Huawei yajidhatiti

Huawei yajidhatiti

Mbona taarifa kutoka Huawei inasema kua OS yao itakua inauwezo wa ku support apk za Android! So nadhani mtu anaweza download apk ya dream league na akacheza, Mbali na hapo wako kwenye mazungumzo na yule Mreno mmiliki wa Aptoide wanataka waifanye kwa muda kama mbadala wa Playstore itakayokuja na OS yao huku wakiendelea kujipanga zaidi japo wana App Gallery pia.... Ngoja tuendelee kufatilia tuone hatima yao japo kazi wanayo sana...
Ku support apk sio issue pia sababu kuna os tayari zinasupport apka kama vile tizen ya samsung, sailfish os ya Jolla na BB10 os ya blackberry na zote hazikufanikiwa. Kuna mambo mbalimbali kama vile
-kuto support google service, hapa haimaanishi tu app za google ndio zitakuwa hazipatikani bali app zote ambazo zinahitaji hii service mfano hio app niliyoitaja hapo juu yaani snapchat, hata uki sideload apk haitafanya kazi.
-runtime, kama utakumbuka android za zamani kama vile jelly bean kushuka zilikuwa zinatumia dalvik runtime ilikuwa slow sana na android ilikuwa nzito baadae google akahama kwenda art tukaona mabadiliko makubwa kuanzia kitkat, os zote zinazosideload apk zinakuwa na tatizo hili inachukua muda sana toka uclick app ya android mpaka kuja kufunguka. Ngoja tuone kama wana maajabu ila nategemea hapa pia kuwa na tatizo.
 
Akifanikiwa kuwa convice makampuni yote ya kichina kutumia OS yake atakuwa amemaliza.
Maana simu zote % kubwa ni Chinnes
 
Alishindwa blackberry hii vita tena wakati ule ndo alikuwa smartphone super brand huku android ndo kwanza ilikuwa inachipukia lakini ikaibuka kidedea hadi wakaruhusu android platform kwenye balackberry os lakini wapi na leo hii wameamua kuungana tu na android mana hakuna namna.
Kampuni za kimarekani sio nzuri kwenye mashindano ya kibiashara hata kidogo. China wameendelea sana ila bado wanasafari ndefu sana kuifikia Marekani, wasipokuwa makini wanapotea kama walivyopotea wengine.
 
Tumebarikiwa sana tunaoshuhudia vita hii ya kihistoria kwenye ulimwengu wa technology,
Ila leo nimeona kwenye blog fln hivi habari inasema eti "HongMeng OS (android alternative ya wachina inayotengenezwa na huawei) inazidi hii android ya Google speed kwa asilimia 60"
Sina uhakika ni hii habari japo inaweza kuwa kweli coz blog hio imeripoti kwamba "GLOBAL TIMES" ndo wametangaza hivo.

Cc CHIEF MKWAWA
Mi mwenyewe nimeliona hilo tangazo, wanasema itaitwa Ark OS sasa swali langu ni vipi wanapima hiyo speed difference na kwa tekinolojia gani wanatumia kutambua hilo?
Wanaonekana kujiandaa kweli maana wamesha sambaza copy 1.million za simu zao zinazotumia hiyo OS kufanya test.
 
Back
Top Bottom