Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,231
- 113,608
Katika ulimwengu mdogo wa kiJF hasira iliyopo ni dhahiri.
Hata uwe kipofu kama Stevie Wonder huwezi kushindwa kuiona.
Na kama wigo wa ulimwengu wako ni theluthi mbili ya maisha yako basi huenda ukadhani nchi nzima sasa hivi gumzo lililotawala ni kukamatwa kwa bwana Mubyazi [Max].
Je, huko Mlalakuwa, Makonde, kwa Aziz Ali, Mabatini, Buzuruga, Dumila, kwa Stella Matituta, Kijitonyama B, kwa Ali Ma-Flower, Mwenge magengeni, Ubungo, Tabata, Banana, Kishapu, Kichangachui, na kwingineko ambapo wewe mdau upo, nako kukamatwa kwa huyu jamaa yetu ni gumzo la kitaa?
Au ni gumzo tu humu humu kwenye ulimwengu wetu wa kimtandao?
Manake wakati mwingine ukichukulia kwa maanani yajiriyo humu unaweza kudhani kilichobamba humu ndicho hicho hicho kilichobamba na kitaa kumbe wapi.
Huko mlipo nini kilichobamba?