Huku ni kunitega au kunijaribu

Huku ni kunitega au kunijaribu

Mimi Niliishi maisha ya Mateso Sana shule ya msingi dhidi ya Walimu. Ila baadae nilipofaulu nilifuta hiyo kauli ya kuteswa na kuwa kufundishwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habarini wakuu, niende kwenye lengo husika, nakumbuka nikiwa shule ya msingi darasa la sita kuna madam mmoja alikuwa ananifuatilia sana kila akiniona lazima ataniita na kuanza kujisemesha Fulani Leo mbona umechafuka hivyo hujachomekea, shati hujanyoosha na mambo mengine mbalimbali.

Nilimzoea sana kwa maneno yake ikafika mahali nikienda ofisini kupeleka daftari kama hakuna walimu ananiita nikae pembeni yake na kuanza kunihoji maswali ya hapa na pale kuhusu somo lake, kisha naondoka nilichukulia kawaida sana wala sikuumiza kichwa kuwaza kingine kiumri nilikuwa mdogo.

Siku moja aliniita na kuanza kunisifia Fulani Leo umependeza sana punguza Michezo usichechafuka kama watoto wengine napenda nikuone ukiwa msafi muda wote nikamjibu sawa mwalimu, akiwa na walimu wenzake hanisemeshi anapita kimya kimya nilikuwa nikishangaa kwa nini madam Leo hujanisemesha wakati huo nimetoka kucheza mpira na kuluka salakasi vumbi mwanzo mwisho.

Nakumbuka ilikuwa siku ya mtihani wa kufunga muhula darasa la sita mwezi wa kumi na mbili somo la kiswahili madam kaja kusimamia, nilikuwa nimekaa na rafiki angu saizi ni msanii wa bongo fleva tumekaa upande wa katikati dawati la nyuma, madam akaja upande niliokaa Mimi akasimama kwa muda sana kama mtu mwenye wasiwasi mwingi akiangalia huku na huku anaenda mbele kidogo analudi nyuma tena akifika nilipo kaa nashindwa kuandika naanza kutetemeka nilikuwa sipendi kusimamiwa kalibu na mwalu wakati nikiwa kwenye mtihani.

Baada ya muda madam akasogea taratibu akaegemea ukuta kisha akaniponda chaki kichwani nikajikausha kama vile sikuona akaniponda nyingine nikainua kichwa kumtazama, hahaha nilishangaa madam ameshika karatasi kwa upande yenye majibu ya kiswahili moja mpaka hamsini, akaniambia kwa ishara andika haraka, mwanaume sikuchelewa nikajipinda kuandika majibu yote, baada ya kumaliza madam akaondoka kaenda kukaa mbele kwenye kiti, baadhi ya wanafunzi wenzangu walishitukia na jamaa angu aliona ule mchezo, nae nikampatia majibu ya maswali 44 tu mengine nikamdanganya tusije fanana hakuwa na uwezo sana darasani mwalimu wa somo asije shitukia.

Kwa kuogopa kupata 50 ya 50 nikajikoshesha maswali mawili kitu ambacho nilifanya kosa kubwa sana, mwanafunzi mmja wa mkondo A alipata 49, na Mimi 48 sikuongoza katika somo hilo, iliniuma sana madam akaniita akaniuliza Fulani imekuwaje nikamwambia nilichanganya wakati naandika, akasema sawa siyo mbaya lakini tokea hapo madam akaenda masomoni tukamaliza shule sijawahi kumuona tena mpaka leo, swali nalojiuliza alikuwa ananitega au alikuwa ananipenda kama mwanafunzi wake lakini kwanini alinipa majibu peke angu na kunifuatilia kila mala, sijawahi pata majibu kwa kweli, ebu ndugu zangu mniambie hii ilikuwa kunitega ama, nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
I guess we all had that kind of teacher during our school days

So usimsome mwalimu vbaya inatokea tu kawaida hio mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi alikuwa ananipa mavyakula kabisa. Chocolates na keki kwa sana, ila nae hakudumu aliondoka.
 
Kwa kweli sikuwa nikimuelewa aiseee. Nilikuwa mdogo sana alinipenda alikaribia kuwa chizi maana kila dakika huyu.
Vivyo hivyo hata Mimi sikumuelewa alikuwa ana lengo gani kwa sasa huwa najiuliza alikuwaga anataka nini Yule madam na kipindi kile alikuwa hajaolewa alikuwa ni binti sema ndo hivyo yeye alikuwa na ajira

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sometimes a person is just that, nice. Sure they'll go the extra mile for you at times but that doesn't mean anything.

Don't read too much into things.
What a wise comment!
Few people have got this abundance of wisdom.
 
Back
Top Bottom