Kibunago
JF-Expert Member
- Jan 11, 2008
- 300
- 122
Kwa vile AMA Chombo husika hakijawajibika ipaswayo kwa mujibu wa Sheria iliyokiunda ya na. 15 ya 1996 hususan sehemu II Ibara ya 5 (1) (d) AU kwa Viongozi waliotangulia kutosikiliza/ tekeleza ushauri wao, leo nateremsha ushauri kwa kutaja mambo ambayo yanatafsirika kuwa HUJUMA (kwa kujua au kutokujua) yatakiwayo kuachwa / kubadilishwa kwa mstakabali wa Amani, Usalama na Maendeleo ya Taifa letu.
Hujuma: 1.
Kutokamilisha Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba ya nchi ni kutowatendea haki Wananchi walioshiriki kutoa maoni; ni kuendeleza manung’uniko yanayofisha Amani yetu na ni kuendelea kuwa na Sheria Mama butu ambayo ina maeneo mengi ya kurekebishwa ili tupate maendeleo stahiki.
Suluhisho: Mchakato wa Katiba Mpya / Yenye Marekebisho ukamilishwe ndani ya Bunge Maalumu (lenye wajumbe maalumu (kila mkoa uwakilishwe na mtu mmoja) tofauti na Wabunge wa Bunge lililopo).
Hujuma: 2.
Kuendelea kufumbia macho matumizi makubwa ya Serikali yasiyo na tija mfano:-
i. Kuwa na Idadi ya Wabunge wengi na wanaojipitishia malipo makubwa kuliko watumishi wanaozalisha na au kutoa huduma kwa umma.
ii) Kuwa na Wizara, Mawaziri na Manaibu Mawaziri wengi ni kuongeza matumizi yasiyo ya lazima.
Suluhisho:
i) Kila Mkoa 1 uchague Mbunge 1 na mishahara yao iwe juu kidogo tu ya kipato cha Diwani
ii) Wizara ziunganishwe ziwepo za kutosha mf. 14 tu kwa mujibu wa Huduma / Shughuli za si za makundi ya watu. Pasiwepo Wizara chini ya Rais wala Makamu wala Waziri Mkuu. Majina yake yaweza kuwa yafuatayo:-
Mipango & Fedha; Afya & Ustawi wa Jamii; Elimu, Teknolojia na Utafiti; Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano; Biashara & Viwanda; Ardhi, Makazi na Mazingira; Nishati na Madini; Tawala za Mikoa, Ajira & Utumishi; Ulinzi na Usalama; Muungano, Mambo ya Nje & Ushirikiano wa Kimataifa; Katiba, Sheria na Sera; Kilimo, Uvuvi na Ufugaji; Maji;
iii) Hata baadahi ya Taasisi nyingi za Serikali zaweza ama kuondolewa au kuunganishwa mfano POSTA, BENKI YA POSTA NA SIMU hilo ni shirika moja; TANESCO & REA ni moja; TANROADS & TARURA hilo ni moja n.k kupunguza matumizi na mparaganyiko katika uwajibikaji.
Hujuma: 3
Ugatuzi wa madaraka katika Wilaya na Halmashauri na uwepo wa ma DC na na DED ni mkanganyiko ya uwajibikaji na mwendelezo wa mivutano ya mamlaka.
Suluhisho:
Chini ya Mkoa kuwepo na Wilaya ambapo Kiongozi wake awe mmoja tu ( aweza itwa Mkurugenzi Mtendaji) na nafasi hiyo ijazwe kwa Wenye sifa kuiomba, kuhojiwa na kuajiriwa na Kamati za Ajira za Mikoa.
Hujuma: 4
Kuwa na Viongozi wa vyombo huru mfano Jaji Mkuu; Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, na Spika ambao wanatokana kwa namna moja au nyingine ama na teuzi za Rais au michakato ya Vyama vya Siasa ni kuhalalisha uwajibikaji wao kwa aliyewaweka kazini! Ni kuendeleza malalamiko ya kutotendewa haki hata kama haki imetendeka.
Suluhisho: Watendaji Wakuu wa Vyombo huru (Independent Organs) mfano Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi; Jaji Mkuu; na Spika wote wapatikane kwa mchakato wa kulinganisha sifa za Waombaji baada ya Tume Maalumu ya Watumishi wa Juu wa Umma kupokea maombi yao na kuwachuja kutokana na sifa na kubakiza wachache (si zaidi ya 5) wenye sifa za juu ili wahojiwe wazi (public hearing) hadi kutangazwa atakayeshinda na kisha aajiriwe.
Hujuma: 5
Nchi kuendelea kushuhudia uwepo wa Wabunge 19 wa CHADEMA wakati CHADEMA haiwatambui ni aibu kubwa sana kwa Muhimili- Mtunzi Sheria.
Suluhisho: Waondolewe au waondoke wenyewe mara moja na kurejesha malipo yote yaliyofanyika kwao.
Hoja yao haianzii pale walipofutwa; inaanzia pale walipoingizwa Bungeni? Uongozi wa CHADEMA ulipotoa Tamko kuwa wao hawajawapeleka Bungeni ni sababu tosha ya kuheshimiwa kabisa toka siku ya kwanza kuwa hawakustahili kuwepo huko.
Mengine yote yanayofuata mfano, ya kupelekewa ‘kipeperushi’, eti kutokusikilizwa nk ni sababu ambazo (hata kama zingekuwa kweli) haziwezi kuwa juu ya ile ya wao kutopelekwa na CHADEMA kwenda Bungeni katika nafasi ya Viti maalumu.