Hukumu Ya Mtanzania Atakayevunja Ahadi Ya Kuoa Au Kuolewa.

NDUKI

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
3,423
2,414



Wakili Leornad Manyama amesema kwa mujibu wa kifungu cha 69 na 71 cha Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, Mwanamke au Mwanaume ana haki ya kwenda Mahakamani kufungua kesi ya kutaka kulipwa fidia kwa kupotezewa muda au kudharirika endapo ataahidiwa ndoa kisha ahadi ikavunjwa.

Sheria hiyo haihusiki kati ya mwanaume na mwanaume au mwanamke na mwanamke unatakiwa kuwa karibu ya mwanaume na mwanamke. Pia awe ametimiza umri wa miaka 18 na kuendelea, asiwe pia mwanafunzi hapo fidia haitawezekana kulipwa kisheria.

Pia mahusiano hayo yasiwe ya kaka na dada au baba na mtoto mahusiano ya Aina hiyo hayatatambulika kulipwa fidia kama mmoja wa hao atakuwa amevunja ahadi.

Na kama kuna mmoja wa wachumba atakayevunja ahadi ya kuoa au kuolewa inampasa yule aliyeathirika kwenda mahakamani na kufungua kesi kwa ajili yako kulipwa fidia.

Kama ikatokea mlipeana zawadi na ahadi ikavunjwa inatakiwa kwenda mahakamani kudai zawadi ulizompa mchumba wako zirejeshwe kwenye umiliki wako.
 
Back
Top Bottom