Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,991
JUU YA HUDUMA YA MAKTABA YA TANZANIA
Mheshimiwa Spika, ningependa kumuuliza mheshimiwa Waziri Mhusika maswali yafuatayo ya msingi:
a. Serikali itaanza lini kujenga maktaba mpya na za kisasa katika jiji la Dar ili kuchangia katika upatikanaji wa habari, kuchochea usomaji na kuwapatia wanafunzi na watumishi mahali mbalimbali mahali pa kukusanya taarifa, kufanya utafiti na vile vile kujisomea na kuchochea mapenzi ya vitabu?
b. Je, ni watumishi wangapi wa TLS ambao wana utaalamu katika mambo ya Maktaba na kati yao ni wangapi wako kwenye utawala wa bodi hiyo makao makuu?
c. Je Maktaba kubwa kabisa iliyo chini ya TLS ina uwezo wa kuchukua watu wangapi?
d. Je, maktaba hizi zote zimeuunganishwa katika mtandao wa kikompyuta ambapo unamuwezesha mkazi wa Mbeya kutumia maktaba ya Dar au Arusha au sehemu nyingine yoyote nchini kwa kadiri ya kwamba maktaba ziko chini ya TLS?
e. Kwanini mfumo wa sasa wa maktaba usivunjwe na kuundwa upya ambapo huduma ya maktaba iachiwe halmashauri za miji kusimamia na kugharimia kwa kadiri ya uwezo wao na kuwa watakiwe kisheria kufikia kiwango fulani ili waweze kupata kiasi cha pesa za uendeshaji wa maktaba hizo kuliko mfumo ulivyo sasa ambao uko centralized utadhani tunaishi kati nchi ya udikteta wa chama kimoja cha kisiasa?
Nitarudi tena mheshimiwa spika.

Last edited by a moderator: