FT: Premier League: Hull City 2-0 Man United. Unamuonaje Kocha Carrick?

FT: Premier League: Hull City 2-0 Man United. Unamuonaje Kocha Carrick?

Mawele

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
920
Reaction score
3,204
ENGLAND: Msimu uliopita #ManchesterUnited iliumaliza kwa kuonesha ushindani mzuri, safari hii Msimu wa 2026/27 katika Premier League imeanza kwa kupigwa 2-0 kutoka kwa timu iliyopanda daraja, Hull City.

Mdau, una neno gani kwa Kocha wa Man United, Michael Carrick?
 
Hull City wamemnyuka Manchester United kwenye mechi yao ya kwanza baada kurejea Premier League baada ya miaka 9.

Hebu vuta picha, unarudi kwenye ligi ngumu kuliko zote duniani baada ya miaka 9 ya kuitafuta, halafu mechi ya kwanza tu unamlaza na viatu Manchester United ya Michael Carrick, moja ya timu zilizowasha moto hatari msimu uliopita, mbele ya mashabiki zaidi ya 24,000 waliokuwa wanapiga kelele mwanzo mwisho.

Kumbuka tu, miaka 5 iliyopita hawa jamaa walikuwa wanavuja jasho Daraja la Tatu (League One), lakini leo wamefanikiwa kupata ushindi nyumbani na kuanza Ligi Kuu kwa kishindo. Mashabiki wote jukwaani machozi yanawatoka kwa furaha.

Kwenye mpira wa miguu bwana hakuna matokeo yaliyokwisha andikwa kwenye mawe. Na msituambie tena soka ni mchezo wa kawaida tu, wanaosema hivyo hawataelewa kamwe hisia tunazopitia wapenda soka.

1787420436392.png
 
Back
Top Bottom