Mkuu tunaofahamu haya mambo ndio maana tunalia tunapoona watu wanapotosha mambo kwa makusudi kwa maslahi wanayoyafahamu wao wenyewe ni ya nani.
Wimbo wa demokrasia unalazimishwa kuonekana ni mtamu kwenye masikio ya watu, wakati kuna nyimbo nyingine watu hawajazisikiliza.
Uhuru wenyewe tumeupata kizembe zembe tu,tumekuwa wazembe hatujui hata maana kutafuta vizuri kwa gharama, tumeishia kudhani kwamba tunaweza kupiga hatua pasipo kuvuja jasho la damu kwa namna yoyote ile.
Tena huu haujapasi kuitwa udikteta,anatakiwa aongeze drip tukae sawa.
Dhana nzima ya kuwa na demokrasia kwenye nchi ni kumfanya kila raia apata kinda dhidi ya Seriakli pindi pale inapovuka mipaka. Na kwa upande mwingine ni kuikumbusha serikali kwamba hata kama ina dola lakini na wao ni raia kama wengine hivyo kuna uwezo wa kutoka pindi hamfanyi yanoyopaswa kufanywa na viongozi waliochaguliwa. Ndiyo maana tunaweka ukomo wa kutawala na kufanya chaguzi. Ule siyo mchezo ambapo umeamka tu asubuhi unaanza kulia na kupinga tu kila kitu; tukosoea panapohitaji kukoselewa na tusifie panapohitaji kusifiwa.
Demokrasia ya leo duniani siyo ile ambayo Wagiriki wa Athens waliitunga.
Kwanza kabla ya yote demokrasia ni lazima iendane na muktadha wa jamii husika.
Ni lazima izingatie miiko ya kijamii, tamaduni husika, utu wa mtu na haki zote za raia.
Leo wengi wetu tumeaminishwa kwamba chochote tutakacho kitaka basi tukiamua kupiga kula tutakipata, hii siyo kweli hata kidogo.
Kamwe, demokrasia haimjengi mtu wala taifa.
Bali watu hujenga demokrasia na taifa lao. Popote palipo na maendeleo ya kielimu na kiuchumi demokrasia huleta maendeleo chanya pasi kuvunja mshikamano na muunganiko wa watu. Lakini demokrasia hiyo hiyo kwenye jamii ambazo zipo nyuma kimaendeleo haswa kwenye nyanja ya kielimu na kiuchumi huleta mmonyoko mkubwa sana wa mshikamano wa kisiasa na kitamaduni.
Mathalani, mpaka leo hii Uchina inajenga demokrasia japo ni ya chama kimoja. Naamini ipo siku itakuwa ni nchi ya kidemokrasia kwasababu watu wake wameendelea kielimu, kitamaduni na kiuchumi; maamuzi yao yatakuwa sahihi sana kwa maslahi ya taifa lao. Mwaka 2007 Marekani alipigwa vita sana na mataifa ya Ulaya kwa kufanya biashara kubwa sana na taifa la Uchina ambalo wao wanasema linjavunja haki za binadamu bila hata soni. Jibu la Marekani lilikuwa ni moja tu kwamba " Uchina ikiendelea kibiashara lazima lazima uchumi ukue na huo uchumi utawaletea watu maendeleo ya kielimu kuwawezesha waweze kufanya mapinduzi ya kifikra" Kwa hiyo msomi atabaki kuwa msomi tu, hata umuweke chini ya shimo. Binafsi naamini Tanzania tuna safari ndefu sana, tunahitaji mabadiliko makubwa sana ya kimtizamo na kifikra.