Mkuu karne ya 24 mbali sana kwa muono wangu kumbuka teknolojia tayari ipo longtime ni suala la muda kidogo kwa mfano Tz kwa sasa kuna zoezi la vitambulisho vya uraia, kwa sasa kuna tulio wengi tuko kwenye paperless currency kwa maana ya kwamba unapata salary iliyolipwa online kwa internet banking, unanunua mafuta ya gari lako kwa fuel kadi, unaenda supermarket unalipa kwa Visa/Mastercard so kidogokidogo uchumi wetu unaanza kutokuwa na pesa kwa maana ya makaratasi soon mifumo ya tehama ya kibenki, mifuko ya hifadhi ya jamii, hospital vitambulisho vya taifa, umiliki wa ardhi, driving licence itakuwa centralized na kuna uwezekano mkubwa hii kwa nchi zisizo na uwezo zikapewa msaada (kupitia UN bodies) ili ziweze kuwa na centralized database ambayo ina information za watu wote! So si muda mrefu watakuja na vichip vyao ambazo vipo linked na central database!
Mbona kuna familia za kitajiri ambazo tayari watu wake wamekewa hizo chip kwa maana ya kwamba hata ukiwateka itajulikana wako wapi na hii ni hasahasa amerika ya kusini.
Na hata wanyama wengi ulaya na marekani wamewekewa hizi!
Actually kwa uelewa wangu, microchip hizo ni kama tu chip za simu i.e. unayo chipu ya simu ambayo iko linked na service provider Voda, Tigo nk then unapata mawasiliano, ila hizi ni chip ndogo sana ambazo zinapandikizwa mwili mwa binadamu na ambazo kwa habari zilizopo sehemu nzuri ambapo kwenye mwili zitakaa hizo chip ni kwenye paji la uso au mkononi kiganjani! Inshort kila kitu kipo tayari na utekelezaji ulishaanza na unaendelea kwa kasi sana ila kwa wengine hawajui kitu wao wakiona matigo pesa, vitambulisho vya taifa, mkongo wa taifa na mengine meengi wanatazama upande mmoja tu na shetani naye anapita hapohapo kama ambavyo Mungu kaumba mahindi na tunakula ugali, shetani amemcorrupt mwanadamu anatengeneza pombe! ngoja niishie hapa.