hukumu kesi ya Chenge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

hukumu kesi ya Chenge

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by quimby_joey, Dec 29, 2010.

 1. quimby_joey

  quimby_joey JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 361
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Wanajamvi naomba mwenye taarifa kuhusu kesi ya Chenge aniarifu
   
 2. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Ametozwa faini ya laki saba na ametoa papo hapo!!!! Hivyo yuko huru kuua tena na kuendesha gari bila insurance. Shame on Tzs laws/procedures.
   
 3. tone

  tone Member

  #3
  Dec 29, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo KALI.......!!!!!! mwanangu namimi cjui nikaue nione nitatozwa Tsh ngapi....!???

  Kweli watanzania tumeishiwa Mitazamo hata matendo yetu,,, Kwishney
   
 4. M

  Mkwele JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bongo kuna wengine sheria haiwabani, lkn sheria inasemaje kwa dereva anayesababisha kifo kwa kumgonga mtu ? Naomba ufafanuzi kwa wanaojua sheria.
   
 5. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2010
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Sheria inayohusu kosa la kuendesha gari na kumgonga mtu na kufa ni kosa linalohusu makosa ya barabarani au traffic case. Sheria zilizopo kwa kesi za traffic ni za kichekesho saana, unaambiwa adhabu yake kwa kosa la kugonga mtu na kuua haizidi faini ya shilingi laki moja au kwenda jela miaka miwili. Chenge kutozwa faini ya laki saba bado inaonesha kama hakimu kamkomoa vile. Kwa sheria kama zilivyo kwenye vitabu adhabu ni ndogo saaana. Ndio maana madereva wetu wa daladala hawajali saana kufanya makosa hata kugonga watu na kuwaua, sababu adhabu zake nyingi ni za faini na ukikosa faini ndio unafungwa. Unless kama sheria ingebadilika na adhabu kuwa ya kifungo tu bila faini labda mauaji ya kugongwa na magari barabarani yangepungua. So kwa Chenge kulipa faini tusimlaumu hakimu na wala hakuna mchezo mchafu wowote hapo bali ni sheria zetu ziko weak saana kwa makosa ya barabarani.
   
 6. M

  Mkwele JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Babayah67 asante kwa kunijuza, kumbe waungwana wengine wanataka mtu afungwe hata kama sheria haisemi hivyo.
   
 7. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #7
  Dec 29, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hapo ndiyo utaona umuhimu wa kubadilisha sheria zetu!!
   
 8. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #8
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Damu ya mtu haipotei hivi hivi.
  Damu ya hao marehemu itamhukumu Chenge!
   
 9. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hayo mnayoyasema ni ya kweli kwamba katozwa faini ya sh. Laki saba? Maana mini sina habari zozote. Lakini kama sheria ndivyo inavyosema hakuna mjadara labda mjadara uwe ni kubadiri sheria ili wahusika waswekwe rumande maana hata faini ikiongezwa sidhan kama thamani ya pesa inaweza kulinganishwa na uhai wa mtu.
   
 10. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #10
  Dec 29, 2010
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  ... hiyo imekaa zaidi ki imani kuliko kisheria. Kisheria Chenge anahatia na kapigwa faini na kwa kuwa anajua fika sheria ilivyo akajiandaa kabisa na pesa ya kulipa, maana kama asingekuwa na pesa ya kulipa angepelekwa jela. Hivyo hata yeyote mwingine ikitokea una kesi na leo ndio siku ya hukumu basi jiandae hasa kipesa ya kutosha ili ukiambiwa ulipe faini basi hapohapo unalipa, maana ukichelewa tu kulipa kaka/dada unapelekwa lupango!!!
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Dec 29, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,515
  Likes Received: 19,937
  Trophy Points: 280
  angeenda lupango
   
 12. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #12
  Dec 29, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Give me a break. Lazima alijua hukumu ya kesi na aliambiwa atatozwa faini hiyo si kwa kuwa anajua sheria tu. He knew he can buy his freedom. Kuna justice ya mahakama na ya Mungu, sasa tumuache Mungu afanye kazi yake.

  So tusubiri keshi nyingine kama hizo tuone kama hukumu zitakuwa hivyo....
   
 13. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #13
  Dec 29, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Hawataishi milele, na Mungu wangu anasema mwisho wao utakua mbaya kuliko mwanzo wao
   
 14. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #14
  Dec 29, 2010
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,922
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ok, msaada tutani:

  Hivi three yrs in Jail is equivalent to 700,000Ths??
   
 15. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #15
  Dec 29, 2010
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 280
  Mara nyingi ajali hutokea bila kukusudia, hata hivyo kama kuna uzembe wa hali ya juu uliothibitishwa au nia ya kukusudia kugonga kabla ya ajali hilo ni swala lingine lenye kuhitaji adhabu kali zaidi.
  Adhabu aliyopewa inamfanya yeye pamoja na wengine wawe makini wanapoendesha magari au vyombo vingine na haikumaanisha kulipa uhai uliopotea.
   
 16. C

  CheGuevarra Member

  #16
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  But we have not talked about driving vehicle without insurance. Was he convicted as well, because I can see only convicted with reckless driving and causing death! Vipi suala la bima ni hiyohiyo laki 7!! Lazima to review sheria zetu
   
 17. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #17
  Dec 29, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  hapo ndo INAPOKUJA UMUHIMU WA KATIBA MPYA,mtu kafanya kosa kubwa lakini hukumu ya keshi haiendani na kosa.
   
 18. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #18
  Dec 29, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0

  Hivi kama alishindwa kutiwa hatiani kuhusiana na rada na kuwa na vijisenti vyenye utata nje bado kuna watu walikuwa hawajui nini kitatokea katika hii kesi.

  Kifupi hii nchii yetu/yao ina sheria mbili kulingana na class/kundi ulilopo. Ca muhimu fanya analysis ujue uko kundi gani

  Nakubaliana na wewe Sheria zinahitaji review lakini tatizo kubwa la nchi yetu sio kutokuwepo sheria tatizo ni kuzitii na kuzifuata. Hata wanaotoa hukumu wanaangalia kwanza mtu huyu ni nani ndio watoe hukumu. Tatizo tulilonanlo ni la kimfumo zaidi na si sheria.

  Tunawez kuwa na sheria nzuri tu lakini kwa mfumo tulionao kazi tunayo
   
 19. L

  Leornado JF-Expert Member

  #19
  Dec 29, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ndo maana nilikimbia uhakimu TZ manake unashinikizwa kutoa hukumu ambayo wewe mwenyewe dhamira inakusuta. Huyu hakimu maskini atakuwa alipewa maelekezo na mafisadi nini cha kufanya na chenge hiyo huku aliijua kabla. Yaani TZ laws ni kwa ajili ya wanyonge tu. Yaani Chenge uue, uharibu bajaji, uendeshe gari usiku umelewa tena bila insurance hukumu yake unalipa laki saba????
   
 20. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #20
  Dec 29, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  hapo nimekuelewa sana mkuu, ndio maana tunahitaji KATIBA MPYA?
   
Loading...