Hujuma kwa mstakabali wa Amani, Usalama na Maendeleo ya Taifa letu

Kibunago

JF-Expert Member
Jan 11, 2008
300
250
Kwa vile AMA Chombo husika hakijawajibika ipaswayo kwa mujibu wa Sheria iliyokiunda ya na. 15 ya 1996 hususan sehemu II Ibara ya 5 (1) (d) AU kwa Viongozi waliotangulia kutosikiliza/ tekeleza ushauri wao, leo nateremsha ushauri kwa kutaja mambo ambayo yanatafsirika kuwa HUJUMA (kwa kujua au kutokujua) yatakiwayo kuachwa / kubadilishwa kwa mstakabali wa Amani, Usalama na Maendeleo ya Taifa letu.

Hujuma: 1.
Kutokamilisha Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba ya nchi ni kutowatendea haki Wananchi walioshiriki kutoa maoni; ni kuendeleza manung’uniko yanayofisha Amani yetu na ni kuendelea kuwa na Sheria Mama butu ambayo ina maeneo mengi ya kurekebishwa ili tupate maendeleo stahiki.

Suluhisho: Mchakato wa Katiba Mpya / Yenye Marekebisho ukamilishwe ndani ya Bunge Maalumu (lenye wajumbe maalumu (kila mkoa uwakilishwe na mtu mmoja) tofauti na Wabunge wa Bunge lililopo).

Hujuma: 2.
Kuendelea kufumbia macho matumizi makubwa ya Serikali yasiyo na tija mfano:-

i. Kuwa na Idadi ya Wabunge wengi na wanaojipitishia malipo makubwa kuliko watumishi wanaozalisha na au kutoa huduma kwa umma.

ii) Kuwa na Wizara, Mawaziri na Manaibu Mawaziri wengi ni kuongeza matumizi yasiyo ya lazima.

Suluhisho:
i) Kila Mkoa 1 uchague Mbunge 1 na mishahara yao iwe juu kidogo tu ya kipato cha Diwani

ii) Wizara ziunganishwe ziwepo za kutosha mf. 14 tu kwa mujibu wa Huduma / Shughuli za si za makundi ya watu. Pasiwepo Wizara chini ya Rais wala Makamu wala Waziri Mkuu. Majina yake yaweza kuwa yafuatayo:-

Mipango & Fedha; Afya & Ustawi wa Jamii; Elimu, Teknolojia na Utafiti; Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano; Biashara & Viwanda; Ardhi, Makazi na Mazingira; Nishati na Madini; Tawala za Mikoa, Ajira & Utumishi; Ulinzi na Usalama; Muungano, Mambo ya Nje & Ushirikiano wa Kimataifa; Katiba, Sheria na Sera; Kilimo, Uvuvi na Ufugaji; Maji;

iii) Hata baadahi ya Taasisi nyingi za Serikali zaweza ama kuondolewa au kuunganishwa mfano POSTA, BENKI YA POSTA NA SIMU hilo ni shirika moja; TANESCO & REA ni moja; TANROADS & TARURA hilo ni moja n.k kupunguza matumizi na mparaganyiko katika uwajibikaji.

Hujuma: 3
Ugatuzi wa madaraka katika Wilaya na Halmashauri na uwepo wa ma DC na na DED ni mkanganyiko ya uwajibikaji na mwendelezo wa mivutano ya mamlaka.

Suluhisho:
Chini ya Mkoa kuwepo na Wilaya ambapo Kiongozi wake awe mmoja tu ( aweza itwa Mkurugenzi Mtendaji) na nafasi hiyo ijazwe kwa Wenye sifa kuiomba, kuhojiwa na kuajiriwa na Kamati za Ajira za Mikoa.

Hujuma: 4
Kuwa na Viongozi wa vyombo huru mfano Jaji Mkuu; Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, na Spika ambao wanatokana kwa namna moja au nyingine ama na teuzi za Rais au michakato ya Vyama vya Siasa ni kuhalalisha uwajibikaji wao kwa aliyewaweka kazini! Ni kuendeleza malalamiko ya kutotendewa haki hata kama haki imetendeka.

Suluhisho: Watendaji Wakuu wa Vyombo huru (Independent Organs) mfano Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi; Jaji Mkuu; na Spika wote wapatikane kwa mchakato wa kulinganisha sifa za Waombaji baada ya Tume Maalumu ya Watumishi wa Juu wa Umma kupokea maombi yao na kuwachuja kutokana na sifa na kubakiza wachache (si zaidi ya 5) wenye sifa za juu ili wahojiwe wazi (public hearing) hadi kutangazwa atakayeshinda na kisha aajiriwe.

Hujuma: 5
Nchi kuendelea kushuhudia uwepo wa Wabunge 19 wa CHADEMA wakati CHADEMA haiwatambui ni aibu kubwa sana kwa Muhimili- Mtunzi Sheria.

Suluhisho: Waondolewe au waondoke wenyewe mara moja na kurejesha malipo yote yaliyofanyika kwao.

Hoja yao haianzii pale walipofutwa; inaanzia pale walipoingizwa Bungeni? Uongozi wa CHADEMA ulipotoa Tamko kuwa wao hawajawapeleka Bungeni ni sababu tosha ya kuheshimiwa kabisa toka siku ya kwanza kuwa hawakustahili kuwepo huko.

Mengine yote yanayofuata mfano, ya kupelekewa ‘kipeperushi’, eti kutokusikilizwa nk ni sababu ambazo (hata kama zingekuwa kweli) haziwezi kuwa juu ya ile ya wao kutopelekwa na CHADEMA kwenda Bungeni katika nafasi ya Viti maalumu.
 
RAISI AJAE

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
2,150
2,000
Hiyo ikifanyika!ccm itaua mfumo wa ulaji na ufisadi! na hii ndio blue print ya ccm tangu uhuru!! ulaji, ufisadi, kujuana n.! hawawezi kuka a tawi walilolikalia wataanguka na kupoteza wana chama wengi waimba mapambio!!!
 
Kibunago

JF-Expert Member
Jan 11, 2008
300
250
Ni mbunge gani atapeleka joja ya wabunge kupunguzwa? Unataka aanze kunyonyoka nywele na kupauka ngozi bila kujua anaugua ugonjwa gani? 🤣🤣🤣
Ndiyo maana halisi ya kichwa cha habari; Ni vidonge vichungu lakini vikimezwa mwisho wake ni kupona kwa fAIDA ya Taifa zima na Watanzania wote. Katiba ikidadiliwa na Wabunge (wasio ndani ya Bunge sasa) wa Bunge MAALUMU INAWEZEKANA.
 
Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,657
2,000
Kwa vile AMA Chombo husika hakijawajibika ipaswayo kwa mujibu wa Sheria iliyokiunda ya na. 15 ya 1996 hususan sehemu II Ibara ya 5 (1) (d) AU kwa Viongozi waliotangulia kutosikiliza/ tekeleza ushauri wao, leo nateremsha ushauri kwa kutaja mambo ambayo yanatafsirika kuwa HUJUMA (kwa kujua au kutokujua) yatakiwayo kuachwa / kubadilishwa kwa mstakabali wa Amani, Usalama na Maendeleo ya Taifa letu.

Hujuma: 1.
Kutokamilisha Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba ya nchi ni kutowatendea haki Wananchi walioshiriki kutoa maoni; ni kuendeleza manung’uniko yanayofisha Amani yetu na ni kuendelea kuwa na Sheria Mama butu ambayo ina maeneo mengi ya kurekebishwa ili tupate maendeleo stahiki.

Suluhisho: Mchakato wa Katiba Mpya / Yenye Marekebisho ukamilishwe ndani ya Bunge Maalumu (lenye wajumbe maalumu (kila mkoa uwakilishwe na mtu mmoja) tofauti na Wabunge wa Bunge lililopo).

Hujuma: 2.
Kuendelea kufumbia macho matumizi makubwa ya Serikali yasiyo na tija mfano:-

i. Kuwa na Idadi ya Wabunge wengi na wanaojipitishia malipo makubwa kuliko watumishi wanaozalisha na au kutoa huduma kwa umma.

ii) Kuwa na Wizara, Mawaziri na Manaibu Mawaziri wengi ni kuongeza matumizi yasiyo ya lazima.

Suluhisho:
i) Kila Mkoa 1 uchague Mbunge 1 na mishahara yao iwe juu kidogo tu ya kipato cha Diwani

ii) Wizara ziunganishwe ziwepo za kutosha mf. 14 tu kwa mujibu wa Huduma / Shughuli za si za makundi ya watu. Pasiwepo Wizara chini ya Rais wala Makamu wala Waziri Mkuu. Majina yake yaweza kuwa yafuatayo:-

Mipango & Fedha; Afya & Ustawi wa Jamii; Elimu, Teknolojia na Utafiti; Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano; Biashara & Viwanda; Ardhi, Makazi na Mazingira; Nishati na Madini; Tawala za Mikoa, Ajira & Utumishi; Ulinzi na Usalama; Muungano, Mambo ya Nje & Ushirikiano wa Kimataifa; Katiba, Sheria na Sera; Kilimo, Uvuvi na Ufugaji; Maji;

iii) Hata baadahi ya Taasisi nyingi za Serikali zaweza ama kuondolewa au kuunganishwa mfano POSTA, BENKI YA POSTA NA SIMU hilo ni shirika moja; TANESCO & REA ni moja; TANROADS & TARURA hilo ni moja n.k kupunguza matumizi na mparaganyiko katika uwajibikaji.

Hujuma: 3
Ugatuzi wa madaraka katika Wilaya na Halmashauri na uwepo wa ma DC na na DED ni mkanganyiko ya uwajibikaji na mwendelezo wa mivutano ya mamlaka.

Suluhisho:
Chini ya Mkoa kuwepo na Wilaya ambapo Kiongozi wake awe mmoja tu ( aweza itwa Mkurugenzi Mtendaji) na nafasi hiyo ijazwe kwa Wenye sifa kuiomba, kuhojiwa na kuajiriwa na Kamati za Ajira za Mikoa.

Hujuma: 4
Kuwa na Viongozi wa vyombo huru mfano Jaji Mkuu; Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, na Spika ambao wanatokana kwa namna moja au nyingine ama na teuzi za Rais au michakato ya Vyama vya Siasa ni kuhalalisha uwajibikaji wao kwa aliyewaweka kazini! Ni kuendeleza malalamiko ya kutotendewa haki hata kama haki imetendeka.

Suluhisho: Watendaji Wakuu wa Vyombo huru (Independent Organs) mfano Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi; Jaji Mkuu; na Spika wote wapatikane kwa mchakato wa kulinganisha sifa za Waombaji baada ya Tume Maalumu ya Watumishi wa Juu wa Umma kupokea maombi yao na kuwachuja kutokana na sifa na kubakiza wachache (si zaidi ya 5) wenye sifa za juu ili wahojiwe wazi (public hearing) hadi kutangazwa atakayeshinda na kisha aajiriwe.

Hujuma: 5
Nchi kuendelea kushuhudia uwepo wa Wabunge 19 wa CHADEMA wakati CHADEMA haiwatambui ni aibu kubwa sana kwa Muhimili- Mtunzi Sheria.

Suluhisho: Waondolewe au waondoke wenyewe mara moja na kurejesha malipo yote yaliyofanyika kwao.

Hoja yao haianzii pale walipofutwa; inaanzia pale walipoingizwa Bungeni? Uongozi wa CHADEMA ulipotoa Tamko kuwa wao hawajawapeleka Bungeni ni sababu tosha ya kuheshimiwa kabisa toka siku ya kwanza kuwa hawakustahili kuwepo huko.

Mengine yote yanayofuata mfano, ya kupelekewa ‘kipeperushi’, eti kutokusikilizwa nk ni sababu ambazo (hata kama zingekuwa kweli) haziwezi kuwa juu ya ile ya wao kutopelekwa na CHADEMA kwenda Bungeni katika nafasi ya Viti maalumu.
Safi sana nakupongeza mkuu kwa hili, shida inakuja wenye nchi hawataki kabisa kusikia mambo haya, sisi wananchi tunapenda haya ili kuleta usawa na haki katika kunufaika na resources zitokanazo na kodi zetu.

Changamoto ninayoiona ni moja, kiongozi mkuu wa sasa ndiye aliyetuletea draft namba mbili ya katiba ambayo wengi wetu hatukuipenda kabisa, lakini kwa upande mwingine, kuna mtu ameshika remote na ndiye aliyechangia kuharibiwa kwa mchakato mzima wa kazi ya tume ya Jaji Warioba

Nchi hii inaweza kuwa na viongozi wachache wenye tija alimradi tu wawe ni wenye vision na commitment, wingi wa wabunge Bungeni siyo faida kwa nchi, ni mzigo mzito kuwalipa watu wanaokwenda bungeni kugonga meza na kusinzia tu.
 
Kibunago

JF-Expert Member
Jan 11, 2008
300
250
Hiyo ikifanyika!ccm itaua mfumo wa ulaji na ufisadi!na hii ndio blue print ya ccm tangu uhuru!!ulaji,ufisadi,kujuana n.!hawawezi kuka a tawi walilolikalia wataanguka na kupoteza wana chama wengi waimba mapambio!!!
Mimi ni Mwana CCM. Hali ilivyo sasa ni ya kutuletea FAIDA ya MUDA MFUPI. Wananchi wanapenda Ustawi ,Uhuru , Amani na Usawa. Ili tujihakikishie kuendelea kuwa na Wanachama KWA MUDA MREFU LAZIMA TUJISAHIHISHE. Mifano iko mingi. Hapo jirani zetu tu palikuwepo KANU isiyotaka mabadiliko chanya leo hii nani anaimba KANU ? Watu wanaimba beat ya BBI kama Reggae huku wakitoka mapovu!
 
jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,667
2,000
Kwa vile AMA Chombo husika hakijawajibika ipaswayo kwa mujibu wa Sheria iliyokiunda ya na. 15 ya 1996 hususan sehemu II Ibara ya 5 (1) (d) AU kwa Viongozi waliotangulia kutosikiliza/ tekeleza ushauri wao, leo nateremsha ushauri kwa kutaja mambo ambayo yanatafsirika kuwa HUJUMA (kwa kujua au kutokujua) yatakiwayo kuachwa / kubadilishwa kwa mstakabali wa Amani, Usalama na Maendeleo ya Taifa letu.

Hujuma: 1.
Kutokamilisha Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba ya nchi ni kutowatendea haki Wananchi walioshiriki kutoa maoni; ni kuendeleza manung’uniko yanayofisha Amani yetu na ni kuendelea kuwa na Sheria Mama butu ambayo ina maeneo mengi ya kurekebishwa ili tupate maendeleo stahiki.

Suluhisho: Mchakato wa Katiba Mpya / Yenye Marekebisho ukamilishwe ndani ya Bunge Maalumu (lenye wajumbe maalumu (kila mkoa uwakilishwe na mtu mmoja) tofauti na Wabunge wa Bunge lililopo).

Hujuma: 2.
Kuendelea kufumbia macho matumizi makubwa ya Serikali yasiyo na tija mfano:-

i. Kuwa na Idadi ya Wabunge wengi na wanaojipitishia malipo makubwa kuliko watumishi wanaozalisha na au kutoa huduma kwa umma.

ii) Kuwa na Wizara, Mawaziri na Manaibu Mawaziri wengi ni kuongeza matumizi yasiyo ya lazima.

Suluhisho:
i) Kila Mkoa 1 uchague Mbunge 1 na mishahara yao iwe juu kidogo tu ya kipato cha Diwani

ii) Wizara ziunganishwe ziwepo za kutosha mf. 14 tu kwa mujibu wa Huduma / Shughuli za si za makundi ya watu. Pasiwepo Wizara chini ya Rais wala Makamu wala Waziri Mkuu. Majina yake yaweza kuwa yafuatayo:-

Mipango & Fedha; Afya & Ustawi wa Jamii; Elimu, Teknolojia na Utafiti; Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano; Biashara & Viwanda; Ardhi, Makazi na Mazingira; Nishati na Madini; Tawala za Mikoa, Ajira & Utumishi; Ulinzi na Usalama; Muungano, Mambo ya Nje & Ushirikiano wa Kimataifa; Katiba, Sheria na Sera; Kilimo, Uvuvi na Ufugaji; Maji;

iii) Hata baadahi ya Taasisi nyingi za Serikali zaweza ama kuondolewa au kuunganishwa mfano POSTA, BENKI YA POSTA NA SIMU hilo ni shirika moja; TANESCO & REA ni moja; TANROADS & TARURA hilo ni moja n.k kupunguza matumizi na mparaganyiko katika uwajibikaji.

Hujuma: 3
Ugatuzi wa madaraka katika Wilaya na Halmashauri na uwepo wa ma DC na na DED ni mkanganyiko ya uwajibikaji na mwendelezo wa mivutano ya mamlaka.

Suluhisho:
Chini ya Mkoa kuwepo na Wilaya ambapo Kiongozi wake awe mmoja tu ( aweza itwa Mkurugenzi Mtendaji) na nafasi hiyo ijazwe kwa Wenye sifa kuiomba, kuhojiwa na kuajiriwa na Kamati za Ajira za Mikoa.

Hujuma: 4
Kuwa na Viongozi wa vyombo huru mfano Jaji Mkuu; Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, na Spika ambao wanatokana kwa namna moja au nyingine ama na teuzi za Rais au michakato ya Vyama vya Siasa ni kuhalalisha uwajibikaji wao kwa aliyewaweka kazini! Ni kuendeleza malalamiko ya kutotendewa haki hata kama haki imetendeka.

Suluhisho: Watendaji Wakuu wa Vyombo huru (Independent Organs) mfano Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi; Jaji Mkuu; na Spika wote wapatikane kwa mchakato wa kulinganisha sifa za Waombaji baada ya Tume Maalumu ya Watumishi wa Juu wa Umma kupokea maombi yao na kuwachuja kutokana na sifa na kubakiza wachache (si zaidi ya 5) wenye sifa za juu ili wahojiwe wazi (public hearing) hadi kutangazwa atakayeshinda na kisha aajiriwe.

Hujuma: 5
Nchi kuendelea kushuhudia uwepo wa Wabunge 19 wa CHADEMA wakati CHADEMA haiwatambui ni aibu kubwa sana kwa Muhimili- Mtunzi Sheria.

Suluhisho: Waondolewe au waondoke wenyewe mara moja na kurejesha malipo yote yaliyofanyika kwao.

Hoja yao haianzii pale walipofutwa; inaanzia pale walipoingizwa Bungeni? Uongozi wa CHADEMA ulipotoa Tamko kuwa wao hawajawapeleka Bungeni ni sababu tosha ya kuheshimiwa kabisa toka siku ya kwanza kuwa hawakustahili kuwepo huko.

Mengine yote yanayofuata mfano, ya kupelekewa ‘kipeperushi’, eti kutokusikilizwa nk ni sababu ambazo (hata kama zingekuwa kweli) haziwezi kuwa juu ya ile ya wao kutopelekwa na CHADEMA kwenda Bungeni katika nafasi ya Viti maalumu.
Nimekugongea love ❤️ kabisa yani. Na unafahamu kuwa wewe ni ccm kindakindaki na mkongwe hata kuliko mimi humu kama sikosei.Bigs up. Hii thread ni lazima itamfikia mama!
Mark my words, ushauri wako unaweza kuchukuliwa. It will be GREAT! GOD WILLING!
 
Kibunago

JF-Expert Member
Jan 11, 2008
300
250
Safi sana nakupongeza mkuu kwa hili, shida inakuja wenye nchi hawataki kabisa kusikia mambo haya, sisi wananchi tunapenda haya ili kuleta usawa na haki katika kunufaika na resources zitokanazo na kodi zetu.

Changamoto ninayoiona ni moja, kiongozi mkuu wa sasa ndiye aliyetuletea draft namba mbili ya katiba ambayo wengi wetu hatukuipenda kabisa, lakini kwa upande mwingine, kuna mtu ameshika remote na ndiye aliyechangia kuharibiwa kwa mchakato mzima wa kazi ya tume ya Jaji Warioba

Nchi hii inaweza kuwa na viongozi wachache wenye tija alimradi tu wawe ni wenye vision na commitment, wingi wa wabunge Bungeni siyo faida kwa nchi, ni mzigo mzito kuwalipa watu wanaokwenda bungeni kugonga meza na kusinzia tu.
Nakuhakikishia kuwa Rais akikubali kuunda Bunge Maalumu lenye Wabunge wachache makini kuwakilisha kila mkoa ataitendea haki Ofisi yake ya Urais na atakumbukwa milele . Nikifuatilia kwa umakini alivyoanza; naona uelekeo wake ni wa kutaka Amani na Ufanisi katika Serikali yake!
Unajua Bunge letu lina watu kibao bila Ufanisi wowote. Hata hawawezi kupata nafasi ya kutosha ya kila Mbunge kuwasilisha hoja zao vyema. Hivyo licha ya kupoteza fedha za umma; tunakuwa na inneffective parliament of the highest order!
 
Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,657
2,000
Nikifuatilia kwa umakini alivyoanza; naona uelekeo wake ni wa kutaka Amani na Ufanisi katika Serikali yake!
Unajua Bunge letu lina watu kibao bila Ufanisi wowote. Hata hawezi kupata nafasi ya kutosha ya kila Mbunge kuwasilisha hoja zake vyema. Hivyo licha ya kupoteza fedha za umma; tunakuwa na inneffective parliament of the highest order!
🤛

👍

🤝
 
babykailama

JF-Expert Member
Mar 5, 2012
247
250
Kibs umekuna ubongo wangu. Haya ndiyo mabandiko niliyazoea toka kwa ma Think-Tank wa JF. Mod aachilie huu uzi utembee watu wachangie.
Mimi naona tunze na hao Wabunge 19 Waondoke Bungeni kuanzia J'Tatu. Kisha ndani ya miezi sita BUNGE la KATIBA liitwe. Wabunge wa Bunge maalumu waombe kazi hiyo kwa kujaza fomu na kueleza sifa zao. Rais aunde TUME MAALUMU YA KUAJIRI KWA MUDA WABUNGE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA. Kazi iendelee!
 
Niza doyi

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
1,211
2,000
Kwa vile AMA Chombo husika hakijawajibika ipaswayo kwa mujibu wa Sheria iliyokiunda ya na. 15 ya 1996 hususan sehemu II Ibara ya 5 (1) (d) AU kwa Viongozi waliotangulia kutosikiliza/ tekeleza ushauri wao, leo nateremsha ushauri kwa kutaja mambo ambayo yanatafsirika kuwa HUJUMA (kwa kujua au kutokujua) yatakiwayo kuachwa / kubadilishwa kwa mstakabali wa Amani, Usalama na Maendeleo ya Taifa letu.

Hujuma: 1.
Kutokamilisha Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba ya nchi ni kutowatendea haki Wananchi walioshiriki kutoa maoni; ni kuendeleza manung’uniko yanayofisha Amani yetu na ni kuendelea kuwa na Sheria Mama butu ambayo ina maeneo mengi ya kurekebishwa ili tupate maendeleo stahiki.

Suluhisho: Mchakato wa Katiba Mpya / Yenye Marekebisho ukamilishwe ndani ya Bunge Maalumu (lenye wajumbe maalumu (kila mkoa uwakilishwe na mtu mmoja) tofauti na Wabunge wa Bunge lililopo).

Hujuma: 2.
Kuendelea kufumbia macho matumizi makubwa ya Serikali yasiyo na tija mfano:-

i. Kuwa na Idadi ya Wabunge wengi na wanaojipitishia malipo makubwa kuliko watumishi wanaozalisha na au kutoa huduma kwa umma.

ii) Kuwa na Wizara, Mawaziri na Manaibu Mawaziri wengi ni kuongeza matumizi yasiyo ya lazima.

Suluhisho:
i) Kila Mkoa 1 uchague Mbunge 1 na mishahara yao iwe juu kidogo tu ya kipato cha Diwani

ii) Wizara ziunganishwe ziwepo za kutosha mf. 14 tu kwa mujibu wa Huduma / Shughuli za si za makundi ya watu. Pasiwepo Wizara chini ya Rais wala Makamu wala Waziri Mkuu. Majina yake yaweza kuwa yafuatayo:-

Mipango & Fedha; Afya & Ustawi wa Jamii; Elimu, Teknolojia na Utafiti; Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano; Biashara & Viwanda; Ardhi, Makazi na Mazingira; Nishati na Madini; Tawala za Mikoa, Ajira & Utumishi; Ulinzi na Usalama; Muungano, Mambo ya Nje & Ushirikiano wa Kimataifa; Katiba, Sheria na Sera; Kilimo, Uvuvi na Ufugaji; Maji;

iii) Hata baadahi ya Taasisi nyingi za Serikali zaweza ama kuondolewa au kuunganishwa mfano POSTA, BENKI YA POSTA NA SIMU hilo ni shirika moja; TANESCO & REA ni moja; TANROADS & TARURA hilo ni moja n.k kupunguza matumizi na mparaganyiko katika uwajibikaji.

Hujuma: 3
Ugatuzi wa madaraka katika Wilaya na Halmashauri na uwepo wa ma DC na na DED ni mkanganyiko ya uwajibikaji na mwendelezo wa mivutano ya mamlaka.

Suluhisho:
Chini ya Mkoa kuwepo na Wilaya ambapo Kiongozi wake awe mmoja tu ( aweza itwa Mkurugenzi Mtendaji) na nafasi hiyo ijazwe kwa Wenye sifa kuiomba, kuhojiwa na kuajiriwa na Kamati za Ajira za Mikoa.

Hujuma: 4
Kuwa na Viongozi wa vyombo huru mfano Jaji Mkuu; Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, na Spika ambao wanatokana kwa namna moja au nyingine ama na teuzi za Rais au michakato ya Vyama vya Siasa ni kuhalalisha uwajibikaji wao kwa aliyewaweka kazini! Ni kuendeleza malalamiko ya kutotendewa haki hata kama haki imetendeka.

Suluhisho: Watendaji Wakuu wa Vyombo huru (Independent Organs) mfano Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi; Jaji Mkuu; na Spika wote wapatikane kwa mchakato wa kulinganisha sifa za Waombaji baada ya Tume Maalumu ya Watumishi wa Juu wa Umma kupokea maombi yao na kuwachuja kutokana na sifa na kubakiza wachache (si zaidi ya 5) wenye sifa za juu ili wahojiwe wazi (public hearing) hadi kutangazwa atakayeshinda na kisha aajiriwe.

Hujuma: 5
Nchi kuendelea kushuhudia uwepo wa Wabunge 19 wa CHADEMA wakati CHADEMA haiwatambui ni aibu kubwa sana kwa Muhimili- Mtunzi Sheria.

Suluhisho: Waondolewe au waondoke wenyewe mara moja na kurejesha malipo yote yaliyofanyika kwao.

Hoja yao haianzii pale walipofutwa; inaanzia pale walipoingizwa Bungeni? Uongozi wa CHADEMA ulipotoa Tamko kuwa wao hawajawapeleka Bungeni ni sababu tosha ya kuheshimiwa kabisa toka siku ya kwanza kuwa hawakustahili kuwepo huko.

Mengine yote yanayofuata mfano, ya kupelekewa ‘kipeperushi’, eti kutokusikilizwa nk ni sababu ambazo (hata kama zingekuwa kweli) haziwezi kuwa juu ya ile ya wao kutopelekwa na CHADEMA kwenda Bungeni katika nafasi ya Viti maalumu.
Tundu lissu umekuja kivingine! katiba haimo kwenye Ilani,wazo lako jaribu baada 2025.
 
Kibunago

JF-Expert Member
Jan 11, 2008
300
250
Tundu lissu umekuja kivingine! katiba haimo kwenye Ilani,wazo lako jaribu baada 2025.
Pole sana; Mawazo ya Kujisahihisha au Maendeleo ya nchi hayaletwi na TL tu. Ubashiri wako ni Mkeka uliochanika ; tandika mwingine.
 
Kibunago

JF-Expert Member
Jan 11, 2008
300
250
Nimekugongea love ❤️ kabisa yani. Na unafahamu kuwa wewe ni ccm kindakindaki na mkongwe hata kuliko mimi humu kama sikosei.Bigs up. Hii thread ni lazima itamfikia mama!
Mark my words, ushauri wako unaweza kuchukuliwa. It will be GREAT! GOD WILLING!
Jmushi; asante ndg. yangu wewe unajua tunachosimamia!
 
babykailama

JF-Expert Member
Mar 5, 2012
247
250
Tundu lissu umekuja kivingine! katiba haimo kwenye Ilani,wazo lako jaribu baada 2025.
NIZA zinduka acha kufikiri habari za Wanasiasa tu; Tanzania ni yetu sote wakiwemo wanasiasa wachache na wasio wanasiasa wengi saaana wanaoitakia mema nchi.
 
sanje

JF-Expert Member
May 12, 2018
439
500
Tundu lissu umekuja kivingine! katiba haimo kwenye Ilani,wazo lako jaribu baada 2025.
Hata kifo Cha dictator jiwe haikuwepo kwenye ilani ya ccm lakini kashafukiwa.msidhani mtaendelea kuiba kura Kila siku is not sastainable
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom