Huenda Mbowe akafilisiwa

Huenda Mbowe akafilisiwa

Wafanyakazi wa b
Kama ameamua kukata RUFAA basi anajua ana haki zake.Na hata kama HAKI itacheleweshwa leo,itakuja tu.Tujifunze kwa wale wafanyakazi 31 wa BOT baada ya miaka 22 wamepewa haki zao.Na Mbowe kama anahaki zake kwenye jengo basi aende kwenye Mahakama ya Rufani,haki ya mtu ipo tu japo itacheleweshwa.
BOTbado hawaja pewa haki yao.
Hawaja pokelewa kazini wala hawaja lipwa pesa yoyote.haki ipi wamepewa??
 
Pathetic!!
Yani kila kitu ni siasa, hapa chama na wafuasi wameingiaje?
 
Sasa kwanini alilalamika kwa kuondolewa Billcanaz?...wacha kurusha miguu kama 'kuku anayekata roho!' unaweza kumtenganisha Mbowe na Mbowe hotels?...Mbowe ni Shareholder wa Mbowe hotels...na kuna mabo yanahitaji director guarantee!
Hivi umeshawahi kumuona mbowe akienda mahakamani kwa ajili ya hii kesi?mbowe hotels ni legal person Ina madeni yake, inashitaki na kushitakiwa, na mpaka wamuite na kumfilisi mbowe Kama mbowe kuna safari ndefu na pia ni legal battle ya kufa mtu, nyie watu mnaropoka tuu hamjui hata company law
 
Mimi nimeongelea suala la ufilisi halina siasa. Sijazungumzia hatua zilizochukuliwa na NHC, Ikithibitika kiseria atayefilisiwa ni Mbowe Hotels nadhani unaelewa maana na consequences za kuwa mufilisi.
Tupo pamoja and nimekuelewa hasa katika utaratibu wa sheria za makapuni pale kampuni inapovaa uhusika wa mtu. Ila kwa mazoea yetu yalivyo na dhana hio ya kampuni kuvaa uhusika wa mtu huwa hatujali na ndio maana hata mbowe alidai kuwa hayo yanatokana kwa sababu za kisiasa
 
Kwa wenzetu kiongozi kukwepa kulipa kodi ni kashfa scandalous, hapa kwetu Tz ni ushujaa. Maskini Tz nchi yangu.
 
Eti kuna watanzania wasomi na wasiosoma wanaotegemea mtu kama mbowe kuleta ukombozi hapa nchini, pole yao!!
 
Anayedaiwa ni Mbowe Hotels na sio Freeman Mbowe.......kisheria kuna tofauti na haihusiani na siasa.

alisema anasakamwa kwa sababu za kisiasa, wewe ndio unatoa tamko la kupingana na mbowe
mahaba yanaum jamani
 
Mbowe kufilisiwa!

Tahadhari za makusudi zisipchukuliwa huenda Ndugu Mbowe akafilisiwa ili kulipa malimbikizo ya deni la pango linalofikia takribani bilioni 1.7 za kitanzania.

Baada ya kesi mahakama kuu kuipa kuhalalisha uamuzi NHC kumfurusha kwenye nyumba yake ni dhahiri sasa kinachofuata ni kulipa deni (Sh.1.7 B) +Gharama za dalali (angalau 8% ya deni) + Adhabu za kuchelewesha kodi + gharama za kesi + gharama za kuondoa vitu kwenye jingo + gharama nyinginezo korti itakazoona zinafaa. Mzigo huu si mdogo kwa Mbowe.

Rufaa;
Kuna tetesi kuwa atakata rufaa mahakama ya rufaa japo hiyo itakuwa sawa na kuahirisha maumivu na kuongeza gharama zisizokuwa na msingi kwani dawa ya deni ni kulipa na namba haziongopi.ushahidi wa mikataba ya pango,demand notice,barua za Mbowe hotels kwenda NHC zote zinathibitisha deni hilo. Hii itakuwa ni sawa na ‘mateke ya mwisho mwisho ya punda anayekata roho’.

Nini kifanyike?
Aka echini na NHC kuandaa mpango wa kulipa deni kwa awamu huku akitafuta wateja wa baadhi ya mali zake kulipia deni hilo. Lazima tukiri tu kuwa biashara nyingi za Mbowe haziwezi kulipa deni hilo labda kwa kutuimia fedha alizoficha nje ya nji kama ilivyowahi kuripotiwa na baadhi ya magazeti ndani na nje kipindi cha uchaguzi mkuu 2015. Ikumbukwe pia kupitia hoteli za familia yao wana madeni NSSF ambayo yanasuasua na kuna kipindi siku za nyuma alilazimika kwenda mahakamani kuomba mali zake zisiuzwe.

Pili, Mbowe ni lazima atumie mwanya wa ‘ufubavu’ wa uelewa wa wafuasi wake ambao amewadanganya kuwa kesi hiyo ni ya kisiasa ili kupata huruma. Hapa fursa iliyopo ni kukitwisha chama mzigo wa deni, kulipa kwa ruzuku na misaada ya wahisani. Hapa atumie propaganda kuwa ‘’sina bei’..’ hata wakinisingizia madeni wanachama wa chadema wapo radhi kulipa ili kupata ukombozi’’, hapa aanzishe kampeni za kukusanya michango mbalimbali kupitia mitandao na harambee. Kadri anavyochelewa ndivyo wanachama watashituka na mabadiliko ya mwenyekiti yanaweza yakawa ‘kaburi’ lake kisiasa kwani hatakuwa na pakushika.

Ni dhahiri madeni haya hayatamuacha salama kisiasa kwani hatokuwa na ‘moral authority’ kukemea wanasiasa wengine waliokwapua fedha kwenye mashirika ya umma na kushindwa kurudisha. Ushawishi wake umekwisha kilichobaki ni ubunge na uenyekiti kama alivyo raisi Zuma wa Afrika kusini amebakiza uraisi tu ila si ushawishi kisiasa.

Naomba tujadili kwa kina na si kutoa matusi na kudhalilishana. Hoja kwa hoja!.
kama hujui si unyamaze tuu
 
Huo si ushauri unalikisha ili upate mrejesho.

Endeleeni na mipango yenu. Mwisho wake ukweli utadhihiri na mtaumbuka tu.
 
80% sawa, ila watu milion 5 tu ndo waliomchagua
Hili nalo la kujivunia?

Mbowe alishamalizwa kisiasa na Kikwete mwaka 2005 alipobwagwa kwa kura 80%, uko wapi wewe? Umelala?

Alipe kodi na deni na asituletee ujinga.
 
Back
Top Bottom