huku ndiko tunakoelekea wakuu!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

huku ndiko tunakoelekea wakuu!!!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by jamiif, Oct 1, 2012.

 1. jamiif

  jamiif JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 2,417
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Miaka michache ijayo, ibada zitakuwa kama ifuatavyo.

  MCHUNGAJI: Bwana asifiweeeee!

  WAUMINI: Ameeeeeeeeeni!

  MCHUNGAJI: Tafadhalini washarika sasa tuchukue iPad, tablet PC, simu na kindle zetu ili tufungue 1 Wakorintho 13:13. Pia washeni
  bluetooth zenu ili muweze kupokea mahubiri. Mnaotumia facebook, twitter, BBM na Whatsapp mnaweza kuendelea kupokea mahubiri haya. Tafadhalini washarika mnaweza kutumia Wi-Fi ya kanisa kwa uhuru kabisa kwa kutumia nywila ya IMANI613. Haleluuuuuuuyah!

  WAUMINI: Haleluuuuyaaaaaaaah!

  MCHUNGAJI: Wapendwa washarika sasa ni wakati wa sadaka kwa hiyo kadri ya itakavyokupendeza kumtolea Mungu unaweza kutumiacredit ama debit card, pia unaweza kutoa sadaka kwa njia ya MPesa, Tigopesa, Airtel money ama ZPesa kupitia namba zinazoonekana kwenye skrini.

  WAKATI WA MATANGAZO
  KATIBU WA USHARIKA: Wapendwa washarika wiki hii kutakuwa na mikutano ya kiroho kupitia group letu la Facebook. Mada kuu itakuwa uponyaji wa kiroho kwenye ndoa. Washarika wote mnakaribishwa kushiriki.

  Siku ya Alhamisi kutakuwa na mafundisho ya Biblia moja kwa moja kupitia Skype kuanzia saa moja jioni. Tafadhali msikose kushiriki. Pia mnaweza kuendelea kufuatilia ibada hii pamoja na mafundisho yote kutoka kwa mchungaji kupitia akaunti yake ya Twitter.
   
 2. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  ehee hii kali.
   
 3. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  kulikoni mzee hadi ukafikiri tutafika huko?
   
 4. mathematics

  mathematics JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 3,291
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Hahahahaha, nimecheka sana
  cons na pros za teknolojia,
   
 5. jamiif

  jamiif JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 2,417
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  mambo ya utanzawazi hayo ndugu yangu maana siku hizi kila kitu mambo ya digital!!
   
 6. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #6
  Nov 5, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  kweli bwana haya yanatokea nilikuwa nasikiliza mchungaji anawahamasisha waumini kuchangia michango ya kanisa akawaambia sasa mnaweza kutuma kwa tigo pesa m pesa au airtel money. nikakumbuka sana hii thread yako.
   
Loading...