Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,143
- 10,549
Ndugu abiria tunapenda kuwafahamisha kuwa ndani ya basi letu tuna huduma ya choo kwa ajili ya haja ndogo pekee! Kama utakuwa na uhitaji wa ziada usisite kuomba msaada wa kondakta.
Hii ni kauli ambayo Inatolewa Na wahudumu wengi ndani Ya mabasi haswa ukiwa safarini. Na huwa wanasisitiza kuwa choo kitumike tu endapo utapata dharura ya haja ndogo (kukojoa).
Je, wewe binafsi kuna changamoto yoyote umewahi kuipata haswa kwenye matumizi ya Choo Safarini.
Ni kwamba mabasi yamekosa nafasi ya kutoa huduma ya haja kubwa, ama ni watu kukosa ustaarabu wa matumizi? Maana kuna watu wameshakula mayai ya kuchemsha pamoja na mahindi ile wakienda kushusha mzigo ni mzigo haswa kiasi kwamba basi lote litajaa harufu kali.