Huku kwenye social media kuna mambo huku

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,272
Kwa sisi tunaotumia majina yetu na CV zetu halisi tumeweka wazi, humu ndiyo connections zinapoanzia unakuta linked link, kuna anaekuhitaji akiona CV anakuunganisha mara umepata mchongo.

sasa kuna wale anakuona jina lako anakumbuka mlisoma wote Wailes, ana request friendship, unamuona ni Queen nani nani amesoma Havard, mmh ukifikiria Queen nilikutana nae wapi mimi, Havard sijawahi kusoma mimi.

mkikutana siku moja kwenye ngoma ya kumtoa mwari anaanza Sky wewe umenichunia huni accept kama rafiki, wewe si Mercy wewe umeniomba lini urafiki.

anajibu mimi ndiyo Queen bwana ni accept ili tuwe tunachat. Khaa Mercy ulisoma Havard unaambiwa kauka mjini hapa.
 
sio huku tuu hata mtaani watu tupo hivyo, unaweza kuta mtu anachukia kuchimba choo akiwa mbele ya kadamnasi lakini yeye ndio mchimbwa choo, mtu anatoa misaada lakini ni mtoa kafara mzuri, kuna watu humu wanajifanya ni wema lakini huko kwake anayafuga majini yote unayoyajua na usiyo yajua, mwingine anacheka usoni huko ndani anaungua yaani ukijichanganya tu kapita na wewe.

Kwahiyo dada yangu hii hulka ya kuficha mambo si ktk mitandao tuu ndio sehemu ya maisha yetu, Mimi ukaja Kwangu/kwetu ukauliza hilo jina kila mtu atashangaa hata kama ni mm mwenyewe ndio nimekuelekeza lakin utaambiwa mtaa huu hakuna mtu mwenye jina kama hilo, nna jina langu mwenyewe la kilugha linatambuliwa mpaka na mizimu ya babu..kingine huku si mahala salama sana kwa kuweka wazi kila kitu chako unaweza kutusua ama likawa ndio anguko lako.
 
Watu wanageuza linked in kua instagram, ile ni sehemu ya kazi tu sio kupiga story.
 
Hujamalizia story. Kila mtu kwenye social media ni; tajiri,anasukuma jaguar tu,shopping Paris,kula hoteli za nyota tano,maji ya kunywa na kuoga imported from London,amesoma Oxford,shule ya msingi IST (siyo vile vigari vyetu), o-level kasomea Washington DC, ameoa/ameolewa na beatiful/handsome.

kila mtu anamuhogo/ mnato, hakuna mwenye kibamia/ bwawa, kila moja anakula/ analiwa na watu classic, kila mtu anajua kukojoza kwa style isiyo ya sayari hii, choo wanatumia vya kutoka Japan, hospitali anaenda za Marekani, hanunui used goods bali new brands.

kila mtu mjuaji/anajua kila kitu,kila mtu ni mchambuzi wa mambo nyeti,hakuna kilaza,wote wasomi,hakuna asiyemiliki usafiri wa nguvu,kila mmoja anapiga vinywaji classic kutoka Italy,kila mmoja anahudhuria mechi za soka live za Barcelona/ Manichester United na Liverpool/ Juventus,michango kwa jamii wanayotoa ni kuanzia milioni tano.

kila moja anapata mialiko kutoka kwa Bakhresa na Mo Dewiji,kila moja akienda kwa mchepuko na asitoe za matumizi na kuzuiliwa kwa nguo zake kulowekwa kwenye maji na asionekane siku 2 ametekwa,hakuna msema uongo/mchochezi bali ni ukweli daima,kila mmoja anamiliki mijengo sehemu mbalimbali za dunia,kila moja anapiga picha maeneo classic,kila moja anaishi ushuani,kila mmoja mapumziko yake ni kwa Madiba (Port Elizabeth) nk, nk, nk, nk, nk.

Hongereni sana wana social media.Sisi wa uswekeni ngoja tubaki uswekeni kwetu tu kama kawa.

Lakini Mungu anatuona na kutushangaa tunavyojikweza wakati wengi wetu vipato vya kujikimu kila siku vinatusumbua.

Sio naibeza mitandao ya kijamii kwa faida zake,bali nazungumzia tabia za sisi watumiaji wa mitandao hiyo.

Hahahaha,Sky Eclat nimeongezea nyama kwenye stori yako.Hukumalizia yote,haraka ya nini?Au ulikuwa unawahi kukata gogo?
Sky Eclat,

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom