Hukumu Kesi ya Mgomo wa Walimu: Mgomo ni batili

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,545
550
Hukumu itasomwa saa nane napiga jaramba nitakuwa nawajulisha live

Updates: Amesema wakati wa kupiga kura labour officer hakuwepo, pia mgomo hawajasema utaisha lini na hivyo mgomo ni batili warudi kazini. Hii ni mara nyingine mahakama zinapendelea serikali na inadhihirisha madai ya Lissu kuwa serikali inateua majaji dhaifu siku hizi ili wazitumie kukandamiza haki za raia

......................
UPDATE
........................
Taarifa nilizozipata hivi punde zinasema mahakama imezuia mgomo wa walimu na kati ya sababu ni
1. Notisi ya saa 48 ilikiuka masharti, ilitakiwaitolewe katika siku za kazi
2. Suala la walimu na serikali bado lipo CMA, hivyo ni mapoemasana kuamua kugoma
Mahakama leo imetengua mgomo wa walimu uliokuwa ukiendelea nchi kwa madai kwamba mgomo siyo halali
mahakama pia imeiamuru CWT kuwalipa fidia wanafunzi walioathirika na mgomo wa walimu
 
Sasa hukumu itakuwa na jipya gani??maana JK ameshasema hawana uwezo na yale masaa yaliangukia week end kwa hiyo mgomo batili warudi meza majadiliano wakaendelee kupotezeana muda!!hakuna jipya hapo!!
 
CCM nao wanashangaa kwa nini wako madarakani,
Walisha shindwa kuiongoza chi siku nyingi zilizo pita,
watanzania bado tunawaamini tu.
 
Tunasubiri Mkuu Japo Mwajiri lazima ataibuliwa kidedea as Usual....Ndiyo maana JK jana alisema tusubiri kesho.Mgomo haukuwa halali na kwa amri ya mahakama walimu wote watakiwa kurudi kazi bila masharti yoyote.Ni mtizamo/wazo:loco: tu wadau!
 
Raisi wenu ndo huyo anasema eti walimu hata mkigoma sistuki maana najua mkirudi kazini mtakuta kazi zenu zenu zote zinawasubiri na syllabus inawasubiri mkave hata hivyo siwezi kuongoza nchi kwa kulipa mishahara tu mambo mengine niendesheje? Je wewe unadhani hiyo ni point na walimu wnaweza kuichukuliaje< waendelee na mgomo au wajirudie tu kazini wakaendelee na kazi kwa ongezeko la asilimia 14% ambayo wala hatujui kama ni kweli atatoa!
 
Huyo Rais wetu kiboko sana kila kitu anachukulia kawaida, Wafanyakazi aliwajibu hivi hivi siku ya uchaguzi akawalamba miguu na Walimu komaeni atakuja kuwaomba msamahaa
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom