Huduma ya Maktaba Tanzania ikoje?

JUU YA HUDUMA YA MAKTABA YA TANZANIA

maktaba2.jpg

Mheshimiwa Spika, ningependa kumuuliza mheshimiwa Waziri Mhusika maswali yafuatayo ya msingi:

a. Serikali itaanza lini kujenga maktaba mpya na za kisasa katika jiji la Dar ili kuchangia katika upatikanaji wa habari, kuchochea usomaji na kuwapatia wanafunzi na watumishi mahali mbalimbali mahali pa kukusanya taarifa, kufanya utafiti na vile vile kujisomea na kuchochea mapenzi ya vitabu?

b. Je, ni watumishi wangapi wa TLS ambao wana utaalamu katika mambo ya Maktaba na kati yao ni wangapi wako kwenye utawala wa bodi hiyo makao makuu?

c. Je Maktaba kubwa kabisa iliyo chini ya TLS ina uwezo wa kuchukua watu wangapi?

d. Je, maktaba hizi zote zimeuunganishwa katika mtandao wa kikompyuta ambapo unamuwezesha mkazi wa Mbeya kutumia maktaba ya Dar au Arusha au sehemu nyingine yoyote nchini kwa kadiri ya kwamba maktaba ziko chini ya TLS?

e. Kwanini mfumo wa sasa wa maktaba usivunjwe na kuundwa upya ambapo huduma ya maktaba iachiwe halmashauri za miji kusimamia na kugharimia kwa kadiri ya uwezo wao na kuwa watakiwe kisheria kufikia kiwango fulani ili waweze kupata kiasi cha pesa za uendeshaji wa maktaba hizo kuliko mfumo ulivyo sasa ambao uko centralized utadhani tunaishi kati nchi ya udikteta wa chama kimoja cha kisiasa?

Nitarudi tena mheshimiwa spika.
Hoja hii ni sawa na kwa kweli Bodi ya Huduma za maktaba ifanye utafiti wa ni jinsi gani fani hiyo imevamiwa na hiyo kuharibiwa ufanisi wake.Kama ilivyo kwa ualimu,udaktari,uasibu n.k.fani ya wakutubi ifanyiwe kazi na wenye sifa hiyo tu na si vinginevyo.
 
kusoma huleta maarifa mengi hadi jinsi ya kujipatia chakula..hata kama unakula Muhogo mmoja kwa siku jitahidi kusoma ukipata muda utaona tu faida zake. Hili la kuwalisha watu woote kwa muda woote hata MANABII mmaarufu sana hawakuweza!

Burn, vipi ndugu yangu yaani hujui kuwa kuna watu walikuwa hawali chochote hata siku mbili lakini walinga'ngania kusoma na sasa hivi wengine ni Marais wa nchi!

Siyo kwakiasi chote, lakini kusoma ni kwa kiasi kikubwa kunafungua mabo mengi sana duniani....siyo kupiga domo tu!

Yaani kwasababu huwezi kula kila dakika ndiyo ubweteke! ufanye nini sasa? upige Lamli!! kusoma ni kuatafuta maarifa lazima yatafutwe kila wakati.
Hata huyo Mwalimu Jk werevu wake mwingi aliupata kwa kupenda kusoma.
 
Bado nadhani ndugu haujui hali halisi,katika jamii zetu kuna watu wasio na uwezo wa kupata hicho kipande cha muhogo and u know what? watu hao ni wengi mno. Nilikuwa nina msimamo kama wako kuwa tunahitaji kuwahimiza watu wetu wasome ili kujikomboa, kwa bahati nzuri au mbaya(nasema inaweza kuwa mbaya kwani nilibadili msimamo) nikakutana na watu wenye mawazo kama hayo na walikuwa na pesa za kufanya mradi huo. Tulipokwenda handeni kwa kazi hiyo tulibadili muelekeo ndani ya mwezi mmmoja wa mradi, kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nilishudia binadamu akiishi kwa kikombe kimoja cha uji kwa siku, hapo tulikuwa na pesa zetu za kununulia madaftari na kutoa motisha kwa wanafunzi bora ilibidi tuzitumie kununua chakula na mbegu na kugawia familia zilizokuwa na shida zaidi. Nadhani katika hali kama hiyo hata uwapatie kila kitu cha kusoma hautoweza kuwaelimisha.

Kama unafahamu Abraham Maslow's needs hierarch nadhani utakuwa unanielewa vizuri. Suala la kusoma au elimu haliwezi kuja kabla ya suala la kula wala haviwezi kuwa sawa katika mpangilio wa mahitaji ya binadamu. Ni lazima binadamu ale ashibe then hayo ya elimu yanaweza kufuata baada ya hapo.
 
MMJ
Hilo jengo lote siyo maktaba. Hizo gorofa za juu wamepangisha mawakala wa meli.
Siyo Mawakala wa Meli tu, hata ofisi za Tanroads na Cotecna ziko hapo. Swala hapa ni je huduma zitolewazo na Maktaba Tanzania zikoje na wala siyo jengo.
 
Nadhani katika hali kama hiyo hata uwapatie kila kitu cha kusoma hautoweza kuwaelimisha. Kama unafahamu Abraham Maslow's needs hierarch nadhani utakuwa unanielewa vizuri. Suala la kusoma au elimu haliwezi kuja kabla ya suala la kula wala haviwezi kuwa sawa katika mpangilio wa mahitaji ya binadamu.Ni lazima binadamu ale ashibe then hayo ya elimu yanaweza kufuata baada ya hapo.

Nadhani wewe pia ni mtu wa kuwajali watu wengine saana, ubarikiwe kwa hilo. Umasikini, ni kweli kabisa nchi yetu inasikitisha kweli, Handeni! pole kwa uliyoyaona mimi nilikwenda Tundu mwaka jana, niliangua kilio!!
Hilo nalo ni mada ya peke yake baba, tukiwa tuna changanya mada tutashindwa kujadili chochote! Maana mwingine atasema mafisadi wamelamba pesa zoote ndiyo maana hatusomi, mwingine atasema kile n.k

Hapa tunsema kusoma kama kusoma, jinsi kulivyo na umuhimu. Hatuwezi kuacha kufikiria kuwapa watu vitabu kwa sababu nchi ina masikini wa kutupwa, hamna siyo hivyo...tunaweza kuwa masikini zaidi.
 
Watanzania wengi ni wavivu wa kusoma vitabu, Hakuna haja ya kuwa na maktaba nyingi wakati hii moja ya Jijini Dar huwa haijai. Nadhani kuna haja ya kuwaelimisha wanafunzi na watanzania wote kwa ujumla juu ya umuhimu wa kusoma vitabu, ndio swala hili lifuate.
 
naona pia si jadi ya watanzania kujisomea, nilienda mktaba flani ya mkoa nataka kusoma kitabu nilijua kipo pale but walitaka ID ya shule au chuo, nkawaambia mimi mfanyakazi walikataa katakata kuniruhusu, so unaona hakuna mwamko au mvuto, au upigadebe wa kujisomea mambo tofauti na mengi, imekaa kisiasa tu pale 'Mwanasihasa' anapozindua kijarida na kuwasihi watu kujisomea, kweli bado hatuhitaji maktaba labda kuwepo na secondary service kama bia ndani ya maktaba oky watz tutaingia kusoma na kunywa kama sio kunywa na kusoma!!
 
Hapa tunsema kusoma kama kusoma, jinsi kulivyo na umuhimu. Hatuwezi kuacha kufikiria kuwapa watu vitabu kwa sababu nchi ina masikini wa kutupwa, hamna siyo hivyo...tunaweza kuwa masikini zaidi.

Hapo kweli ninahitaji kukalia kichwa ili nijue umuhimu wa makalio..lol
 
a. Asilimia 30 ya Watanzania walio katika umri wa kujua kusoma na kuandika hawajui mambo hayo.

b. Maktaba ambazo ni sehemu za bure za watu kuweza kujisomea ziko katika hali duni na kama alivyosema ndugu yangu mmoja ni "prehistoric". Hakujawa na mwamko wowote wa kuhamasisha watu kujisomea maktaba (siyo kununua vitabu au magazeti). Yaani bure kama sisi wengine tulivyojisomea enzi zile kwenye maktaba ya Tanga kila Jumamosi!

Ni kutokana na hayo naamini kuwa serikali ya CCM inapenda kutawala watu wasiojua kusoma na kuandika.
 
Tanzania for change msingi wake ni elimu tuu ndio mradi wetu mama maabara na videoconference lecture zitatolewa nchi nzima bure
 
Nahisi kuna baadhi ya ndugu zetu watanzania hamjui kabisa hali za watanzania wenzenu, hivi kweli unaweza kutoa wazo hili eti soma tu hata ukipata mhogo mmoja, ndugu yangu tema mate chini kama haujawahi kuisikia njaa au umebahatika kupitiwa mbali na janga hili.

Asante sana kwa kunisaidia kujibu hili suala. Huyu mwenzetu ni wazi haelewi nini maana ya njaa. Kuna watu hata kuupata huo muhogo ama kipande cha kiazi ni taabu. Sasa atasomaje katika hali hiyo?. Usiombe janga hilio likukute hata siku moja. Unakwenda shuleni tumboni hakuna kitu na shule zetu za Tanzania hazitoi chakula, hakuna kinachoweza kuingia akili na mwalimu unamuona kama mdudu tu anakupigia kelele zisizo na maana.

Tanzania tuna safari ndefu sana. Watu wengi wanashindwa kupata mlo kwa siku, na hata kama wanapata basi ni ule mlo ambao bora tumbo lijae.
 
Asante sana kwa kunisaidia kujibu hili suala. Huyu mwenzetu ni wazi haelewi nini maana ya njaa. Kuna watu hata kuupata huo muhogo ama kipande cha kiazi ni taabu. Sasa atasomaje katika hali hiyo?. Usiombe janga hilio likukute hata siku moja. Unakwenda shuleni tumboni hakuna kitu na shule zetu za Tanzania hazitoi chakula, hakuna kinachoweza kuingia akili na mwalimu unamuona kama mdudu tu anakupigia kelele zisizo na maana.

Tanzania tuna safari ndefu sana. Watu wengi wanashindwa kupata mlo kwa siku, na hata kama wanapata basi ni ule mlo ambao bora tumbo lijae.

Mkuu, naona hunisoma sawa sawa. Suala la umasikini wa kutupwa wa nchi yetu hata mimi unanitapisha kabisa! Lakini suala la kuwafanya watu wasome ni muhimu sana tu pia!!
Hilo la mlo 1 kwa siku mbili ni maada nyingine.....please tusichanganye mambo jamani!
 
Hivi kuna nchi ambapo kuna maktaba za watu binafsi(Private) Naona wazo hili linawezekana TZ. Maana watu kama British Council walijitoa na sijui ni kwanini?
 
Maktaba, Maktaba, Maktaba... tangu enzi na enzi.. walioweza kusoma ndio walioweza kutawala wenzao au kuongoza. Wale walioonekana angalau wanajua... na mara zote wale walioonekana wanajua wanapokutana na wale wasiojua huwatawala... Mtu mwenye kujua huwa anauliza maswali; anahoji..hakubali kirahisi rahisi tu..
 
Back
Top Bottom