How to Negotiate Anything with Anyone Anywhere Around the World

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,221
1,788
Jina la Kitabu.How to Negotiate Anything with Anyone Anywhere Around the World

Jina la Mwandishi.Frank Accuf

Mchambuzi.Nanyaro EJ



Utangulizi:

Mwandishi anasema kitabu hiki ni mwongozo kwa yeyote ambaye angependa kufanya majadiliano(Negotitions)na watu mbalimbali au taasisi mbalimbali za kimataifa zenye historia na desturi tofauti tofauti,pia zenye uzoefu na wazoefu wa kila aina.Kwa mtu ambaye angependa kufanya negotiating ya Kimataifa na kwa bahati mbaya hakufanya maandilizi ya kutosha,basi hiki kitabu ni chake na kitampa mwongozo bora

Mwandishi anasema kuwa kitabu hiki ni matokeo ya somo/darasa alillojifunza baada ya kushindwa.Ni matokeo ya mambo ambayo anatamani angepata mtu ambaye angemwambia kabila na kumfundisha kabla,ya kuingia kwenye global negotiations

Kama una mwingiliano na watu wa kada mbalimbali,desturi mbalimbali au kibiashara au katika safari za kawaida,basi hiki kitabu ni chako.Kama huko nyuma umepata ugumu wa kufanya biashara au mwingiliano wa kawaida na watu wengine,basi hiki kitabu ni chako.Kimsingi hiki kitabu ni cha yeyote ambaye katika maisha yake ya kila siku anakutana na kufanya kazi na watu(binadamu),hiki ni kitabu kwa ajili ya Madaktari,wajasiriamali,wanasheria,wanadiplomasia,na kada nyingine za watu ambao wanajishughulisha na watu

Hivo basi kitabu hiki kitakusaidia kuepuka makosa ambayo hufanywa na wengi hasa linapokuja swala la negotiation za kimataifa.Pia kitakujenga kiakili,kitakusaidia kukuongoza katika mchakato muhimu hatua kwa hatua,kitakupa ubunifu wa kitamaduni na uelewa mpana wa namna ya kusoma mchezo

Mwandishi anasema kitabu kitakusaidia na kukufungua kutambua ni wakati gani unapaswa kusema hapana na wakati gani wa kusema ndio,kitakupa mbinu ya kujua makubaliano yepi ukubali na yepi ukatae

Mwandishi ataelezea mbinu na mikakati ya maeneo ya Kidunia kutokana na mila na desturi za eneo husika,mfano Ulaya Magharibi,Ulaya Mashariki,Latin Amerika,Mashariki ya Kati,Afrika ya Kaskazini,Afrika kusini mwa jangwa la Sahara.Kila ukanda una tabia zake,tamaduni,mila na desturi…ungana name ukae kwenye ramani ya Ulimwengu
 
WATANZANIA bhana.Umepewa jina la kitabu,mwandishi alafu unasema eti tupia kitabu,fikiri tofauti.
 
Jina la Kitabu.How to Negotiate Anything with Anyone Anywhere Around the World
Jina la Mwandishi.Frank Accuf
Mchambuzi.Nanyaro EJ

• C H A P T E R 1 •

Negotiating in Any Language: How Negotiations Work

Mwandishi anasema kuwa lazima uwe na kiasi…ongea kidogo ya kile ujuacho,yaani usiwe mjuaji,maneno kidogo matendo mengi! Anasema negotiation ni swala kwenda na wakati na majira,kunamambo huamuliwa na muda(nyakati na majira() ambayo katika hali ya kawaida yangekuwa magumu,mfano Dunia ya leo inaendeshwa na kanuni mbalimbali lakini swala la Teknolojia ndio linaloongoza,na utandawazi wa kidunia(Dunia imekuwa kwenye kiganja)
Mwandishi anasema kuwa miongoni mwa watu ambao walikuwa negotiator mzuri ni Musa(Yule nabii tunayemsoma kwenye vitabu vitakatifu)anasema Nabii Musa aliongoza vizuri,negotiation sio tu wakati wa kwenda kwa farao bali hata wakati wa kupewa amri kumi na Mwenyenzi Mungu,alikaa mlimani siku arobaini,aki negotiate
Mwandishi anasema kuna MSINGI wa Ku negotiate ambao unaweza kufanana bila kujali eneo Iwe upo Afrika,au Amerika au Ulaya,Au upo Dodoma,au Pretoria,au Toronto,msingi huu ni pamoja na
1.Kuelewa dhana nzima ya Negotiation
2.Kuwa na uwezo wa kupanga negotiation yako
3.Kuelewa dhana nzima ya Win-Win
4.Kutambua umuhimu wa kufunga/kufikia hitimisho la dili

Hii ni baadhi ya misingi mikuu katika majadiliano yoyote yale,ingawa ipo misingi Zaidi yah ii.Mbinu na mikakati ambayo tutaiona ni ile ambayo tuliitumia tukiwa wadogo,yaani mbinu na stadi ambazo huwa tunafundishwa tukiwa wadogo,lakini husahau kwa kadri umri unavoongezeka,mfano mtoto hajui maana ya neno HAPANA,watoto hutambua kuwa pale mkubwa wake anapomwambia HAPANA huwa anamaanisha Hapana kwa 50% na ndio kwa 50%,,watoto huwa hawakwaziki kirahisi,watoto huwa na uwezo mkubwa wa kumsoma mkubwa kuliko uwezo wa mkubwa kumsoma mtoto

Negotiating ni mchakato wa mawasiliano wenye lengo la kufikia makubaliano dhidi ya mahitaji tofauti,au mawazo tofauti,mchakato huu unapaswa kuwa wa matumizi ya akili tu na sio matumizi ya nguvu hata kidogo,ndio kusema mchakato huu unahusisha mawasiliano kwa lengo la kuuza au kununua,au kutangaza,unaweza pia kuwa ni swala la utatuzi wa mgogoro fulani,au swala la kisaikolojia kwa maana ya kuponya hisia fulani.Ndio kusema ni mchakato ambao mwisho wa siku utavutia upande mmoja yaani kumfanya mtu mwingine/taasisi ingine ifanye kile ambacho ungetaka kifanyike.Ndio kusema negotiator anaweza kuwa mnunuzi au muuzaji,mteja au msambazaji,bosi au mfanyakazi,mke/mume/mtoto,matokeo ya kile unachovutia kwako ndio yatakuwa kielelezo cha uwezo wako wa ushawishi

Mwandishi anasema kuwa kwa misingi ya kufanya negotiation ya biashara za Kimataifa,kuna maeneo muhimu ambayo lazima yazingatiwe,1.Bei 2.Masharti/Vegezo, (lini na kwa namna gani malipo yatafanywa)3.Delivery 4.Kiwango(quality) 5.Huduma. 6.mafunzo 7.Rasilimali(Watu,malighafi,fedha) 8.Scope 9.Mchakato.
Mwandishi anasema ni muhimu kwenda kwenye majadiliano ukiwa na na fikra ya Win-Win hii fikra itakufanya usiwe kwenye presha isiyokuwa na msingi,anasema wafanyabiashara wengi wa USA wa fikra za kushinda tu,jambo ambalo huwafanya wanapoteza,anashauri kuwa ni muhimu kuwa na na hii fikra !jambo la kuzingatia ni kuwa haufanyi kazi ya msaada! Kwa uzoefu wake anasema amesikia mara nyingi yule anayepoteza akijipa moyo na kusema..utaona tu kama sio leo lakini ntakukamata tu……

Mwandishi anasema ili usishindwe unapaswa kufanya yafuatayo,tambua dhamani kile unachotaka ku negotiate,kisha weka frequency ambayo upande mwingine utapenda/ili kuwachanganya,kisha weka mkazo kwenye Maslahi badala ya nafasi yako(Tazama Zaidi masilahi ya kampuni yako au ya nchi yako badala ya nafasi yako,ikibidi kufanya lolote ambalo litakuwa na faida kwa kampuni/nchi fanya hata kwa gharama ya nafasi yako)
Inashauriwa kuwa pale itakotokea upinzani kutoka kwa mtu wakati wa majadiliano hupaswi kukasirika,na ule upinzani usikuondolee focus.Jambo lisilokuwa na upinzani ni jambo la kawaida,jambo lolote zuri na la maana upinzani haukwepeki!,unachopaswa kufanya ni kutambua chanzo cha upinzani ili ujue namna ya kukabiliana kwa akili
Mwandishi anasema pamoja na ukweli kuwa huu ni mchakato wa majadiliano ya pande mbili,si vibaya kutumia ujanja ujanja ili kufikia lengo lako,anasema hakusudii kufundisha ujanja ujanja ila ni ruksa kutumia kwa maslahi yako au kampuni yako au nchi yako,msingi mkuu ni kuepuka kuwa muhanga wa negotiation(epuka kwa gharama yoyote ile kuwa muhanga)
Anasema lazima uwe makini kutambua ofa gani utoe,ofay a kiwango gani,uende kwa mwendo gani,etc .Hii ni kwa kuwa usipokuwa makini unaweza kwenda kwenye mkutano wa biashara,mfano umesafiri kwenda Kigali,yule mwenyeji wako akiwa smart anaweza akaomba tiketi yako ya ndege akijifanya anakusaidia kufanya reconfirmation lakini lengo lake ni kujua lini unarudi,hii itamfanya acheleweshe mazungumzo yenu hadi siku ya mwisho wakati unarudi Uwanjani,sasa kwa kuwa utakuwa umekaa siku nne Kigali,na unaona unarudi bongo kavu,unaweza kuingia mkataba ukiwa Uwanjani ili usiwe umeenda bure,hapa utakuwa umeliwa) hapa mwandishi anasema hii ni mbinu inatumika sana huko Magharibi(Ni ujanja ujanja)
Ili usiwe muhanga punguza kuongea sana,punguza kuwa mahususi kuhusu ulipofikia au tarehe zako za tiketi ya ndege
Kuwa mjanja epuka kuwa mhanga
 
Jina la Kitabu.How to Negotiate Anything with Anyone Anywhere Around the World
Jina la Mwandishi.Frank Accuf
Mchambuzi.Nanyaro EJ

Chapter 2

What Makes Global Negotiations Different? How Global Negotiations Work
Mwandishi anasema kuwa binadamu wana asili fulani inayofanana Duniani kote,isipokuwa mila na tamaduni ndio huwatenganisha au kuwatofautisha watu.Anasema wakati mwingine ni vigumu Zaidi pale ambako mchezaji ana uelewa wa mchezo na ana faida ya kucheza nyumbani,kutoka na haya mazingira tofauti mwandishi anatoa suluhisho kwenye baadhi ya mambo
Mwandishi anasema kuwa kwenye baadhi ya tamaduni muda sio jambo kubwa wakati kwenye baadhi ya nchi mfano Uswisi,ujerumani,USA etc wanajali sana muda,huko Latini amerika wanajali sana muda wa mwingine,mfano unawezakuta mwandishi ana appointment na waziri wa habari,hapo utasikia mwandishi akisema kuwa nina kikao na waziri nawahi ili nisije nikampotezea waziri muda wake,hizi ni jamii mbili tofauti zenye mtazamo tofauti kwenye swala moja.Hata wakati wa kufanya negotiation ni muhimu kutambua mtazamo wa kijamii kwenye swala la muda.Mwandishi anasema unajikuta umewahi pale lakini waziri anakuja masaa mawili baadae au asije kabisa akatuma ujumbe kuwa amebanwa na majukumu mengine! Huku Mashariki ya kati mradi unaweza kuchelewa kwa miezi miwili tangu tarehe iliyopangwa na isiwe shida maana wanasema tumesubiri miaka kumi au Zaidi sasa tukichelewa miezi miwili kuna shida gani?
Mfano mwingine ni wa Muktadha wa majadiliano dhidi ya Njia/Utaratibu wa majadiliano..kwenye baadhi ya jamii mfano Japan wanazingatia sana njia/kanuni kuliko Muktadha
Mwandishi anasema wakati wa kufanya negotiation lugha ya mwili ni muhimu sana(Body Language)iwe ni macho,mikono au chochote hii itasaidia kupeleka ujumbe wako kuelekweka kwa kina na msikilizaji.Pia hujenga Imani na kujiamini na kuaminika na upande wa pili.Wakati wa kupeana mikono pia huamua hatma ya negotiation hivo ni muhimu kutambua kama unatoa mkono(handshake) usitoe kwa unyonge utampa mpinzani wako faida ya goli la mapema.Ingawa kutoa mkono kwa ukakamavu sio tiketi ya ushindi pekee,aidha anasisitiza kujua matumizi ya lugha ya ishara mfano kwenye jamii nyingi dole gumba humaanisha kuwa kila kitu kipo sawa

Mbali ya Lugha ya Mwili lugha ya mdomo ni muhimu pia kujua neno gani utumie kutokana na utamaduni wa eneo husika.Yote hii ni kukupa upenyo wa kibiashara au jambo unalotaka kufanya lifanikiwe bila kutumia nguvu,mfano ukiwa New York unaweza kuongea Ki new York,lugha ambayo huwezi kuitumia ukiwa Jakarta au Osaka (hapa kwetu huku Kusini ukienda kwa nyumba ya mtu ukaomba maji ya kunywa kama aliyekuletea ni mwanamke anapiga magoti hadi umalize kunywa,wakati huku Kaskazini anaweza kukuletea akiwa anakimbia mchakamchaka).Kwa ujumla lazima ujue mchezo na namna ya kuucheza ndio siri ya mafanikio
Mwandishi anasema ili uwe negotiator wa Kimataifa lazima ujenge IMANI yaani ujiamini na uaminiwe na upande wa pili.Ili uaminike ni lazima ujike kwenye lile ambalo ni la msingi…..yaani uweke kisu vizuri kwenye mfupa au ulenge kwanza kabla ya kufyatua,watu wengi hufyatua risasi kabla ya kulenga na kujikuta akikosa shabaha na haaminiki tena
Baadhi ya changamoto zinazokabili biashara ya Kimataifa
1. Pace of Negotiations 2. Negotiating Strategies • Opening offers vis-a `-vis final settlement • Presentation of issues (e.g., one at a time versus in a group) • Presentations (e.g., formality, level of detail) • Dealing with differences (e.g., argumentative, conciliatory) • Concession behavior 3. Emphasis on Personal Relationships 4. Emotional Aspects • Sensitivity • Degree of emotions • Loyalty (e.g., degree and to whom) 5. Decision Making • Overall method (e.g., amount of authority) • Areas of emphasis (e.g., logic, concepts) • Emphasis on group/team • Emphasis on face-saving • Influence of special interests on decision makers 6. Contractual and Administrative Factors • Need for an agent • Degree of contract specificity • Degree of paperwork/bureaucracy • Need for an agenda
 
Huu uzi mkuu ni mzuri saaana ila shida ni kwamba tangia nimeanza kuusoma Mimi
Akili yangu imetamani kujua negotiations kuhusu utongozaji wa wanawake tu, maana biashara sina, uwezo wa kusafiri hadi nchi za nje kwenda kushawishiana na watu sina. Kwahiyo nimeelewa mambo mengi tu ila akili yangu yote imeelekeza hili darasa kwa madem na nitaaza kesho kufanya practical.
Safi sana mkuu Ila najua utanicheka Ila tupo wengi tu tunaowaza hivo
 
Huu uzi mkuu ni mzuri saaana ila shida ni kwamba tangia nimeanza kuusoma Mimi
Akili yangu imetamani kujua negotiations kuhusu utongozaji wa wanawake tu, maana biashara sina, uwezo wa kusafiri hadi nchi za nje kwenda kushawishiana na watu sina. Kwahiyo nimeelewa mambo mengi tu ila akili yangu yote imeelekeza hili darasa kwa madem na nitaaza kesho kufanya practical.
Safi sana mkuu Ila najua utanicheka Ila tupo wengi tu tunaowaza hivo
Mkuu kama vile ulijua ntacheka😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃biashara hata hapa ndani unaweza kuuza mayai au hata karanga ni biashara
 
Jina la Kitabu.How to Negotiate Anything
with Anyone Anywhere Around the World

Jina la Mwandishi.Frank Accuf

Mchambuzi.Nanyaro EJ

C H A P T E R 3 •

Ten Powerful Strategies for Negotiating Around the World
Kuna msemo wa Kiarabu unasema kuwa ‘‘If I listen, I have the advantage: if I speak, others have it.’’
Katika sehemu hii tutatazama mikakati kumi ya negotiation ambayo inaweza kuleta mabadiliko chana! Ni muhimu kukumbuka kuwa sehemu illiyotangulia tuliona kuwa tofauti za mila,desturi,na tamaduni huadhiri negotiation,hili lazima kulizingatia!Hata hivo mwandishi anasema hizi kumi alizochagua zinaweza kuleta matarajio

1: Plan Your Negotiation .Hapa zingatia kuwa kila mtu angependa kutoka akiwa mshindi kwenye biashara yoyote ile,kila mmoja angependa kupata sehemu kubwa Zaidi,kupata dili bora Zaidi,kwa msingi huu ni muhimu/lazima kufanya homework yako kwa ufasaha.Swala la maandilizi lazima liwe tabia isiwe tukio la siku moja(sio tukio kama harusi)jenga tabia ya maandilizi ya jambo lako lolote ulifanyalo,lipe maandalizi ya kutosha(wale watu wenye tabia ya kuamka na kutandika kitanda kabla ya jambo lolote huwa na nafasi kubwa ya kufanikiwa mambo yao katika mpangilio kuliko wale wa kuamka na kusepa))(Mpenzi msomaji jenga tabia ya kutandika kitanda ili uweze kupangilia siku yako)

2: Adopt a Win-Win, Mwandishi anasema huu ni mkakati wenye lengo la kumlainisha mtu wa upande wa pili!hapa utajenga mazingira ya yule mtu aone kuwa hapotezi chochote(hata kama kiuhalisia anapoteza)!ukifanikiwa kumfanya ajisikie mshindi,utakuwa umepata ushindi mapema sana!

Strategy 3: Maintain High Aspirations.Mwandishi anasema huu ni mkakati unaotumiwa sana na una matokeo chanya ya hapo kwa hapo.LAzima kumjengea mteja wako matarajio makubwa kutoka kwenye biashara unayokusudia kufanya.Mfano unaenda kijijini kutafuta sehemu ya kujenga hotel ya kitalii,na unataka wakupe ardhi,sasa utaonyesha vile kijiji kitanufaika na hiyo hotel kuanzia kodi za moja kwa moja na ambazo sio za moja kwa moja,ajira rasmi na ajira za muda,ule mnyororo wa usambazaji,kuanzia kwa mkulima wa karoti,mfugaji wa kuku na mayai yake hadi meneja atakayekuwa mzawa.Hii itatoa fursa kubwa ya kijiji kuingia kwenye 18! Au una kampuni kubwa ya usafirishaji let say una malori 100 yanayoenda mikoani,matumizi yake ya mafuta kwa siku ni lita elfu moja,unaweza kwenda kwenye kituo cha mafuta ukaomwonyesha yale matumizi yako ya kila siku na ukataka akupunguzie bei chini ya ile ya Ewura na hakika atakubali tu

Strategy 4: Use Language That Is Simple and Accessible .Matumizi ya lugha sahihi wakati wa mjadala ni nguzo muhimu katika kuleta mafanikio chanya.Ni marufuku kutumia lugha za mtaani.Lakini pia ni lazima utumie lugha ya ujumla ambayo sio ya kutengana…mfano unaweza kutumia nafsi ya tatu wingi…tukale nyama kwa mrombo wakati tunaendele na mazungumzo yetu….tukanywe kahawa…tupande mwendo kasi etc…..tumia lugha laini na tamu kwa kadri inavowezekana

Strategy 5: Ask Lots of Questions,
Kwa kadri utakavouliza maswali mengi ndio utakuwa na nafasi kubwa ya kujifunza na kumjua upande wa pili!ila lazima yawe maswali ya msingi sio yale maswali yatakayokuondolea uhalali.Hapa lengo kuu ni wewe kupokea taarifa,na ukiwa na taarifa sahihi uwezakano wa kushinda ni mkubwa sana
Sikiliza kwa hisia kali na onyesha kuwa unajali kusikiza,sio unasikiliza alafu unagusa simu,au kitu kingine hiyo itaonyesha ukosefu wa Umakini na itafanya uonekane wa kuja,na hivo kushindwa kupata dilil lako.Mwisho vaa upendeze,mavazi yako na viatu visafi! Mwonekano wako wa nje ni muhimu sana


Strategy 6: Build Solid Relationships
Mwandishi anasema kama ilivokuwa huwezi kushinda ubishi wa kisiasa au kidini ni muhimu ukaachana nao maana hautakusaidia chochote! Jambo la msingi ni dili lako la biashara hayo mengine sio sehemu na hayapaswi kuwa sehemu ya majadiliano.Kwenye nchi nyingi mahusiano binafsi husaidia katika kutengeneza dili,hivo una wajibu wa kutengeneza mahusiano yako na watu (Maisha ni watu)Baadhi ya maneno ambayo yatasaidia kujenga uhusiano(Kumbuka mahusiano yanajengwa na lugha nzuri)….nimefurahi kukutano na wewe…..tafadhali nielezee kwa kina kuhusu proposo yako…..samahani bado nina maswali machache kwako….Nimeumia hatujaweza kukamilisha……ni faraja kubwa hapa tulipofikia….etc


Strategy 7: Maintain Personal Integrity
Mwandishi anasema lazima uwe na uadilifu usiotiliwa shaka,maana kama sio mwadilifu hakuna mtu w maana atakuambia jambo la maana na wala hutamanika kwa watu wa maana.Kama hauaminiki na watu utajikuta unaambiwa mambo ya kawaida kabisa yasiyokuwa na msingi wowote.Ukiwa ni mtu mwadilifu hata upande wa pili utayeyuka mbele yako au utapata upenyo kwenye dili lako,maana lazima kuna mtu atakuja kukuambia nini cha kufanya kwa vile tu ni mwadilifu,Mwandishi anasema unaweza usiwe na cheti chochote cha shule au chuo lakini ukawa unafanikiwa kufanya mambo makubwa kuliko msomi wa PhD

Strategy 8: Conserve Concessions
Hii inatumika sana hapa kwetu hasa kwa machinga wanajua wateja wao,unakuta kiatu cha 50,000 mmachinga anaanzia laki moja.Hii ni kwa kuwa yeye mmachinga anajua kabisa kuwa wewe mteja utatamka 50,000 ambayo ni nusu ya bei,then yeye Machinga atakubali ile hamsini yako…wewe utajisifu kuwa umemshikia chini maana ilikuwa laki moja,kumbe ni kwamba machinga ameshasoma mchezo na anajua kwake yeye sio hasara


Strategy 9: Make Patience an Obsession
Mwandishi anasema uvumilivu ni muhimu,na kuna faida kadhaa ikiwepo,kupata taarifa Zaidi,hujenga mahusiano na husaidia katika kupata dili la faida

Strategy 10: Be Culturally Literate
Mwandishi anasema kuwa ni lazima kuzingatia na kuheshimu mila,desturi na tamaduni za maeneo mbalimbali,mfano unaweza kushika tama wakati wa mazungumzo kwenye baadhi ya jamii ukaonekana kama vile upo msibani.Mwandishi hakusudii kusema ufuate kila jambo bali anakusudia kusema kuwa ujifunze yale ambayo yanafaa na yasifaa kwenye jamii husika ili kufikia lengo tarajiwa.
 
Jina la Kitabu.How to Negotiate Anything with Anyone Anywhere Around the World
Jina la Mwandishi.Frank Accuf
Mchambuzi.Nanyaro EJ

• C H A P T E R 5 •

Negotiating in Western Europe

Mwandishi anasema tutaangalia jinsi ya kufanya negotiation kwenye nchi mbalimbali za Ulaya Magharibi,na EU kwa ujumla hasa kwa kuzingatia malengo yake makubwa ya kuwa na soko moja!
Mwandishi nasema kuwa ukiwa Ulaya Magharibi Muda ni mali,watu wengi wajali muda kuliko chochote,muda ni bidhaa adimu,aidha watu ni wabinafsi sana kule,mambo ya ujamaa hakuna kabisa,mbuzi anakula urefu wa Kamba yake,na mwenye kisu kikali ndie hula nyama nono….
Vitu kama likizo ndefu pamoja na kutumia muda na familia ni sehemu ya utamaduni wa Ulaya Magharibi(Likizo zao huwa kuanzia Julai/Agosti,ndio muda ambao husafiri sana kuja hapa kwetu kwenye hifadhi zetu na Zanzibar)wakati huo usitegemee kufanya nao chochote maana hawatakuwa tayari kuacha likizo yao.
Nchi kama Ujerumani au Austria zinazungumza Kijerumani lakini lafudhi tofauti na hupaswi kuchanganya wakati unadili na mojawapo ya hawa watu.Heshimu muda kufika kwa wakati kutakuongeza dhamani,nenda moja kwa moja kwenye swala na lielezee kwa kina…hizi ni jamii zinapenda kujua jambo kwa kina na mapana yake
………..Kumbuka uhusiano binafsi utaboresha uhusiano wa kibiashara…………..
Ukiwa Ubeligiji hupaswi kuzungumzia maswala ya siasa au lugha au mambo binafis,wala hata kuuliza swali binafsi.Unapaswa kufanya lile likupasalo kufanya.
Mwandishi anashauri kuwa ni muhimu sana kuzingatia ukaaji mezani,pamoja na ulaji unaozingatia mambo muhimu kutokana na tamaduni husika.Mfano ukiwa Ireland ni vema ukaepuka kujadili mambo ya nchi yao hasa mgogoro wa Kaskasini na Kusini ambao ni wa karne na karne,au Ukiwa Spain usijadili chochote kuhusu Catalunya na eneo linalobaki la nchi,hoja hapa ni kujua nchi husika ili usije ukaharibu biashara yako,ukashindwa kufikia malengo na jambo ambalo hauna suluhisho nalo.Raia wengi wa Ulaya Magharibi ni Wahafidhina hivo ni kwenda nao vile walivo cha msingi ni lengo lako lifikiwe(kuna kisa cha balozi wa Ufaransa EU alihutubia kingereza nchi yake ikamwondoa mara moja)licha ya kuwa na Umoja wa Ulaya bado kila Taifa limeshikilia lugha yake kama moja ya tunu za taifa husika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom