Huenda Mbowe akafilisiwa

Haya ndiyo mahesabu ya CCM kummaliza Mbowe na upinzani nchini. Mbona kina Diallo wanadaiwa? Watu wamekwapua mabilioni ya Escrow wamenyamaziwa!
Hizi ndio dalili za kumfanyia Mbowe "Harambee" sasa kwa madai ya kuwadanganya wanachadema kwamba ccm inataka kummaliza, wakati mnajua fika kuwa anadaiwa na NHC.
 
MIND YOUR OWN BUSINESS!
 
kwahiyo asidaiwe kwakuwa diallo anadaiwa...CHADEMA kimevamiwa kwakweli. nimekubali wagonjwa wa akili kweli wameongezeka.

halafu watu wanachanganya deni la dialo ni tofauti na la mangi , mbowe anadaiwa kodi ya pango , ambalo pia ameshaapewa , na notice achie ,jengo wenye pesa wapangishe, walipe kodi hizo ni resilimali za watanzania
diallo yeye anadaiwa kodi ya biashara zake , na amekiri , hilo kuwa atalipa na sababu zilizomfanya ashindwe kulipa hiyo inakubalika popote dunia , sasa mbowe amefaidi NHC miaka yote bado anaona ni haki yake kuendelea kuishi huko , kiujanjajanja
 
Hapa ndipo tunapofeli Sikh zote...kumsafisha mchafu kwakutumia uchafu wa MTU mW engine.
Haya ndiyo mahesabu ya CCM kummaliza Mbowe na upinzani nchini. Mbona kina Diallo wanadaiwa? Watu wamekwapua mabilioni ya Escrow wamenyamaziwa!
 
Mbowe ni mfanya Biashara mkubwa tuu so he will pay, ingawa hili swala linaonekana kutawaliwa na siasa. Ni jambo dogo tuu
Ndio maana kuna haja ya kupeleka muswada wa kuwatenganisha wafanyabiashara na wabunge na viongozi wa vyama na serikali, ili kumaliza manung'uniko ya Ku shift burden kutoka kudaiwa na NHC na kulifanya kana kwamba ni CCM eti ndio inamdai Mbowe!
 

Kama ameamua kukata RUFAA basi anajua ana haki zake.Na hata kama HAKI itacheleweshwa leo,itakuja tu.Tujifunze kwa wale wafanyakazi 31 wa BOT baada ya miaka 22 wamepewa haki zao.Na Mbowe kama anahaki zake kwenye jengo basi aende kwenye Mahakama ya Rufani,haki ya mtu ipo tu japo itacheleweshwa.
 
Suala la ukwepaji kodi isn't about nani ni nani, kama mahakama ime rule kuwa MBOWE HOTELS Co....ilipe, basi ilipe.
 
Hili suala lilipelekwa kisiasa ili kumpunguza Mbowe makali ya UKUTA sept 1,

Kwa kuwa ni maoni yako na una Uhuru wa kuyatoa pasi na shaka tubakie hapo na neno HUENDA.
 
Yericko yuko wapi na Ben.. Maana wamekua watetezi wa madeni binafsi ya Mbowe
 
Ni Tanzania tu wakwepa kodi wakubwa wanabembelezwa!
 
Mkiona mmekwama mnaazia CDM ili kupata kiki, mwambieni Nchi inakwenda kama gari bovu.
 

Mbona sioni mjadala hapa, naona tu hukumu uliyotoa? Hebu lete huo mkataba unasemaje na tukianzia hapo ndipo tunaweza kuwa na mjadala. Vinginevyo 'this is just vapour'!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…