Hukumu ya Kijana Abdul Nondo

Hukumu ya Kijana Abdul Nondo

Hata Mandela alifungwa japo hakustahili. Halikadhalika, Yesu pia alihukumiwa na kusulubiwa japo hakuwa na hatia yoyote..Hivyo, wakimfunga Nondo, haitakuwa ajabu, ila akishinda, basi haki itakuwa imeshinda dhuluma na uonevu.
Mandela unamfananisha na Nondo?? Aiseee
 
ID yako tu pekee imetosha kunifanya nijutie kwanini nimeufungua na kuusoma huu ' Uzi ' wako.
Waulize wajuzi wa Mambo na wakongwe humu watakujuza ..Halafu kuwa Mpole kijana acha kujifanya Mtu wa codes tunakuchora tu utakuja liwa timing ukose pakutokea
 
Waulize wajuzi wa Mambo na wakongwe humu watakujuza ..Halafu kuwa Mpole kijana acha kujifanya Mtu wa codes tunakuchora tu utakuja liwa timing ukose pakutokea

Tena hakuna Mtu anayependa Vita vya Kuviziana na Kumalizana kama Mimi na bahati nzuri naviweza vizuri sana hivyo kama vipi nakuomba tu ulianzishe ili tuone Mimi na Wewe nani ameiva vyema. Pimbi mkubwa Wewe!
 
Umepanic 😄si unaona sasa unaanza kutema matusi kama Konki Master .Kijana usione watu wanajitoa akili na wewe ukaanza kucheza na beat utapotea.Mimi nimeshamaliza na wewe ujumbe umekufikia
 
Umepanic 😄si unaona sasa unaanza kutema matusi kama Konki Master .Kijana usione watu wanajitoa akili na wewe ukaanza kucheza na beat utapotea.Mimi nimeshamaliza na wewe ujumbe umekufikia

Asili yangu tu yenyewe ni Mtu wa Mapigano ya Kimedani ( Battle ) sasa sijui utaniwezaje ' Kisudu / Mpuuzi ' Wewe.
 
November 5, 2018
Iringa, Tanzania

Hukumu : Abdul Nondo ashinda kesi

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa leo, Jumatatu, Novemba 5 imemuachia huru Mwenyekiti wa mtandao wa wanafunzi nchini, Abdul Nondo baada ya Jamhuri kushindwa kuthibitisha makosa mawili yaliyokuwa yakimkabili mshtakiwa huyo.

5 Nov 2018
"Siwezi kurudi nyuma hata kidogo...hata kidogo...siwezi...pale haki inapominywa nitaendelea kusema," - ni kauli ya Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Abdul Nondo aliyoitoa dakika chache baada ya kutoka mahakamani.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa, Riad Chamshama amesema baada ya pande zote mbili kukamilisha ushahidi waliwasilisha majumuisho yao ambapo upande wa Jamhuri haukuwa na ushahidi wowote juu Abdul Nondo kutenda makosa hayo mawili ya kusema uongo.

Amesema mshtakiwa alikiri kuwepo mjini Mafinga lakini upande wa Jamuhuri ulishindwa kueleza kabla ya Abdul Nondo kuwepo Mafinga alikuwa wapi hivyo ushahidi namba moja na namba sita ni wa hisia kitu ambacho mahakama haikubaliani nacho.

Aidha ushahidi mwingine uliotiliwa mashaka na mahakama ni kielelezo namba 6 ambacho ni maelezo yaliyotolewa na mshtakiwa yakielezwa kuwa yalikuwa ni ukurasa mmoja wakati mahakamani ziliwasilishwa kurasa nne hali iliyoleta mkanganyiko kwa mahakama.

Hakimu Chamshama amesema ushahidi namba 1&2 nao ulikuwa na mkanganyiko kwani walimchukulia Abdul Nondo kama mhalifu badala ya mlalamikaji pindi alipofika kituoni kutoa taarifa za kutekwa kwake.

Nje ya mahakama Abdul Nondo ameishukuru mahakama kwa kutenda haki na kuongeza kuwa licha ya kuyumbishwa na kesi hiyo, hatakaa kimywa kamwe katika harakati zake za kutetea maslahi ya wanaoonewa.
Source : azam tv
c.c Mzushi Magonjwa Mtambuka Mtaa wa Lumumba
 
Back
Top Bottom