Tatizo la Hp anatabirika atakachoongea, nimemsikiliza akiongea kupitaia Star Tv, Clouds FM, TBC mambo ni yaleyale. Kwa mfano ataongea kwamba kiongozi hatakiwi kuwa tajiri! huu ni ujuwa hata china wajamaa Deng Shao Ping alikataa siasa za namna hiyo zimepitwa na wakati. Ataongea tena kwamba kiongozi hutakiwi kuwa na madoa, Nani kakwambia kwamba tunatafuta malaika?
Katiba ya nchi inatamka kwamba kila mtu ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa na hakuna kifungu kidogo chochote kinachosema tajiri hatakiwi kuwa kiongozi. Kama napalilia umaskini ni yeye na familia yake. Kinachotakiwa si kumzuia mtiu tajiri kuwa kiongozi bali ni kuweka mfumo unaomlazimisha kiongozi hata kama ni tajiri asijipendelee. George Bush na Dick Cheney ni matajiri wakubwa lkn walipewa uongozi wa nchi ya Marekani.
Naweza nikatabiri mengine lkn niishie hapa