Huku sio kudhalilishwa kwa Rais wetu na Media za Nje? Je, watanzania tukubali, Tukae kimya?

Pasco hivi wewe ulisomea wapi uandishi wa habari?
Wewe ni mwandishi kweli? na Kama ni mwandishi mbona hujui lolote kuhusu taaluma ya habari? au utangazaji wa TV ni tofauti na uandishi mwingine?

Ni wapi Rais kadhalilishwa ?kuchorwa katuni ndo kudhalilishwa? hapo ajabu iko wapi? katuni aliyochorwa imeenda sambamba na tukio, yaani kauli yake dhidi ya watoto wa kike kupewa mimba, na ktk hilo kila media ina mtazamo wake.
Wewe ulitaka media zote hadi za nje ziandike habari hiyo Kama gazeti la Uhuru? pasco umezidi kujipendekeza, hata Kama ni njaa hiyo yako imezidi bro...
 
...
Nilishangaa sana kuona hata VP ambaye ni mwanamke, Naibu Spika ambaye ni mwanamke walishindwa hata kutoa kauli kuhusu hili la mimba.

Again, as usual in Africa when we eat we don't talk!

Masanja hili la mabinti shuleni kupata mimba ni la kukemea siyo tu kwa nguvu zote ila kuchukua hatua kali kwa wote wawili (binti na aliyempa mimba).

Ni mimba ya utotoni, ambayo sheria yetu ya Makosa ya Kujamiana (1989) inakataza. Na pia kuruhusu ni sawa na kuhalalisha ndoa za utotoni, kinyume na Sheria ya ndoa (1971).

Masanja, mkuu, nadhani hujapata kuwa na binti au wa ndugu/rafiki aliyepata mimba ya utotoni, tena akiwa shuleni. Msongo wa akili anaoupata ni mkubwa sana kuliko wa kubakwa, kama hakupenda au kupanga apate uja uzito. Binti kama huyo, kamwe hawezi kuwa na maendeleo mazuri, katika mkondo wa kawaida wa elimu.

Hili la vyombo vya habari, vya nje ya nchi, kumwandika vibaya Rais, Paskali ametoa ushauri sahihi kwa Wizara husika kulishughulikia. Hicho ndo tunachoweza kufanya sisi wanajamvi na kuwaasa hao Waandishi wa Habari kushughulikia ya kwao huko, na ya Ngoswe watuachie. Kama kuna WaTz wanawafadhili,wakigundulika wafikishwe kwenye vyombo husika.
 
Kusemwa vibaya na media za nje maana yake nini? Anasingiziwa au anatungiwa uongo? Raia yeyote wa dunia anaweza kusemwa popote na yeyote hapa duniani mradi tu asitungiwe uongo, ambao hata inamlazimu yeye mwenyewe kujisafisha. Watu husema jambo alizualo mtu alitetee, alisimamie na kulimaliza mwenyewe
 
Ulivoandika nikajua labda wamemtukana au kumdhalilisha nje nje kumbe ni mtu tu anaexpress opinion zake kuhusu mimba za watoto wa kike? Hujui maana ya Opinion & Editorial section ya gazeti?
Issue ya mimba za watoto wa kike sio issue ya ndani ya Tanzania hiyo ni issue inayowagusa wanadamu wote na Tanzania is a sovereign state existing within a family of nations lazima kitu kikitokea Tanzania kijadiliwe na wengine.
 
Mkuu hili swala kila mtu ana namna anavyoliona. Na kwa vile Mkuu wa Kaya keshatoa tamko..amehitimisha mjadala. Kama tungekuwa na bunge la maana (achana na hili ambalo ni useless na ndiyo mzee), we could have our efforts directed through the bunge. Kupitisha sheria (hata kama JPM angekataa kuipitisha), lakini atleast angejua kwamba people are not with him kwenye hili.

Nilishangaa sana kuona hata VP ambaye ni mwanamke, Naibu Spika ambaye ni mwanamke walishindwa hata kutoa kauli kuhusu hili la mimba.

Again, as usual in Africa when we eat we don't talk!
Acha maneno ya kebehi kwa Serikali.Tumesoma shule za Serikali na hakuna sheria inayoruhusu mwanafunzi kusoma akiwa na mimba au baada ya kujifungua arudi shuleni alikokuwa anasoma!

Ila wengi wamepata mimba na kufukuzwa shule na baadaye wamesoma kwa njia zisizo rasmi. Hapo sio Marekani ambako Watoto wanasoma na mimba na Hata baada ya kujifungua ataendelea na shule.

Mtoto wangu mwenyewe darasani kwao grade 11 wako wanafunzi 4 wajawazito na wanasoma kwasababu sheria zinawaruhusu huko USA.
 
Hata kama sikubaliani na kauli yake. Hayo wanayosema huko nje hanihusu saana has a kwenye hiyo kumsema vibaya.
Kama nikusema tu. Kwenye issue hii, who cares, waache waseme, sisi tunaendelea na yetu
 
Paskali,

Kosa la magufuli sio kuwa against na mimba za utotoni, hata wanaosema hawa watoto warudi mashuleni, wasingependa mabinti zao wapate mimba. same way wanaouza na kutumia ARVs wasingependa kupata HIV at will.

kuwarudisha shule hawa watoto kwenye other setting and circumstencase ni kama insurance policy, you can choose to have it or choose to ignore it.

Mtu kama huyu ukimwambia awe na life insurance atakuambia itanichulia, as if hatakufa. lakini akinunua gari mpya mwepesi kabisa kuiwekea comprehensive insurance.

Gap lililokuwepo ni ELIMU. mheshimiwa hana uelewa wa kutosha kuhusu umuhimu wa elimu kwa kila mtu hasa mtoto wa kike. hakuna ulazima wa kufunganisha elimu na mimba, one can have both.

Mheshimiwa angenyamaza, sio kila jambo linahitaji kauli. sio kila battle inahitaji fighting. some battles are meant to be lost to win the war. Huyu wetu anataka kuwin every single damn battle, just to service his ego.

Media zinachofanya ni kutumia obvious BLUNDER from his side, to sell their papers, you can not FAULT THEM in that. You may not like what they write, but mheshimiwa picked an unnecessary battle that is costing him the war.
 
Acha ujinga wako na maneno ya kebehi kwa Serikali.Tumesoma shule za Serikali na hakuna sheria inayoruhusu mwanafunzi kusoma akiwa na mimba au baada ya kujifungua arudi shuleni alikokuwa anasoma!

Ila wengi wamepata mimba na kufukuzwa shule na baadaye wamesoma kwa njia zisizo rasmi.

Hapo sio Marekani ambako Watoto wanasoma na mimba na Hata baada ya kujifungua ataendelea na shule.

Mtoto wangu mwenyewe darasani kwao grade 11 wako wanafunzi 4 wajawazito na wanasoma kwasababu sheria zinawaruhusu humo USA.
Wewe Kwani hizo sheria za kumkandamiza mtoto Wa kike haziwezi kubadilishwa?
 
Pasco hivi wewe ulisomea wapi uandishi wa habari?
Wewe ni mwandishi kweli? na Kama ni mwandishi mbona hujui lolote kuhusu taaluma ya habari? au utangazaji wa TV ni tofauti na uandishi mwingine?
kifupi wewe pasco ni mbumbumbu mkubwa Sana wa taaluma ya habari.
Ni wapi Rais kadhalilishwa ?kuchorwa katuni ndo kudhalilishwa? hapo ajabu iko wapi? katuni aliyochorwa imeenda sambamba na tukio, yaani kauli yake dhidi ya watoto wa kike kupewa mimba, na ktk hilo kila media ina mtazamo wake.
Wewe ulitaka media zote hadi za nje ziandike habari hiyo Kama gazeti la Uhuru? pasco umezidi kujipendekeza, hata Kama ni njaa hiyo yako imezidi bro...



hebu kaa utulze kichwa umsome mwanzzo mwisho utamwelewa kasmamia upande gan! pole
 
Kule wanajielewa ... ingekuwa tanzania lingefungwa..maana ccm na watu kama mayalla huwa wanaanzisha nyuzi za kushauri kufungiwa gazeti...watu wana uhuru...hii maada kwa wenzetu itachekwa
 
Back
Top Bottom