Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Mgeni akifika Zanzibar, watu wa huku ukiwatizama wanazuga kama hawana tyme nae!

Lakini lazima huwa wanamfuatilia nyuma nyuma kuona anaelekea wapi na ni mgeni wa nani!
Wakishajiridhisha mahala ulipofikia wakikuona tena!!

Utawasikia " Huyu si aishi pale kwa Ariiiiii!!" (Yaani mgeni wa Ally)

Wanawake huku Zanzibar waoga sana kusemeshwa njiani na mtu wa bara, yaani hata ukimsalimia anaitikia kwa sauti ya chini wala hasimami!

Huku Zanzibari;
  • Round about inaitwa (ikipinda) au (mviringo), kwenye daladala utasikia Shusha hapo ikipindaaah! Maana yake shusha round about
  • Huku Zanzibar sufuria linaitwa dishi,
  • Kisima cha maji kinaitwa kisima cha kuvuta
  • Huku hakuna fundi bomba Bali kuna fundi mfereji, ukitaka maji ya bomba inabidi useme unaomba maji ya mferejini
  • Pombe wanaita- moja moto moja baridi
  • Ukitafuta chupi utazunguka sana hupati hadi useme unatafuta HAFU
  • Shule huku zinaitwa skuli
  • Ukitaka kununua chepe/koleo huku hawalijui hadi useme unataka Li-PAULO
Hakika huku Zanzibar ni tabu tupu, nasubiri tarehe 30 nirudi zangu bara!
 
Si afadhali hata wangekuwa wanasema "shusha" sasa, wengi wanasema "tia"! Kuna sehemu inaitwa Dole konda akisema "Dole" anayeshuka hapo anasema "tia", au utasikia n'tie Dole hapo!

Yaani wale maneno mengi wanayoyaongea ukiyaleta kwa tafsiri ya bara unakuta ni Matusi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom