Ndio maana nakubaliana na Tundu Lisu! Tusipobadilisha namna ya uteuzi wa majaji hatuwezi kuleta mageuzi ya aina yoyote katika utoaji wa haki nchini. Haiwezekani mteule wa Rais, mara nyingi kama zawadi, atahukumu dhidi ya Rais! Wanatuambia mahakama iko huru na Jaji anamua kwa uhuru. Lakini haitoshi tu kusema hivyo, ni lazima ionekane kuwa Jaji yuko huru kuamua. Kwetu hapa Jaji aliyekuwa "handpicked" na Rais, kwa kufuata vigezo visivyo wazi, haonekani kuwa huru kuamua kesi ambayo Rais ameiongelea jana. Ndio maana hiyo ruling yake ina reasons zile zile alizotoa Kingkwete jana - notice ya 48 hours ili-include Saturday na Sunday. Sijui, kati ya Jaji na Rais, nani amekopi kwa mwenzake.