Pascal Ndege
JF-Expert Member
- Nov 24, 2012
- 2,977
- 1,897
Nimesoma sana habari za ST.Joseph University kwenye magazeti nimeamua kutoa ya moyoni kuhusu hivi vyuo.
Nadhani Elimu bora ni kuwa na walimu bora wenye uwezo wakufundisha wakiwa na amani na wala si vifaa bora na library nzuri pekee, Mazingira bora ya walimu hasa nyumba ni muhimu, mwalimu anakaa hostel kitanda cha double deck na masters yake ama PhD yake nikuminya haki za msingi za kibinadamu.
Hebu Serikali ingilie kati Ajira za hawa waalimu wanaoletwa kutoka india wananyanyaswa sana wengine wanaishia kulia na kuteseka hapa Tanzania nchi ya amani na upendo.
Hiki chuo kimekuwa na tabia ya kuajiri hukohuko India na kuwaleta kama volunteers kwa mgongo wa kanisa katoliki kisha huwanyng'anya passport, Hawa vijana wadogo hulipwa mshahara mdogo sana kiasi cha Dola 200 mpaka 500 ambazo hazilingani na Elimu walizonazo na kufanya wawe na mastress muda wote na wengi wao hukimbia wanapopata upenyo.
Hebu Idara ya uhamiaji waende kwenye Hostel wanazokaa waalimu, wakague waalimu wanaishi vipi! watakuta walimu wa chuo kikuu wanakatisha tamaa sana kunakipndi walikuwa wanakaa hadi watano chumba kimoja.
Kwa ada zaidi ya mil 2.7 kwa kila mwanafunzi kisha walimu wanapunjwa kwa ujira kidogo na makazi yasiyo na hadhi ya professor hii si dhamira bora ya kukuza elimu hapa nchini.
Mwalimu wa St. Joseph na mfungwa awana tofauti walipwe atleast vizuri na makazi bora.