Kisa Chid Benz, bifu la Lady Jaydee na Ray C laibuka upyaaaaaa

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
18,547
23,322
Bifu lilianzia baada ya hii interview aliyofanyiwa Chid Benz ,Chid alishauri Lady Jaydee akaimbe Gospel miaka miwili akae sawa ndipo arudi tena kwenye bongo fleva .

Sasa lady Jaydee aliona kama hii dharau fulani hivi akajibu mashambulizi πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

-802050257.jpg

Ikumbukwe Lady Jaydee na Chid Benz walishawahi kuwa na bifu miaka hiyo ya nyuma mpaka ikapelekea Lady Jaydee kumfuta na kufuta verse alizofanya Chid Benz kwenye video ya wimbo wa UPO JUU japo si Chid wala Lady Jaydee aliyejitokeza kujibu sababu haswa ilikuwa ni Nini japo habari za chini chini inasemekana Chid akimtongoza Lady Jaydee,Lady Jaydee akaona kama kavunjiwa heshima na Chid ukizingatia amemuacha kiumri mbali sana.Lakini wengine wanadai Chid alimvimbia Lady Jaydee kuna baadhi ya gharama za ziada alikuwa anahitaji ikiwemo nguo za kushutia video,nauli nk maana kipindi hicho alienda Kenya kwenye show ,,Jide akaona isiwe shida akamfuta.

Twende kazi,

Ikumbukwe pia Chidi siku za hivi karibuni amekuwa mtu wa malalamiko kila kukicha akilaumu wasanii wenzake kutomsaidia, mara amlaumu Diamond anarudisha wasanii wenzake nyuma maana anapenda kusujudiwa ,mara amlaumu Manara nk

Tazama moja ya video yake hapa chini πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
1690323947.jpg


Sasa ghafla bin vuuuu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚naona Ray C katoka huku mafichoni kaja kununua ugomvi kana kwamba ujumbe wa Lady Jaydee ulikuwa unamuhusu yeye.

Ray C akarusha kijembe kwa Jide kwamba heri ya yeye mla unga lakini amezaa kuliko Jide ambaye ni tasa.

Tazama hapa πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

-944071203.jpg


Baada ya hicho kijembe Cha Ray C ,Jide akaja tena kujibu mashambulizi .

Tazama tena πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

-576124909.jpg


Mashabiki nao hawakuwa nyuma ,wametoa nao michango yao.

Tazama πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
253073014.jpg


376461081.jpg


Ikumbukwe bifu la Jaydee na Ray C lilidumu kwa muda mrefu kipindi hicho sababu kuu inayoaminika na wengi ilikuwa kugombania kuwa juu kila mmoja kuona yupo juu kuliko mwenzake.

Baadaye hilo bifu liliisha na wakafanya wimbo wa pamoja unaoitwa Namlaumu kama sikosei.

Wakawa marafiki kimtindo na kushirikiana mambo mbalimbali kutembeleana nk.

Tazama hapa picha Yao ya pamoja.


1460313801270.jpg


Tunangojea majibu kutoka kwa Ray C tuone atajibu nini, tupo standbyπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Jide ni mshenzi kama washenzi wengine......
Alisema amemzidi Chidi Umri? Kile kijamaa cha Naija alichodate nacho wapo umri sawa?
Na kuanza kukejeli watu mitandaoni kunaonesha alivyo.
Talent ya kawaida, ila longetivity amefanikiwa.
Ray C talent kubwa Upumbavu wake umempoteza.
Kwenye uimbaji hapo kila mmoja ana ladha yake na wote wanajua na nyimbo zao zinaishi .

Ila Jide mpaka sasa anaweza kutoa hit song kwa upande wa Ray C jahazi limeshazama, si rahisi tena kutoa hit song.
 
Kwa battle ya lady jay dee na ray c ilivyokuwa, kuna mtu atashangaa kuwa na bad blood kati yao

Kwanza tu issue ya Ray c kuwa na Ruge wakati huo huo Ruge akiwa na bifu kali na jide, sidhani kama wangeweza kuiva, Never
 
Ruge alikuwa anawapiga minyama nje minyama ndani x 100 wote wawili hao

ila andiko limeshiba, kama movie vile
Wote walitokea utangazaji wa clouds na chini ya management moja ya smooth vibes iliyosimamiwa na Ruge.
Issue ya lady jay dee na Ruge labda scandal ya kulala hotel moja kwenye tuzo za Kora South Africa, mbali na hapo hakuna mwenye ushahidi mwingine

Ila Ray C ilikuwa wazi sana kuwa anatoka na Ruge na hata jamaa alipofariki aliweka wazi kupitia tweets zake. Sasa imagine Ruge alivyokaa kati kati yao, kuna uwezekano hawa artists wangependana. No way
 
Kwenye uimbaji hapo kila mmoja ana ladha yake .

Jide mpaka sasa anaweza kutoa hit song ila kwa Ray C jahazi limeshazama, si rahisi tena kutoa hit song.
Ray c yupo relevant zaidi kwa lifestyle na kizazi cha sasa. Lady jay dee alikuwa anaiimbia old audience toka kitambo ndio maana licha ya pesa, bado anastruggle kutoa hitz

Ni hii mambo matano at least imepata mileage
 
Back
Top Bottom