Habari wakuu,
Baada ya majaribio na kadhalika, sasa unaweza kupiga simu kupitia whatssap kwa mtu yeyote ambae yupo kwenye contact list bila kuhitaji activation kutoka kwa mtu yeyote kasoro kwa wale ambao hawaja-update application yao ya whatssap kwa muda, ambao nao ni kuapdate tu na kufanikisha.
Japo zilikuwepo Apps nyingi zenye feature ya kupiga simu kama viber, tango na nimbuzz, lakini hazikuwa na customer base kubwa kama whatssap ambayo sasa imefikia milioni 700+ na tayari imeshazua taharuki kwa wamiliki wa mitandao ya simu kwa kuona watapoteza sana kipengele muhimu zaidi katika faida yao hasa sehemu ambazo internet inatumika kwa kiwango kikubwa na haina usumbufu pia watu wengi zaidi wanamiliki vifaa ambavyo vina uwezo wa kudaka whatssap.
