzalendo kwa chama na Taifa kwa ujumla , CCM ni kisima cha viongozi bora kabisa! Sasa na upinzani watuambie wanalipwa kiasi gani ?"

Anauliza Pole Pole

View attachment 860506

Source:EATV
Kwa kazi gani pesa yote hiyo?
 
Back
Top Bottom