Huenda kwa sasa Tanzania hakuna mchezaji mwenye upeo, busara, nidhamu na kipawa kama Chemalone

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,131
35,174
Kama wewe unajua mpira na unafuatilia soka la Tanzania huenda utakubaliana na mimi. Ni vigumu mnoo kuwa na mchezaji mwenye sifa hizi.
1. Usikivu wakati wote.
2. Utulivu wakati wote.
3. Umakini wakati wote.

Kukosea kupo, lakini standard za uchezaji wa Chemalone zimebakia katika kiwango kile kile cha usikivu, utulivu na umakini.

Sio rahisi mchezaji kusajiriwa na timu za Simba na Yanga kisha moja kwa moja kuwemo katika kikosi cha kwanza na kila mechi apangwe. Chemalone ameweza hilo.

Kwa mbali unaweza ukahisi labda huyu ni Keneth Mkapa wa Yanga ya miaka ile ya 90s.
Ama akahisi ni John Terry wa Chelsea kipindi kile cha Mourinho.
Na kwa karibu unawza ukahisi huyu ni Edgar Devis wa kipindi kile akiwa uholanzi.
 
Mkuu, hili ni jukwaa mahsusi kwa ajili ya mambo ya siasa. Habari za michezo na burudani yana jukwaa lake rasmi pia.
 
Mkuu, hili ni jukwaa mahsusi kwa ajili ya mambo ya siasa. Habari za michezo na burudani yana jukwaa lake rasmi pia.
Che malone anaye mzunguzia yeye ni raisi samia wa mwenyekiti wa CCM siasa haihusiki hapo!
 
Back
Top Bottom