Huduma za afya nchini: Mkapa vs Kikwete. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huduma za afya nchini: Mkapa vs Kikwete.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ZeMarcopolo, Jul 7, 2012.

 1. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Sote tunashuhudia jinsi madaktari wanavyomshambulia Rais Kikwete kwa shutuma za kutozipa kipaumbele huduma za afya nchini. Kumbukumbu zangu zinaonyesha kuwa kipindi cha Mkapa hakukuwa na shutuma kali kiasi hiki. Nimejaribu kuchimbachimba ili kujua kwa nini shutuma hizi zimekuwa kali zaidi kipindi hiki nikagundua kuwa:

  1. CT scanner ya kwanza Tanzania ilianza kutumia mwaka 2007 katika hospitali ya Muhimbili. Hii ni baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani. Sote tunajua kuwa madaktari mara nyingi hutumia mfano wa kipimo hichi kuwa ni miongoni mwa vitu muhimu vinavyokosekana kwenye utoaji huduma bora za afya. Rais Mkapa hakununua CT scanner hivyo kuwaacha madaktari wasijue nini wanachokosa, na hivyo wakatulia tuliii. "Kimbelembele" cha Kikwete kutaka kuleta technologia ya kisasa nchini inamgharimu. Sasa madaktari washaijua CT scanner na wanataka zaidi na zaidi.

  2. Magnetic Resonance Imaging machine ya kwanza Tanzania imeanza kutumika mwaka 2009 baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani. Mkapa alijua kuwa akileta hivi vitu, wataalam na wananchi watataka zaidi na matokeo yake "watamuona mbaya". Mkapa aliwafanya watanzania waamini kuwa vitu hivi kwa Tanzania haviwezekani kabisa, Kikwete amejaribu kuonyesha kuwa tunaweza kwa kiasi fulani - wananchi na wataalam baada ya kuona tunaweza kwa kiasi fulani sasa wanataka tuweze "to the fullest".

  3. Kituo cha upasuaji wa moyo nchini kimeanzishwa baada ya rais Kikwete kuingia madarakani. Mkapa alijua kuwa ukishaleta mambo ya upasuaji wa moyo watanzania watataka zaidi, akayaacha. Sasa madaktari wanalalamika kwa nini kituo hicho hakina wataalam na vifaa vya kutosha.

  4. Huduma ya kusafisha damu kwa figo la mashine, dialysis, imeanza kutolewa nchini baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani. Madaktari vijana wamepewa fursa za kwenda nchi mbalimbali kujifunza juu ya huduma hii. Baadhi yao wamesharudi nchini na wanatoa huduma hiyo. Miongoni mwa vijana hao ni viongozi wa mgomo wa kutaka huduma bora za afya na maslahi zaidi. Iwapo Kikwete angefanya kama Mkapa na kuacha huduma hii isipatikane nchini pengine madaktari wangeendelea kuamini kuwa hilo haliwezekani Tanzania na kuwa watulivu.

  5. Baada ya kuona kuwa kuna vijiji havipati kabisa huduma ya usafiri wa wagonjwa, serikali ya Kikwete imebuni utaratibu wa kutumia Bajaj ili kila kijiji nchini kiwe na aina fulani ya huduma ya kwanza ya usafiri wa kuwafikisha wagonjwa sehemu ambayo watapata aidha usafiri bora zaidi au huduma bora ya afya. Jambo hili limefanya serikali ya Kikwete ishambuliwe sana, huku watu wakisahahu kuwa Mkapa aliona bora awaache wanakijiji hap bila huduma yoyote. Kwa vile Mkapa alikaa kimya kabisa kuhusu hili, hakulaumiwa. Kimbelembele cha Kikwete kutafuta utatuzi wa matatizo ya watu wa vijijini umemponza, sasa analaumiwa kwa kubuni njia ya kwasaidia watanzania.

  6. Hivi sasa Kikwete anajiandalia tena "bomu" lingine kwa sababu serikali yake imeshaanza kutuma madaktari vijana wakajifunze Afrika Kusini na Ulaya jinsi ya kufanya operesheni kwa kutumia kamera (laparoscopic operations), vijana hawa wakirudi watafunguliwa vituo vya kufanya operesheni hizo ambapo mtu anaweza kufanyiwa operesheni ya tumbo na kurudi nyumbani siku hiyohiyo bila kovu! Ninapata hisia kuwa vijana hawa nao wataanzisha mgomo wa kutaka huduma iwe ya kiwango cha juu kama kule walikotoka kujifunza na kumtupia lawama muasisi wa utamaduni wa kuheshimu taaluma ya udaktari kwa kuwapa madaktari wa Tanzania exposure.

  Nyongeza: Utamaduni huu wa Rais Kikwete kuleta maendeleo ya kweli umemgharimu pia katika sekta ya elimu ambapo alihamasisha kuwepo kwa shule za kata na kuwapa fursa watoto ambao wangekosa kabisa elimu kupata angalau fursa fulani ya kuelimika kwa kiwango fulani. Hivi sasa shule za kata ndio zimekuwa kigezo cha kulaani jitihada za serikali kwa kuwa wanafunzi "wanafeli". Kikwete angewaacha waishie darasa la saba kama ilivyokuwa kipindi cha Mkapa na marais wengine, wasingekuwa shule, hata kufeli wasingefeli na Kikwete asingelaumiwa kwa matokeo mabaya.

  Hofu: Kwa mafunzo haya yanayotolewa na wananchi kwa Kikwete, Rais ajaye atatakiwa kuchagua mtindo wa Mkapa au Kikwete! Mpaka hapa tulipo inaonekana kuwa mtindo aliotumia Mkapa una manufaa zaidi kwake na chama chake kisiasa, lakini je vipi kuhusu maisha halisi ya watu wetu?

  Nini kifanyike: wataalam, wanaharakati na wananchi ni wajibu wao kudai huduma bora na kuishinikiza serikali ifanye kila liwezekanalo kutoa kilicho bora zaidi kwa watu wake. Hata hivyo makundi haya yanawajibika kutambua, kuheshimu na kutamka hadharani jitihada za viongozi wanaojitoa kimasomaso kuzisaka huduma bora kwa watanzania ili kuwatia moyo waendelee kufanya hivyo. Tukilalamika zaidi kuliko kuonyesha moyo wa shukurani tutaishia kuambiana "LIWALO NA LIWE".
   
 2. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  "liwalo na liwe"
   
 3. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  Haya ni maoni yako, maoni ya wengi wanasema hali ilikua nzuri katika sekta zote kipindi cha Mkapa na ni mbaya kipindi hiki. Labda hizo mashine hazijakidhi matarajio au hazijafanya kazi kutokana na ukosefu wa umeme; na hivyo vyumba vya madarasa (ambavyo wananchi wamejenga kwa nguvu zao na katika kiwango cha chini sana) havijainua ubora wa elimu.

  Fanya utafiti ujue kwanini wanalalamika kabla ya kusifia. Wananchi walimchagua Kikwete kwa zaidi ya 80% mwaka 2005, hawawezi kuwa kipindi hicho walikua na akili halafu sasahivi wamebadilika wakawa vichaa na kuanza kumlalamikia kwa kutendewa mazuri. Walitarajia awafute machozi ya mapungufu yaliyokuwepo serikali iliyopita, bado hajafanikiwa. Nakumbuka alisema hili ni deni kubwa kwa serikali atakayoiunda, sasa limekua gumu kulilipa.


  Binafsi nachukizwa na maneno yasiyoendana na matendo! Kwa mfano, Pinda alikataa shangingi mpya na akasema serikali haitanunua tena mashangingi, mwaka huo huo wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama (Polisi, Takukuru, Usalama wa Taifa, JWTz etc) wakapewa gari la pili aina ya Range Rover Vogue. Wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa mikoa, wakuu wa idara ndani ya wizara na ofisi mbali mbali za serikali woooote wanatumia Mashangingi wa wanaendelea kunua mapya! Hawa wote saizi yao ni RAV4.

  Kwa kifupi fanya utafiti, inawezekana wengi au wote hatumjadili JK kwa kumlinganisha na mtangulizi wake, bali tunalinganisha ahadi zake na utekelezaji, pamoja na fursa zilizopo. Sasa ukichukua ahadi ile kubwa kabisa ya Ari mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya, hatuioni hasa katika kupamba na ufisadi. Halafu ukichukua ile nyingine ya Maisha BORA kwa KILA mtanzania, hapo ndio kabisaa machozi yatakutoka! TUSIFIE LIPI?

  Niache mie niwahi nikamnyonyeshe ndama wangu!
   
 4. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hao wanaosema huduma zilikuwa bora kipindi cha Mkapa ni wataalam?
  Kama ni wataalam maana yake ni kwamba hiyo mitambo na wataalam alioleta Kikwete sio muhimu. Na kama sio muhimu kwanini tunataka viongezwe wakati tunaona vilipokosekana mambo yalikuwa poa zaidi?
   
 5. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  "Ukiwa unakula na kipofu usimshike mkono"
  Hata Kichaa huwa anajiona ndio ana akili kuliko wengine.
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  ZeMarcopolo, utaratibu wa kutoa huduma vijijini kwa kutumia bajaj ulibuniwa na UNFPA. Na hata hizi kelele wanazopiga kuwa wameimarisha afya ya mama na mtoto huu nao ni mpango wa UNFPA, infact Tanzania walikuwa miongoni mwa nchi za mwisho kuuzindua huo mpango kwa sababu ya porojo za serikali. Wakati mwingine kama hujui mambo uliza.

  i.e Kama huduma za afya zimeboreka sana kwanini idadi ya vigogo wanaotibiwa nje ya nchi ni kubwa kuliko ilivyokuwa huko nyuma?
   
 7. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Tatizo la watanzania ndio hilo. Linapofanyika baya lawama ni za kiongozi, likifanyika zuri basi limefanywa na mwingine. Sasa hao UNFPA wamejikuta wamedondoka tu Tanzania kama mvua?
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Wewe unawajua UNFPA? Au unataka kutuambia kuwa UNFPA wameletwa na serikali? Unajua kitu kinachoita Project funds au Basket funds?
   
 9. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #9
  Jul 7, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Tambua kuwa serikali kushirikiana na wadau mbalimbali kuleta maendeleo kwa watu si jambo jipya na wala si jambo linalofanyika Tanzania tu. Bila jitihada za serikali hakuna cha UNFPA wala mdau wowote atakayekuja nchini. Jiulize, kwani UNFPA imeanzishwa baada ya Kikwete kuingia madarakani?
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kipindi cha Kikwete tumeona "life span" imepanda kwa miaka zaidi ya miaka 5 kwa miaka 7 tu. Haijwahi kutokea kabla yake, wakati Nyerere anamuachia Mwinyi madaraka "life span" ya Mtanzania ilikuwa miaka 48 tu. Kipindi cha Mwinyi na Mkapa ikapanda miaka 2 (imagine kwa miaka 20 imepanda kutokea 48 na kufika 50), kipindi cha Kikwete imepanda na kufika 55, ni miaka 7 kwa miaka saba tu. Halafu huyo huyo anaonekana mbaya kwenye afya.

  Life span aliyoacha Nyerere 48 years - Miaka 24 ya kutawala
  Life span waliyoacha Mwinyi na Mkapa 50 years - Miaka 20 ya kutawala
  Life span iliyopo wa huu wa Kikwete 57.4 years - Miaka 7 ya kutawala. (rikodi ya dunia).

  Source: http://www.google.com/publicdata/explore?ds=d5bncppjof8f9_&met_y=sp_dyn_le00_in&idim=country:TZA&dl=en&hl=en&q=tanzania+life+span#!ctype=l&strail=false&bcs=d&nselm=h&met_y=sp_dyn_le00_in&scale_y=lin&ind_y=false&rdim=region&idim=country:TZA&ifdim=region&hl=en_US&dl=en&ind=false

  Afya haipatikani hospitali pekee, ni kuanzia kwenye lishe, namna ya kukinga maradhi, huduma za mwanzo (vituo vya afya).

  Hakuna aliyemfikia Kikwete kwa hayo yote. Vituo vya Afya na zahanati ni vingi zaidi kuliko wakati wowote, huduma ya mwanzo ni kubwa zaidi kuliko wakati wowote (vibajaji ni mfano mzuri), Kuzuwia maradhi (vyandarua ni mfano mmoja wapo).

  Rais Kikwete alipoingia madarakani tu alikutana na matatizo sugu na makubwa matatu aliyoyarithi kutoka kwa Mkapa nayo ni; Njaa, Umeme na Ujambazi (nani asiyekumbuka?). Na akayashughulikia hayo ipasavyo. Bado tu ni mbaya?
   
 11. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #11
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  Wanaosema hivyo sio wataalam, ni wapata huduma!, Madakitari na wataalam wengine hawamlinganishi JK na Mkapa, wana-judge kwa kuangalia opportunities zilizopo za kufanya zaidi ya yaliyofanyika. Kwa mfano juzi tu mmoja amesema bei ya Mashine 1 ya CT Scanner ni sawa na bei ya shangingi 1. hii ni dhahiri hawamlinganishi na mtangulizi wake, bali na hali halisi.

  Mkapa hawakumlalamikia sana kwasababu alifanya alichoahidi, aliwaambia wananchi wafunge mkanda atabana sana ili arekebishe mfumuko wa bei aliouacha mwinyi (akautoa 32% mpaka 4%) na ili alipe madeni waliyoyaacha watangulizi wake ikiwa ni njia muhimu kuelekea kujitegemea kiuchumi na kimaamuzi (akalipa sana tu). Ukweli ndio uliomuokoa.
   
 12. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #12
  Jul 7, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Mwananchi wa kawaida ambaye siyo mtalaam hawezi kujua umuhimu wa vifaa na wataalam waliokosemakana kipindi cha Mkapa. Ingekuwa ni wataalam wamesema hivyo tungekuwa na la kujadili.
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Kwa bahati nzuri nafahamu vizuri idea ya Bajaj ilikujaje na ndio maana nacheka sana kusoma propaganda hapa. Na hata hiyo programme ya maternal health nimeitaja makusudi kwa sababu ina connection na Bajaj ambulance. Sitoshangaa kusikia unasema kuwa serikali ndio inagharamia hivyo vitu!
   
 14. B

  BMT JF-Expert Member

  #14
  Jul 7, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  mkapa alijikita zaidi na miundombinu hasa barabara za lami,we mleta mada acha uongo,uzandiki na ushakupena,halaf una matatizo kumlinganisha mkapa na kikwete,HUJUI MKAPA ALIYOYAFANYA,Namkubali jk lakni katika unafki wako huu siko tayari kukuacha ukipotosha ukwel
   
 15. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #15
  Jul 7, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Tatizo la vijana wa leo, wengi wao hawajadili kwa kutumia evidence. Wanafuata mkuombo. Haya sasa mnapewa data hapa, kama mna data za kujibu hili leteni lakini siyo kujibu kwa hisia.
   
 16. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #16
  Jul 7, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Mkuu, tunajadili sekta ya afya. kama yapo aliyofanya Mkapa tujulishe. unakumbuka Mshahara wa daktari ulikuwa sh. ngapi wakati Mkapa anatoka madarakani?
   
 17. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #17
  Jul 7, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Unaelewa vibaya. Hakuna aliyesema vimegharimiwa na serikali. Tunachojadili hapa ni uwezeshaji wa upatikanaji wa huduma. Serikali kuwezesha wananchi kupata huduma sio lazima itumie pesa za walipa kodi, inaweza kushirikiana na wadau mbalimbali kwa namna mbalimbali lakini mpaka mwisho cha muhimu ni kwamba mwananchi amepata huduma.
   
 18. k

  kabenge Member

  #18
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hacha uongo kumtetea mhuza sura CT scaner zilikuwepo toka 2004 pale BUGANDO, KCMC,na MHUHIMBIL mie nimetibiwa pale BUgando kwa 2004 zilikuwepo
   
 19. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #19
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Porojo zinazosaidia ni njema sana kuliko porojo zisizo saidia.

  Utawala wa kabla ya Kikwete ulikuwa wapi? usiwe wa mwanzo? mpaka anakuja Kikwete ku rescue bado ni mbaya? au UNFPA ilikuwa haipo? fikiri.
   
 20. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #20
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  Lipi ambalo limeisha au limepungua? Tatizo la njaa na umeme lipo pale pale, na pengine limeongezeka. Juzi tumetangaziwa TANESCO imefilisika. Ujambazi umebadilika tu, kutoka ule wa kutumia silaha mpaka ule wa kwenye mtandao! TUWE WAKWELI.
   
Loading...