Hukumu ya zinaa katika dini

Zerock

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2026
Posts
964
Reaction score
1,959
Tunapokuwa tunazungumza Sheria katika dini, tunamaanisha miongozo iliyonyooka, (haibadilishwi).

Katika dini (uislamu) hukumu ya zinaa imetajwa katika mafungu mawili
• wazinifu walio kwenye ndoa
• wazinifu ambao hawajaoa

Katika kila kundi lina adhabu yake kutokana na athari watakazoacha kwenye jamii husika.

Watu wengi sahiv ujisifu kwa zinaa (kwenye mitandao au masikani yao) " dalili za kiyama "

Katika mafundisho ya dini (uislamu) mwanamke ndiye chanzo kikubwa cha zinaa.

KIVIPI..?

• Zinaa haiwezi kutokea bila ridhaa ya mwanamke, mwanamke anauwezo wa asilimia 100 kukataa na mwanaume hasiweze kumlazimisha kukutana faragha.

• Athari za zinaa umwangukia zaidi mwanamke kuliko mwanaume
(Mimba,aibu kwa familia na kuharibu nasaba)

Sura al Nuur: inasema...
Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanaume....

Kwanini aya imeanza na mwanamke...?

Mwanamke ndiye mwenye funguo ya kufungua zinaa au kufunga zinaa.

Zerock
 
Good sana mim dudu langu naunga hoja kabisa....
 
Kila mwanaume amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha zini......

How about women? Au mpaka wafanye...
 
Kama wanawake ni wengi kuzidi wanaume je wengine watapewa doz na nan?

Kwa maana ndugu zetu wanajitahidi kuoa wawili au watatu lakini wanawake ni Bado ?
 
Kila mwanaume amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha zini......

How about women? Au mpaka wafanye...
Ili zinaa kubwa itimie lazima ipite katika hatua (7)
Mtume Muhammad (s.a.w) anasema

Mwana wa Adam ameandikiwa fungu lake la zinaa, atalipata bila shaka.
• Zinaa ya macho (kuangalia )
• zinaa ya masikio (kusikiliza)
• zinaa ya ulimi (kuongea)
• zinaa ya mikono (kushika)
• Zinaa ya miguu (kutembea)
• zinaa ya moyo (kutamani)
• zinaa ya utupu (kutenda kitendo)
 
Najiuliza vitabu vya dini vingeandikwa zama hizi, zingemuoneshaje mwanamke kutokana na mabadiliko ya leo.

By the way, kiislamu mwanaume anapewa adhabu gani katika zinaa
 
Nilifikiri utasema Ile adhabu ya kupigwa bakora 100 kwa watu wanaofanya ngono nje ya ndoa kama vile Quran ilivyoamrisha.
 
Najiuliza vitabu vya dini vingeandikwa zama hizi, zingemuoneshaje mwanamke kutokana na mabadiliko ya leo.

By the way, kiislamu mwanaume anapewa adhabu gani katika zinaa
Adhabu ni wote wanatakiwa wapigwe viboko 100 kila mmoja.
 
Nilifikiri utasema Ile adhabu ya kupigwa bakora 100 kwa watu wanaofanya ngono nje ya ndoa kama vile Quran ilivyoamrisha.
Kweli,ila sikutak kuandika aya yote...
Nilitaka kuonyesha nani mhusika mkuu kwenye zinaa
Ndo maana nimeinukuu nusu tu
 
Kweli,ila sikutak kuandika aya yote...
Nilitaka kuonyesha nani mhusika mkuu kwenye zinaa
Ndo maana nimeinukuu nusu tu
Kwa nini unaficha kwamba adhabu ya zinaa kwa Muislamu ni bakora 100 ??
 
Hovyo et zinaa haiwezi kutokea bila mwanamke vip bila mwanaume kutongoza inawezekana je hiyo zinaa

Yaani asiongelewe wa kwanza anasemwa anaemaliza

Hata hivyo haishangazi kwa hii dini ya mfumo dume

Dini ni utapeli tu
 
Najiuliza vitabu vya dini vingeandikwa zama hizi, zingemuoneshaje mwanamke kutokana na mabadiliko ya leo.

By the way, kiislamu mwanaume anapewa adhabu gani katika zinaa
Kuna makundi mawili ya wazinifu
1) walioowa
Hawa hukumu yao ni kupigwa mawe hadi kufa.
Lakin hadi hukumu isimame lazma wawepo mashahidi (4) walioshuhudia hicho kitendo , chini ya mashahid 4 hakuna hukumu na uliyeshitaki utapigwa bakora 80

2) wazinifu ambao hawajaoa
Kupigwa bakora 100 kila mmoja
 
Hovyo et zinaa haiwezi kutokea bila mwanamke vip bila mwanaume kutongoza inawezekana je hiyo zinaa

Yaani asiongelewe wa kwanza anasemwa anaemaliza

Hata hivyo haishangazi kwa hii dini ya mfumo dume

Dini ni utapeli tu
Nadhan nimejibu swali lako la siku ile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…