Uchaguzi 2020 Huenda Askofu Gwajima akawa ni msaada mkubwa kwa nchi yetu

Atakuwa anafufua wabunge wakifa!!!?? Si ana danganya anafufua watu?

Nchi watu wenye akili wanaisha I see, Gwajima ni tapeli kabisa!
 
Tukiondoa itikadi za vyama na ushabiki usio na maana sana hasa kwa kipindi kama hiki cha uchaguzi, tujikite sasa kuangalia msaada wa mtu binafsi kwa jamii husika. Askofu Gwajima ambaye ni kiongozi wa kiroho upande wa Wakristo na mgombea ubunge Jimbo la Kawe kupitia CCM anaweza kuwa msaada mkubwa kwa jamii. Nitaweka baadhi ya shahidi amabzo kwangu naona ziko sahihi.

1. Askofu kuwa mbunge ni alama tosha kuwa kuna alama ya unyenyekevu inaongezeka bungeni, na huu ndio muda pia maimamu wetu kuamka na kuchukua nafasi bungeni. Hii itasaidia mambo yanayopitishwa na bunge kuwa na maslahi ya kiMungu ambapo Mungu ndio mmiliki wa watu

2. Muamko mkubwa kwenye kampeni za Gwajima ambapo jambo kubwa linaloongelewa na wananchi ni NJOO UTUSAIDIE ASKOFU linaonesha wazi uwezekano wa Askofu Gwajima kuwa msaada unakuja kwa kasi jimboni.

3. Sera za maendeleo zinazotolewa na Gwajima huenda zikaibadilisha Kawe kuwa mpya kama kauli mbiu ilivyo.

4. Exposer yake nje na ndani ya nchi sio ya kubezwa na mtu, ameonekana kuanza maongezi na viongozi wa serikali huku akianza mara moja utekelezaji wa ahadi hata kabla ya kuapishwa. Watu waliokuwa na migogoro ya ardhi kule Chasimba wameishapata jibu lao mapema.

5. Kama Askofu Gwajima atashinda ubunge. Huenda tukaanza kujilaumu kwanini hatukujua mapema tukamshtua agombee ile miaka 10 tuliyokuwa tunaongozwa na Halima Mdee ambaye amemaliza muda wake.

Imeandikwa na;
Mchambuzi Huru

Hongera sana! Naona wewe umechungulia fursa ya kwenda Birmingham Marekani tu sio kitu kingine! Nyau wewe
 
Nyie mnaomtetea gwajima mbona hata kuandika kwenu mnaonekana nyie ni matapeli wenzake?
nani alikuambieni kuwa gwajima ni mtumishi wa Mungu? ( labda awe 'mumgu' mwingine)
 
Back
Top Bottom