Hukumu Kesi ya Mgomo wa Walimu: Mgomo ni batili

Tatizo si uhalali wa mgomo wa waalimu,bali tatizo ni juu ya KIINI cha mgomo huo,hata kama mahakama imesitisha mgomo huo kwa kuwa si halali CWT watakubaliana kusitisha mgomo kwa muda wajipe muda wa kuandaa mgomo mwingine HALALI kwa mujibu wa sheria na kuutekeleza tena kwakuwa dhamira ya kugoma inaishi ktk mioyo yao hadi hapo serikali itakapokubali kuketi ktk meza ya majadiliano ili kutibu tatizo ,kilichofanyika sasa ni kuahirisha tatizo la leo kwa kulihamishia kesho.panapofuka moshi ndugu zangu sharti uzime moto chini na DHAMIRA ya jambo fulani ina nguvu hata wakilazimishwa kurudi madarasani tutavuna mabua! GRANT

Kinachoiokoa serikali hii kila siku ni mahakama zake,na wameifanya mahakama kuwa km msuluhishi wa matatizo ya kada mbalimbali ambayo yanahitaji tathmini ya kina katika kuelewa chanzo chake,sasa kila siku wao wana buy time.
 
Mimi niliwashauri walimu wasigome bali waendelee na kale kautaratibu, kupeleka wanafunzi kidato cha kwanza wasio jua kusoma na kuandika, kidato cha nne kufeli kwa asilimia 85. Mwisho umma ndiyo wangegoma na siyo nyie walimu. Mkanipuuza mmewaona mafisadi walivyo na mbinu chafu. Narudia tena kuwashauri endeleeni na ule utaratibu tena kazeni sana mwaka huu kidato cha nne wafeli kwa 95% na kidato cha kwanza 2013 50% waende wasiojua kusoma na kuandika, halafu muache umma utaamua tu, wala msijisumbue na lolote, poleni sana .
Mkuu hapo unaweza kuwa sahihi na pia unaweza kosea sana. Watoto wa hao viongozi hawatakosa elimu nzuri. Tena utakuwa umebariki dhamira zao, wanataka wao na watoto wao wapokezane uongozi wa nchi daima. Watu wengine wote wabakie na 'zidumu fikra zao'. Chunga hilo Mkuu.
 
kwa hiyo mnawashauri waalimu waanzishe mgomo baridi.
ccm hawana cha kupoteza ili mradi wawaone shuleni,mpaka sasa kulikuwa na mgomo bubu ndo maana std 7 walifaulu huku hata jina hawawezi kuandika.
 
asubiri sasa kuvuna alicho patanda,tunachemsha mbegu kisha twaenda panda ili landlod akavune! Shwaini!
 
Halafu leo nimemsikia waziri wa elimu akilidanganya bunge kuwa walimu wanadai nyongeza ya mshahara na allowance za mazingira magumu nk. Madeni ya malimbikizo na uhamisho na mengineyo yameshalipwa. Huo ni uongo kwani hata mimi ni mwalimu na ninadai malimbikizo yangu pamoja na walimu wengine wengi ninawafahamu pia wanadai malimbikizo
Hapa walimu wanachopaswa kufanya ni kesho kureja kazini, na Jumatatu ijayo kuipa tena serikali masaa 48 ikiwa hawajalipwa hayo kwenye red, Jumatano tarehe 8/8 wagome tena hadi kijulikane (ikiwa na hapo hawataambiwa mgomo haukuwa halali kwa kuwa 8/8 si siku ya kazi - Nyambaffffffff!!!).
 
nilijuatu kuwa hukumu iliyotolewa itakuwa hivyo tulisha pata taarifa toka jana kupitia kwa rais
 
Kama mahakama imesema saa 48 zililikuwa siku za weekend, wamesahau kama mahakama hiyo hiyo ilifanya kazi siku ya jumapili ktk kuuzuia ule mgomo wa walimu wa kwanza? kwa maana hiyo lile pingamizi la siku ya jumapili lilikuwa BATILI.

mwanasheria wa CWT naye alikuwa mpumbavu tu
 
ndugu yangu tatizo ni zaidi ya ccm, NI MFUMO!mfumo huu hata kije chama gani bado mwalimu atabaki kuwa daraja la chini YANAHITAJIKA MAPINDUZI YA MFUMO!
ondoa ujinga wako wewe!ccm wakitoka na mfumo mzima wa uendeshaji nchi utabadilika,including kueta ulinganifu wa maslahi kwa kada zote kwa vigezo vinavyopimika.
 
Hakuna ujanja, Tunarudi Kazini. Kikubwa "MESSAGE SENT" na tutaendelea na mgomo wa aina ya pili, na madhara yake yatakuwa ya muda mrefu. subirini, mtaona.

Nasikia mgomo wa pili ni kwenye sensa? eti ni kweli walimu wamepania kuihujumu sensa, ili kumalizia hasira zao huko?!
 
ondoa ujinga wako wewe!ccm wakitoka na mfumo mzima wa uendeshaji nchi utabadilika,including kueta ulinganifu wa maslahi kwa kada zote kwa vigezo vinavyopimika.

hakika ni mjinga maana walimu wenyewe waliotufundisha waanaendelea kufundisha ujinga kutokna na mgomo wao baridi,na ndio maana pia sikioni chama mbadala na kwa sababu hiyo mapinduzi sahihi ya mfumo hayapo kwa kuiondoa ccm madarakani isipokuwa kwa mimi na wewe kubadilika na kuliondoa taifa la wajinga na kuanzisha taifa la weledi.
 
Nasikia mgomo wa pili ni kwenye sensa? eti ni kweli walimu wamepania kuihujumu sensa, ili kumalizia hasira zao huko?!

Hayo yote tisa, kumi ni 2015!!! Watakoma!!! Hasira zote zitaishia hapo, labda watuletee T-shirt za Maisha bora kwa kila mtanganyika.
 
Pole km ulitegemea Mahakama ikupe jibu ulilokuwa ukisubiria... Bora ungeenda kujisomea mbinu za kudhibiti shinikizo la moyo uzeeni, ujiandae na njia za ku-cope na disappointments za ukawaida maisha kwa kila mtanzania!!
 
Hivi ule mgomo wa TUCTA wakati wa Mgaya ulizuiwa vipi na mahakama siku ya Jumapili usiku? Mbona serikali ilipeleka pingamizi siku ya mapumziko na uamuzi ukatolewa?
 
Natamani kuondoka TZ lakini uwezo sina, maskini mie! Haki iko wapi?

Mkuu wewe una hatari sana kwa hasira uliyonayo utakuja kumpasua mtu nazi. Ila inaboa sana, nina hasira na mambo yanavyopelekwa kisanii hapo tz. Badala ya viongozi kutafuta suluhisho la kudumu wanaishia kutisha watu na kutoa majibu mepesi kana kwamba wananchi ni watoto. Naelewa unavojisikia na tupo wengi kama wewe
 
Back
Top Bottom