Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 962
- 1,909
Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar amesema kampuni kubwa za kimataifa za Moody’s na Fitch Ratings zilifanya tathmini ya awamu ya kwanza ya uwezo wa nchi kukopa na kulipa madeni kwa mwaka 2026.
Matokeo ya tathmini yalionesha kuwa Tanzania inakopesheka na ina uwezo mzuri wa kulipa madeni yake.
Matokeo hayo yanatokana na ukuaji mzuri wa uchumi, utekelezaji wa mageuzi ya kimuundo yanayoboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, pamoja na nidhamu ya matumizi ya fedha za umma na ongezeko la mapato ya Serikali.
Amesema "Kutokana na kuimarishwa kwa usimamizi wa deni la Serikali, Tanzania imeibuka mshindi wa jumla katika Tuzo ya Usimamizi wa Deni la Serikali katika nchi za Jumuiya ya Madola. Ninapenda kuwahakikishia watanzania kuwa Serikali itaendelea kulinda uthabiti wa deni la Serikali na kudhibiti gharama za ukopaji kwa: Kuendeleza mageuzi ya uchumi; kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani; kutoa kipaumbele kwa mikopo yenye masharti nafuu; na kuongeza uzalishaji na thamani ya bidhaa za ndani ili kuongeza mauzo nje na hivyo kuongeza fedha za kigeni."