Huenda hiki alichokitabiri msanii Chid Benz kwa Makonda kikatimia?

msovero

JF-Expert Member
Jun 30, 2019
839
1,472
Baada ya waziri wa habari kudai wanasubiri ripoti ya uchunguzi wa uvamizi wa kituo cha runinga cha clouds dhidi ya aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa dar es salaam bw. Paul Makonda imenikumbusha ushauri aliowahi kupewa RC huyo wa zamani na msanii wa kizazi kipya 'Rashid Makwilo' a.k.a 'Chid Benz'.

Katika moja ya mahojiano yake 'interview' msanii 'chid benz' alimshauri Paul Makonda wakati akiwa bado ni RC wa jiji la Dar kuwa ni vyema akajikita kufanya mambo ya msingi yaliyomweka kwenye kiti na kuachana na mambo madogo madogo yasiyo na tija ambayo yanaweza kumharibia na hata kumuingiza kwenye jinai.

Katika mahojiano hayo msanii 'chid benz' alimshauri Makonda kushughulika zaidi na mambo ya kiserikali ikiwemo kutatua kero za wananchi kama vile kuboresha huduma za afya mahospitalini, kupanga machinga, kuboresha vituo vya dala dala, kuboresha mazingira ya wafanyabiashara wafanye kazi kwa uhuru n.k.

Msanii 'Rashid Makwilo' a.k.a 'Chid Benz' hakuishia hapo bali alienda mbali zaidi na kumshauri makonda kuboresha mazingira ya magereza zilizopo katika mkoa wake huku akitolea mfano gereza la Segerea kwamba hata yeye kwa matendo anayofanya ipo siku ambayo haijulikani na yeye anaweza kuwa mfungwa mtarajiwa na kufungwa kwenye magereza hayo hayo yenye mazingira mabovu.

Lakini kwa hulka aliyokuwa nayo kijana makonda alipuuza ushauri huo na kuendelea kufanya mambo yake aliyokuwa anaona ni sahihi kwake ikiwemo kusakizia watu kesi za madawa ya kulevya na mambo mengine mengine.

Kwa kuzingatia ushauri huo wa msanii 'Chid Benz' je, ni karma imeanza kumwandama makonda? Je huenda kweli sakata la uvamizi wa Clouds likaibuliwa na makonda akafungwa kwenye magereza alizomtabiria msanii chid benz?

Muda utasema!

Zaidi, msikilize hapa rapper 'chid benz' akimchana live makonda
 

Attachments

  • Chid__Benz__amlipua_RC_Paul_Makonda.(144p).3gp
    1.7 MB · Views: 6
  • Chid__Benz__amlipua_RC_Paul_Makonda.(144p).3gp
    1.7 MB · Views: 2
Makonda Ngoma ni ngoma iliyovuma sana, bahati ni kwamba haikupasuka kwa wakati bali iliishia kupata ufa, ila sasa naona inapasuka rasmi.
Mmmh! Acha tuone ila kijana alijisahau sana kwahiyo yakimpata ya kumpata sidhani kama atakuwa na wa kumtetea
 
Usipoziba ufa utajenga ukuta naona kwenye Kona kumeachia kabisa bado cona yapili
Matukio haya mawili ya makonda na sabaya inabidi yawe fundisho kwa vijana wengine ili pale wanapoaminiwa na kupewa madaraka makubwa wasiyatumie madaraka hayo vibaya isipokuwa kwa kuwaletea maendeleo wananchi wanaowaongoza
 
Kuna interview chid alisema sema Makonda aachane na mambo ya wasanii na kiki yeye afanye kilichomweka pale , maana mwisho wa siku sisi tunachotaka ni hela hamna kingine
 
Samia kaja kivyake vyake tu kuwàchia ma papa walaji wa inchi kuakamata akina mbowe na kulipiza visasi ngoja tuone
 
Hii issue baada ya kuona taarifa imeundiwa tume ambayo hatujui hata ilitangazwa lini, naamini huo ndio mwisho wake, huyo jamaa sidhani kama atapelekwa mahakamani na serikali labda watu binafsi.
 
Hii issue baada ya kuona taarifa imeundiwa tume ambayo hatujui hata ilitangazwa lini, naamini huo ndio mwisho wake, huyo jamaa sidhani kama atapelekwa mahakamani na serikali labda watu binafsi.
inavyoonekana serikali haimpeleki ila watu binafsi but hao watu binafsi watakuwa na backup isiyoonekana
 
Atasema ye anaitwa Daudi Bashite
Itakuwa na maana gani kukana jina ikiwa sura, mwili na mwonekano ni vya kwake na ushahidi wa footage za cctv camera zinazoonyesha mwonekano wake halisi zipo?
 
Baada ya waziri wa habari kudai wanasubiri ripoti ya uchunguzi wa uvamizi wa kituo cha runinga cha clouds dhidi ya aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa dar es salaam bw. Paul Makonda imenikumbusha ushauri aliowahi kupewa RC huyo wa zamani na msanii wa kizazi kipya 'Rashid Makwilo' a.k.a 'Chid Benz'...
Inawezekana likatimia!. Chid unaweza kumwona ni chizi lakini maneno yake yana maana kubwa sana na hasa anapozungumzia hali ya magereza na kwamba anybody can be an inmate! Na hii pia inafundisha kwamba cheo for sure ni koti la kuazima
 
inavyoonekana serikali haimpeleki ila watu binafsi but hao watu binafsi watakuwa na backup isiyoonekana
Kesi ikianza kuunguruma kila kitu kitajulikana. Come on next week..
 
Lakini kwa hulka aliyokuwa nayo kijana makonda alipuuza ushauri huo na kuendelea kufanya mambo yake aliyokuwa anaona ni sahihi kwake ikiwemo kusakizia watu kesi za madawa ya kulevya na mambo mengine mengine.
Ktk lile la madawa ya kulevya aliwadhulumu wengi sana mali na fedha zao!
Bado la Bureau de change nalo aliwanyanganya watu wengi fedha zao bila huruma.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom