Huko kitaa niaje?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
86,641
2,000
Katika ulimwengu mdogo wa kiJF hasira iliyopo ni dhahiri.

Hata uwe kipofu kama Stevie Wonder huwezi kushindwa kuiona.

Na kama wigo wa ulimwengu wako ni theluthi mbili ya maisha yako basi huenda ukadhani nchi nzima sasa hivi gumzo lililotawala ni kukamatwa kwa bwana Mubyazi [Max].

Je, huko Mlalakuwa, Makonde, kwa Aziz Ali, Mabatini, Buzuruga, Dumila, kwa Stella Matituta, Kijitonyama B, kwa Ali Ma-Flower, Mwenge magengeni, Ubungo, Tabata, Banana, Kishapu, Kichangachui, na kwingineko ambapo wewe mdau upo, nako kukamatwa kwa huyu jamaa yetu ni gumzo la kitaa?

Au ni gumzo tu humu humu kwenye ulimwengu wetu wa kimtandao?

Manake wakati mwingine ukichukulia kwa maanani yajiriyo humu unaweza kudhani kilichobamba humu ndicho hicho hicho kilichobamba na kitaa kumbe wapi.

Huko mlipo nini kilichobamba?
 
Wong Fei

JF-Expert Member
Apr 13, 2016
3,931
2,000
kilichobamba mtaani, ni tamko la Ndalichako kutoajiri walimu wa sanaa.
Kila mtu anaisoma namba kimpango wake.
Na ww jiandae kwa makosa ya kimtandao. Tenga milion 7 kabisa. Maana TRA wanahasira sana. Hii issue ikivuja. TWAFAAAAAAAAAAAAAAAA
Me nipo Silali (Mara) huku, muda wwte nazamia Kenya
 
QUIGLEY

JF-Expert Member
May 23, 2015
27,680
2,000
Ngoja waje wakitaa, binafsi muda kupata habari za kitaa ni mdogo sawa na hakuna
Katika ulimwengu mdogo wa kiJF hasira iliyopo ni dhahiri.

Hata uwe kipofu kama Stevie Wonder huwezi kushindwa kuiona.

Na kama wigo wa ulimwengu wako ni theluthi mbili ya maisha yako basi huenda ukadhani nchi nzima sasa hivi gumzo lililotawala ni kukamatwa kwa bwana Mubyazi [Max].

Je, huko Mlalakuwa, Makonde, kwa Aziz Ali, Mabatini, Buzuruga, Dumila, kwa Stella Matituta, Kijitonyama B, kwa Ali Ma-Flower, Mwenge magengeni, Ubungo, Tabata, Banana, Kishapu, Kichangachui, na kwingineko ambapo wewe mdau upo, nako kukamatwa kwa huyu jamaa yetu ni gumzo la kitaa?

Au ni gumzo tu humu humu kwenye ulimwengu wetu wa kimtandao?

Manake wakati mwingine ukichukulia kwa maanani yajiriyo humu unaweza kudhani kilichobamba humu ndicho hicho hicho kilichobamba na kitaa kumbe wapi.

Huko mlipo nini kilichobamba?
 
Mwingereza

JF-Expert Member
Jan 21, 2014
886
1,000
Hali ni tete aisée. Mimi ni mwana matako bar. zamani kupat kitt ilikuwa inachukua dakika 15 hadi 20. yaani panajaa balaa, watu siyo chini ya 80 had 200. sasa hivi ni watu 4 au 5 wakiwa wengi
 
Hamis Juma

Verified Member
Nov 4, 2011
2,221
2,000
Tangazo la Ndali kuhusu ajira
Kuna mzee hajaenda shule, nimekuta analalamika kamaliza namba zote japo kwa kuelekezwa, mtoto aliemlea kwa kuuza miwa alisoma sanaa na kazi hakuna na ana wengine kibao hakuwapeleka shule. Mtaani kwetu hilo ndo linabamba
 
Yohana Kilimba

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
8,116
2,000
1% ya watz ndio ipo humu!
Hao waliobakia wako nje uko!
Na kati ya hao 99%,almost 50% wako kijijini,na hawa ndio wanaongoza kwa ujinga,ila bahati mbaya au nzuri,hawa ndio wakulima na mwaka huu Magufuli aliwakingia kifua wakapata bei nzuri ya mazao yao!kanda ya ziwa watakuwa mashaidi zangu wazuri!
Labda upepo utabadilika kama mvua ikikataa mwaka huu na 2017 wakapata njaa na Magufuli akatekeleza agizo lake la kutowapa chakula cha Misaada!
Kule kusini korosho imeuzwa kwa 4000/=, Baada ya Magufuli kuwakingia kifua!
Labda ugonjwa uue mikorosho na ukame ukaushe pamba,ila ukiendelea hivi,Magufuli hana mpinzani!
Hawa asilimia 49 ni wafanyabiashara walio mjini,hawa ni maadui wa Magufuli!kifupi hana kura baada ya Mikodi mini isiyo na tija!
Kwahyo mpaka sasa Matokeo ni:
MAGUFULI 50%,50% wape wapinzani,na hapo bila TUME Wala Polisi!
 
Mr Dumila

JF-Expert Member
Jun 3, 2016
251
500
Huku DUMILA tumechukia sana na tunatamani 2020 ifike haraka

HATUMTAKI DIKTETA UCHWARA

alianza kwa LEMA
akafuatia kwa BEN
sasa kaingia hadi chumbani(JF)

HATUMTAKI BABA JESKA
 
Mdudu halisi

JF-Expert Member
May 7, 2014
2,730
2,000
Hapa mtaani kwetu tuna kijiwe cha kupashana yanayoendelea hapa nchini kila siku. Kwa kipindi cha wiki tatu zilizopita habari kuu ilikuwa kupotea kwa Ben na kuuawa na kutoswa mtoni kwa wale wahamiaji haramu wa Mwigulu, lakini toka Max akamatwe hatuna mjadala mwingine zaidi ya huo huku mara kadhaa tukitafakari kupotea kwa Ben.
 
ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
7,718
2,000
Hali ni tete aisée. Mimi ni mwana matako bar. zamani kupat kitt ilikuwa inachukua dakika 15 hadi 20. yaani panajaa balaa, watu siyo chini ya 80 had 200. sasa hivi ni watu 4 au 5 wakiwa wengi
Sitaki kuamini kama Hujaelewa Maada inataka nini
 
goodluck5

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
4,045
2,000
Mwaka jana na hata uchaguzi mkuu ujao ilikuwa fursa nzuri kwa upinzani kuchukua nchi
Tatizo timu ya upinzani kwa sasa imetekwa........imezingirwa na mafisi yenye njaa hatari, yakipata mwanya tu nchi itabaki mifupa!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom