A
Anonymous
Guest
Hali ya maji Ubungo ni mbaya sana na DAWASA wapo kimya, hawatoi solution kwa Wananchi, kuna baadhi ya maeneo wiki ya nne sasa hatujapata maji, wenzetu wa Mabibo Makutano - Mtaa wa Kanuni nao ndio kabisa, maji kuna muda yanatoka kidogo tena kwa saa moja tu hali ambayo imedumu tangu Oktoba 2025.
Suala la maji imekuwa kama tunaomba msaada, wakijisikia wafungue kisha wakae miezi kadhaa ndio watoe tena huduma, tunajikuta tunatumia gharama kubwa katika kununua maji licha ya kuwa tuna miundombinu yote ya mabomba.
Upande wa Ubungo maeneo kama Kimashi, Kilungule, Baruti, Makopo na sehemu nyingine nyingi zina changamoto zaidi ya mwaka sasa maji ni ya kusuasua na hakuna solution yoyote kutoka kwa mamlaka ya maji.
Juzi Waziri wa Maji Juma Aweso anasema kina cha maji kimerejea na maji yanatoka kwamba ile hali ya mpito imepita lakini hakuna mabadiliko ya ukweli kama anayosema akiwa jukwaani.