How I Met My Wife

11th of Nzi Chuma..

Nitaandika hii mpaka nifike mwisho..

Mwaka wa tatu wa chuo kwangu ulikuwa na ubusy kidogo, so sikuwa na time sana na mapenzi kiviile, muda mwingi nilikuwa chuo, nikirudi usiku sanaa geto nimechoka, naweka simu silent nalala. Nai alikuwa mwanamke mwelewa sana, hakusumbua, shida niliipata hapa kwa single mama, akiwa yupo pale usiku anapiga simu mpaka unajuta yaani..mpaka sometimes nikawa nazima simu..yeye muda wote anataka mapenzi tu!! Mwezi mmoja kabla ya UE huyu single mother nae akapata mimba yangu. Alifurahi sana, alinambia kumbe alihangaika muda mrefu sana kupata mimba nyingine, lakini mimi nimemuwezea. Kwangu sikuona shida, nilijua kwa sababu anafanya kazi na ametafuta mtoto kwa muda mrefu, atazaa tu na atalea.. Lakini haikuwa hivyo. Nilivyoondoka tu pale Moro baada ya kumaliza UE, wiki mbili tu nyuma akaniambia imeharibika, nikajua atakua ameshaitoa.

Niliendelea kuwasiliana na Nai na pia niliendelea kuhudumia mtoto kwa Sophy!. Sikukaa sana kitaa nikapata kazi katika mradi flani ambao walikuwa wanatulipa vizuri, hapo nikaamua kujitegemea rasmi na kuanza mipango ya kuanzisha family.. Moyoni mwangu aliishi Nai tu. Niliamini nitamuoa tu one day.. Baada ya kufanya kazi kwa miezi sita hapa jijini nikawa niko vizuri sana. Nikarudi home na kuwaeleza mikakati yangu juu ya kuanzisha familia, nikawaeleza kuhusu Nai na yote yaliyotokea. Vidume vikajitokeza kunisaidia, nikavipa map vikafika kuonana na wazazi wake Nai..naam mtu mzima dawa, hawakutoka patupu..nikapata mrejesho wa kulipa mahari, nikalipa na kumuoa Nai, mtu niliyempenda zaidi maishani mwangu..!!. Lakini Nai hakuwa na raha na ndoa yetu, alikuwa anajua kuwa hawezi kupata mtoto. Lakini mimi nilimpa moyo kwa kumwambia kuwa ni bora nimekuwa mimi ambaye ndio msababishaji wa yote haya ndiye niliyekuoa kuliko angekua mtu mwengine, angekunyanyasa sana.. Nilijitahidi kufanya kila niwezalo Nai awe na furaha katika ndoa, lakini sidhani kama nilifanikiwa kwa 100%.

Muda flani akaanza kunilazimisha nioe mwanamke mwengine ili nipate mtoto (hapa tulishakaa miaka miwili katika ndoa). Alihisi sina amani. Lakini mimi nilikomaa nae, kila daktari mtaalam wa Gynecology niliyemsikia nilionana nae, dawa nyingi zikitumika lakini bado hatukufanikiwa. Mwisho nikamweleza ukweli Nai kuhusu Sophy, akaniambia niwasiliane na Sophy ili Abdul aje hapa atufariji.. Nikawasiliana na Sophy, nikamueleza mpango wangu, hapo ndipo Sophy aliponibadilikia na kunieleza kuwa yule mtoto hakuwa wangu kabisa, ni kuwa tu baba yake hajiwezi kiuchumi ndo maana akanibambikia, na ndo maana kipindi cha ujauzito hakunishirikisha..lakini baada ya mtoto kuzaliwa wakahisi atakosa huduma muhimu ndo maana wakanibambikia. Hapo hamu ikaniishia, sikutaka kuujua undani sana wa huyo mtoto nikaamua kupotezea.. Nikaconcentrate na Nai wangu..

Miaka ilipofika mitatu bila mtoto, nikalifanyia kazi wazo la Nai, nikaenda zangu kuchukua shombeshombe Pemba (how i met her, it's another story). Huyu ni kama alipata mimba siku ya harusi hivii...hahhahaa manaake alizaa miezi tisa kamili. Lakini Mungu sio Mzee Mkumba, baada ya kuoa, Nai alishika mimba mwezi mmoja tu mbele.. So alipishana na yule mke wangu wa pili mwezi mmoja tu kujifungua. Baada ya mwaka mmoja Nai akashika mimba nyingine na kuniletea toto la kiume (wa kwanza alikuwa wa kike). Kwa sasa nina watoto wanne, wawili wa kike na wawili wa kiume (kila mke mmoja akiwa na mtoto wa kike na kiume). Wanapendana sana na tunaishi kwa amani iliyopitiliza.
Wadau, nimejitahidi kufupisha ili nisiwachoshe.. and this marks the end of how I met my wife...!!.


Nzi Chuma, hadhuriwi na uvundo

Hongera sana ila sophy alikuwa mjanja sana na ulisema mtoto alikufanana kumbe ilikuwa wenge tuu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Then nilisikia tu, “oh My Gooooood”, nikaacha kufunga mlango kwenda kucheki. Sikuamini nlichokiona maze, Uso kwa uso na Boss Rona.
aisee hapa nimefanya kurudisha mwili nyum akwenye kiti nilichokaa na kushika kichwa na kusema oh shiit dah! nmejikuta nashka kichwa yani imeenda vibaya kinom adah bora angejua kivingine kwa kuambiwa dah aisee ....maan YOU ARE THE BOSS WITH THIS HISTORY...ni story matata sana
 
kamasi zinamtoka, machozi yashalowanisha uso mzima, Analia huku ananitazama as if ananiambia, “look at what we’ve done”.
da hivi hii ni stoty imetokea ati duh ..kama movie ...hey au ni story tu duh...tel me its real ....dah REAL SCENE LIKE A MOVIE
 
Tuliyoyafanya hayakua sawa, najua ulinipenda sana, na ningumu kuruhusu mpenzi wako wa zamani kuwa na mwanao lakini ni muda sasa umepita, please niruhusu niwe na mwanao tulee mjukuu wako”,
hatimaye Nora anajua...Series ya ukwelli sana...you have a stort to tell man...hii hata movie inatengenezwa
 
Nikasikia kitu ambacho sikutarajia kusikia kutoka kwake, “kalale kwanza na mama yako ndo uje hapa k***lamamayako".
this shows how people can change sana...nina experience ya kumuona school mate binti mmoja changing from innocent to kind of a bit**
 
The trip ilinireflesh kinoma. Na zaidi ya yote nlitokea kumuona vizuri Nasra. Ndani ya baibui aliyokua anavaa kulikua na shepu moja amazing mazee, na ile rangi nyeupe ya kirangi kwa.kweli she was good looking
atleast the NIGGA IS BACK ON HIF FEET...HAHAHAHA
 
KigaKoyo kaka yangu dunia ina masahibu makubwa sana kaka, wakati mwengine mtu anakusimulia yanayomkuta utaona kabisa huyu anadanganya, lakini kumbe ni ukweli mtupu, enzi za ujana wangu nilikutana na dada mmoja mrembo kutoka Arusha pale maisha club masaki akanisimulia jinsi alivyorubuniwa na tajiri fulani mkubwa kisha akaenda kumtelekeza kwenye shimo la machimbo usiku mkubwa katika Kafara za mali Baada ya kumlewesha chakari. Alikaa shimoni kwa siku 3 na kukumbana na mambo ya kuogofya sana, kutokea hapo Ndio alivyotambua ukweli juu uwepo wa Mungu. Alikuwa ananisimlia stori tunalizana mimi na yeye Kama watoto, makovu kwenye mwili wake hadi leo yanaonekana, ama kwa Hakika binaadamu tunapitia mengi na yakuogofya sana.
STORY YAKE PLEASE JAPO KIDOGO JF NI DARASA LA ELIMU DUNIA
 
“Kiga……. (akapause) pole kwa msiba, najua ni kipindi kigumu unapitia bt Mungu atakuvusha”… alivonambia hivi, sijui hata kilio kilitoka wapi, ila nilihisi simanzi nzito mno moyoni. I started crying
I CANT BLV KAMA NMELIA VILE YANI IMENIGUSA NA MACHOZI YAMEJA WA MACHO JAPO HAYAJATOKA....MUWASHO WA MAJI NDANI YA MACHO MACHOZI YANAPOANZA KUTOKA DAH HII NI FIRST STORY JF TO TOUCH ME EOTIONALY KWA MFULULIZO INSHPRT NISHALIA WANAUME NDIO TWALIAGA HIVI IMYA KIMYA AU KWA MACHO TU KUMOYOKUMOYO
 
I CANT BLV KAMA NMELIA VILE YANI IMENIGUSA NA MACHOZI YAMEJA WA MACHO JAPO HAYAJATOKA....MUWASHO WA MAJI NDANI YA MACHO MACHOZI YANAPOANZA KUTOKA DAH HII NI FIRST STORY JF TO TOUCH ME EOTIONALY KWA MFULULIZO INSHPRT NISHALIA WANAUME NDIO TWALIAGA HIVI IMYA KIMYA AU KWA MACHO TU KUMOYOKUMOYO
Thanks for the compliments man. If time allows ntakua naandika short stories.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli tulifunga ndoa, tukahamia mitaa ya tegeta nyumba kubwa Zaidi. Now miaka minne since nimemuoa Nora. Kama unajiuliza Nora alikua serious kuruhusu kushare na Nasra, jibu ni ndiyo. Sio mara moja ashanisurprise kwa threesome. Sometimes hotel room najua yuko alone, nawakuta wote wako ready kuliwa. Sometimes naangalia football sitting room nikienda kulala nawakuta wote bed, Tunapiga mechi ya mtu tatu kiroho safi.
THIS IS BEYOND AISEE HADI UKAPATA BARAKA ZA THREESOME...AISEE NA SISI UJAITOTEA HIYO..KWELI YOU HAVE A STORY ZAIDI YA STORY NA HAPO LIE IS GOOD MAANA THEY BOTH KNOW...ILA WOTE HALALI YAKO.
 
Nilikata simu na sikuongeza neno lolote, nikiri wazi kuwa sasa ni zaidi ya miaka 12 tangu sis anijib hivi sijawahi kupokea simu yake, kumpigia wala kujibu msg zake na najitahidi kumkwepa kila ambapo nitaambiwa yupo, hata kwenye misiba.. Maumvu ya siku ile uone hatma hayawezi kupona kabisa moyoni mwangu (na sijui ni kwanini). Kama sista unasoma hapa hii ndio sabbu kuu ya mimi kutopokea simu zako, na nadhani itabaki hivyo mpaka nitakapokufa iwe kwa Corona au Ukimwi...
sema kiukweli ulikuwa upumbavu huo hata kama hutumii condom...mimba zile ulikuwa mzembe na mpuuzi kuruhusu zembe vile..wote hata kama ulinogewa unplanned mimba zilikuw tatizo sana..mara moja sawa sio kila mara...haya we shusha tu sasa naogopa yanayotokea baadae na hizomimba ..ni kama horroe movie au kutotaka sikia saad events kwemye story na ukijua zitakuja tu hizo SAD events
 
8th Of Nzi Chuma

Nadhani sasa tunaweza kuendelea...

Naamini kutokana na urefu wa story na kwa sababu mimi sio msimuliaji mzuri, itakua nimesahau kuwaambia vitu vingi sana, lakini cha muhimu kwa sasa ni kuwa nilikaa kwenye hostel za chuo miezi mitatu tu, nikapanga nje, so wakati sekeseke la mimba ya Nai linaanza mimi sikuwa tena katika hostel za chuo...
Haya turudi sasa kwa Nai alipokuja geto.
Hii siku nahisi ni moja kati ya siku ngumu kuwahi kukutana nazo, Nai aliniamini kabisa na akahisi kupitia penzi letu lililokuwa moto kipindi hicho, tungeishi tu pamoja...Lakini kwangu mimi hofu ilikuwa kubwa sana, hili nadhani lilinizidi uwezo. Kukaa na Nai hapa ndani tena akiwa ametoroka kwao? Daaah...niliona kabisa siwezi. Vipi kama wataamua kumtafta binti yao halafu mwishoni kabisa wakamkuta geto kwangu? Ingekuaje?. Nai alichukua simu yangu na kuizima, kitu ambacho sikukubaliana nacho kabisa. Nilihisi hiyo ndo ishara kabisa ya kuwajulisha kuwa mimi niko na Nai... Kila nilivyojaribu kumwambia Nai kuwa aiwashe simu yangu, bora ya kwake ndo ikaendelea kubaki off aliniambia kuwa simpendi..kwani wakijua kuwa yeye yuko hapa ndo nini? Nikamwambia sasa lengo lako la kutoroka litakua na maana gani kama utabambwa siku ya pili au leoleo?? Mabishano yalikuwa marefu mpaka tulipozama mapenzini, tukayasahau yootee...nilipata nguvu ya kugegeda as if hatuko katika hatari..tulipomaliza, akili yangu ikarudi upya sasa, nikaichukua simu kinguvu na kuiwasha...sekunde kadhaa tu ikaingia msg iliyoandikwa kwa herufi kubwa.. "NAI NI MTOTO WA WATU SIO MKEO, RUDISHA MTOTO WA WATU KWAO USIJITAFUTIE MATATIZO". Msg kutoka kwa Mama Nai, nikamuonesha Nai hakuonekana kushtuka akanambia tu mjibu mwambie siko na wewe.. Mimi nikaamua kumpigia simu Mama Nai.." Haloo.. Mama nimeona msg yako lakini sijaielewa"... "Wewe usinifanye mimi mjinga, mrudishe Nai haraka" nikaamua kukaza mpaka maza akaamini kabisa kuwa mimi sikuwa na Nai pale geto..Mama Nai akaanza kuniomba ushirikiano wangu kama ninafahamiana na rafiki zake niwasiliane nao tuhakikishe kuwa Nai anarudi nyumbani kabla ya baba yake.. Ni siku hii ndo nilijua ukaribu uliokuwepo kati ya Nai na babaake, kumbe faza alikuwa akirudi nyumbani kitu cha kwanza anamuulizia Nai,yaani hiyo ni kabla hata hajaingia ndani..baada ya simu ya mama Nai ikaingia ya sista Hafsa kutokea Mbeya, naye alinihoji kwa nafasi yake akikata nimweleze ukweli kama Nai niko nae or not, akiniahidi kunilinda..mimi nikamkazia kuwa hatukuwa pamoja na wala sijui Nai alipo, wala hajawasiliana na mimi, mara ya mwisho ikiwa ni jana jioni..akanihoji vimaswali ambavyo vingempa mwangaza labda nimefacilitate Nai kutoroka kwa namna moja ama nyingine, lakini hakuambulia kitu..alipokata yeye nikapata muda wa kujadili na Nai juu ya hatma ya yeye kuendelea kubaki pale, italipa kweli!? Itakua na tija kiasi gani? Nai alikaza kuwa plan zote anazijua yeye na ni lazima ashinde hii vita. Baadae kidgo na kwa mara ya kwanza akapiga simu sista yule wa chuo, akijitambulisha kwa jina na Zai, yeye alikuwa mkali kidogo kuliko wenzie waliotangulia, yeye straight alikuja na command kuwa nimrudishe Nai kwao, ni kama alikuwa na uhakika hivi kuwa Nai yupo pale.. "Mimi mwenyewe nishayaharibu hapa nilipo lakini sikufikia hatua hiyo, kutoroka nyumbani hiyo ni hatua kubwa sana, msisitize Nai asifanye hivyo, arudi nyumbani, kama baba atakuja kulijua hilo atakufa, baba hawezi kuivumilia hiyo hali ya Nai kulala nje ya nyumbani, nakueleza kuwa kama hujui uzito wa hilo jambo mnalofanya na Nai basi ni jambo la hatari sana, haliwezi kuishia hivihivi...". Simu zote zilizopigwa niliweka loudspeaker Nai asikilize, lakini hakuonyeshwa kustuka, hii ya sasa ndo alicheka sana baada ya kukatwa. Mimi nilifikiria hatma yangu na lengo la mimi kuwa pale Moro ni masomo, kama itafika stage nitafukuzwa chuo kisa kumtorosha mtoto wa mtu kwa sababu dhaifu kabisa ya mapenzi nitakua mzembe wa nafsi yangu mwenywe, hapa sasa nikaanza kumbadilikia Nai. Nikaanza kumshawishi awashe simu na awasiliane na ndugu zake, atunge uongo wowote aujuao ili aruhusiwe kurudi nyumbani. Simu ziliendelea kumiminika, wale watu watatu walio sehemu tofauti wakawa kama wanapishana hivi katika simu yangu, akitoka kupiga Hafsa anapiga Zai mara mama Nai, nami niliendelea kuwapa ushirikiano kadri walivyonipigia nikiendelea kumsihi Nai awashe simu awasiliane nao arudi home, ila lilikuwa ni zoezi gumu kwakweli.. Muda flani akapiga simu Mama Nai akiwa analia "Hivi mwanangu, mimi leo unafikiri nitalalaje? Baba yake Nai akirudi hapa itakua kasheshe, naomba unisaidie mwanangu, fanya juu chini Nai apatikane arudi nyumbani..." Hii ilikuwa yapata saa 12 jioni sasa. Simu ya mama yake akiwa analia Nai aliisikia vzr tu, nikamwambia sasa tunaenda kupata laana...hii ni laana...nikamwambia acha mimi niende nikakutane na Mama Nai nimueleze ukweli, siwezi kukubali kuona mama yako analia namna hii kwa sababu ya ujinga wako, siwezi!! Nilimchimba biti Nai huku nikivaa nguo tayari kwa kutoka, nilikuwa sina nia ya dhati ya kwenda huko, lakini niliamini atastuka kwa hili.. Matokeo yake Nai akanigeuzia kibao..."wewe ni mwanaume muoga sana, hujiamini, sikutegemea kama utakuwa hivi, yaani hujiamini kabisa sijui ukoje, mimi nitarudi nyumbani lakini akilini mwangu najua kuwa nina mwanaume muoga asiyejiamini". Niwe mkweli, haya maneno yalipenya sana na kuniumiza, lakini tatizo la Nai aliangalia upande mmoja tu-wa mapenzi, mimi niliangalia pande zote, mapenzi na masomo..nikakubali kubeba lawama kuliko kuja kutia aibu familia, niliamini ni moja kati ya maamuzi magumu kwangu ambayo yatanifanya nisome kwa amani maana ndo kilichonileta Moro.. Nai akawasha simu yake, kigiza kikiwa kinaingia sasa, akampigia sista wake wa Mbeya-Hafsa akamueleza..."nilikwenda kushinda kwa rafiki yangu mitaa ya forest, bahati mbaya umeme haukuwepo na simu ya rafiki yangu pia ilizima kwahy akashindwa kutoa taarifa, kwa sasa baada tu ya kuwasha simu Nzi Chuma amenitafta na kunambia kuwa amepata usumbufu wa hali ya juu kwa sababu yangu, mnanitafuta sana..mimi niko poa ni simu tu ilizima". Dada yake alipomuuliza why hakuaga, alijibu hilo ni kosa na anaomba dada amuombee msamaha kwa mama ili akifika nyumbani asiadhibiwe...sista akaelewa na kumpigia bi mkubwa na kumwambia kuwa Nai asiguswe akifika hapo...dakika moja baadae sista Hafsa akanpigia na kuniambia "Nai kumbe alikuwa kwa rafiki yake Forest huko, amenipigia sasa hivi na nimemwambia arudi nyumbani, pole sana kwa usumbufu".. Nikajua sista amepangwa akapangika.. Mama Nai na sista Zai wao wala hawakunipigia.. Mpaka Nai alipofika home na kunijuza kuwa bi mkubwa amempokea bila kusema neno lolote, nikamtwangia bi mkubwa.. " Vipi mama mmefikia wapi? Mimi niko njiani nakuja huko tupange tunafanyaje".. Bi mkubwa akanambia "pumzika tu amesharudi" na kukata simu.. Huyu bi maza ni mtu kauzu kwelikweli, sijui kama alinielewa au alijua namchezea chezo tu.. At least Nai aliishi japo siku mbili tatu bila usumbufu wa kutakiwa kutoa mimba. Nikapata kiwiki kimoja flani cha likizo pale chuo, nikasepa TA. Huku nyuma nikapata taarifa mpya kuwa kwa sasa sista Hafsa ameungana na mama na sista Zai wote wanataka lazma mimba itolewe..hapa ndipo nilipomshirikisha hili jambo mtu ninayemheshimu kuliko watu wote ndani ya familia, aunt yangu flani hivi mwenye jina la mtoto wangu wa kwanza... Alinisikiliza kwa makini na kuact neutral.. "Sasa hapo kwakuwa familia nzima wamekubaliana kuwa wamtoe mimba, na kwa stage iliyofikia manake hawatakulazimisha wewe ndo ukamtoe wataenda wenyewe, wewe kinachotakiwa kutoka kwako ni kumshawishi tu Nai akubali hilo jambo, mimi naona kama ukubaliane nao, kuna siri nyingine za familia huwezi kuambiwa mwanangu, hao watu wanaweza kukuona unawawekea usiku na wakaamua kukushughulikia kwa njia wanazozijua wao.. Usiendelee kushindana nao..". Maelezi ya aunt ni kama vile yaliniingia hivi.. Ila nikamueleza jinsi Nai atakavyoniona msaliti.. Akaniambia mpigie simu Nai nikusaidie upande huo..nikampigia simu Nai wakasalimiana na kutambuana, kisha aunt akaanza kumpanga.. " Nzi Chuma amenieleza kuhusu hali yako ya mimba na amenieleza pia kuhusu mgogoro wenu, ila naomba nikwambie kuhusu mila na desturi za ukoo wetu, sisi hatuoi mke aliyezaa nje ya ndoa wala mke mwenye mimba, huu ni utaratibu wetu, kwetu sisi ni laana kufanya hivyo. Kwahyo nakuomba ukubaliane na wazazi wako muitoe hiyo mimba, kisha ukishakaa sawa mimi nakuahidi tutatuma watu kukuposa hapo..na nikikata hapa nitakutafuta kwa namba yangu ili tuendelee kuwasiliana mwanangu". Walizungumza kwa muda mrefu hadi Nai akakaa sawa. Lakini baada ya kukata simu akanitumia msg.. "Asante kwa kunisaliti, lakini naendelea kusisitiza kuwa wewe huna msimamo, kesho mimi nitaenda kuitoa mimba lakini Nzi Chuma wewe huna msimamo". Hii sms sikumuonesha kabisa aunt, nilikausha.. Kesho yake Nai aliongozana na mamaake wakaenda kuitoa mimba hospitali flani pale Moro, tumshukuru Mungu alitoka salama na ilimchukua wiki mbili tu kukaa sawa akawa kama awali. Baada tu ya kupona, Nai akaomba tuonane tena..akaja geto nakumbuka that day akiwa na kuku wa kienyeji aliyechinjwa na kutengenezwa na kuwekwa kwenye friji.. Alikuwa anawabeba mara kwa mara akija geto nilikuja kujua baadae sana kama walikuwa wakiwafuga kuku mle ndani kwao..akapika wali na kuku, tukagonga menu kisha akaniambia sasa kuwa amekuja na condom, hataki masihara kabisaa...akaitoa condom na kunivalisha kabisaaa kabla ya kuanza hata kumkiss..hii ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kutumia condom, yaani sikuelewa kabisaa.. Nilihisi kama nazingua.. Nilisubiri Nai akiwa amenogewa vilivyo nikachomoa mashine na kuivua condom na kuitupa chini kisha kurudisha mashine ndani, hiki kitendo kilichukua sio zaidi ya sekunde 3 kwahiyo ilikuwa si rahisi kwa Nai aliyenogewa kustukia, hatimayee nikauza mechi tena... Nai wala hakujua kama nimemwaga ndani, ni baadae usiku huko wakati yuko nyumbani kwao ndo akanambia kuwa amesikitika sana kuona nimemmwagia ndani wakati alinipa condom, na hata ilipofika round ya pili na ya tatu alinivalisha mwenyewe..ila nilimwambia Nai ukweli kuwa mimi hayo macondom siyaweziiii, akanambia "ok sawa ila nikipata mimba nyingine this time siitoi hata mfanyeje..". Tuliendelea na utaratibu wetu wa kumla yaani almost ni kila siku, penzi la Nai kwangu lilikuwa sio la mchezo...Mungu sio Mzee Mkumba, Nai akapata mimba nyingine sasaa.

Tumpe break Nai kidogo, tusije tukasahau story ni " how I met my wife".. Nani anafikiria kuwa Nai ndo mke wangu kwa sasa? Kama unafikiria hivyo, acha niendelee upande wa pili kabla sijarudi kwa Nai..

Jioni moja nikiwa pale chuo, alipita mtoto flani mwenye rangi za Kondoa, mrefu kiasi, alikua na sura ya kuvutia, na mwendo wake ulionesha ni mtu wa kazi.. Hakuwa na chura wa maana, lakini nilikuwa interested kumjua. Nikawauliza watu wawili watatu nikafahamu course anayosoma pamoja na room anayolala. Nikaanza kuwinda...siku moja nikakutana nae akiwa anaenda kuchukua msosi Canteen.. "Hellow Zahara, mzima?".. "who told you naitwa Zahara, mimi sio Zahara..." "basi aliyeniambia details zako hakuwa anakujua vizuri".. " Ni nani huyo?" "hata mimi simjui"... Blablaa.. Mpaka nikafanikiwa kumjua sasa kumbe anaitwa Zulfa na nikapata namba yake ya simu, nikaanza kuwasiliana nae..wakati naanza nae mawasiliano ndipo nikagundua Zulfa alikuwa ameniacha miaka minne, ingawa sura yake haikuonesha kama ana umri mkubwa kiasi hicho. Siku moja nikamuita sehemu flani iliyotulia pale chuo na kutaka kumfahamu kiundani, nikaanza kwa kujitambulisha mimi na kujielezea kiufupi, baadae akaanza kunieleza kuhusu yeye...story ya maisha yake ilinistua kidogo.. Pamoja na umri huo, hakuwahi kuwa na mahusiano na mwanaume yeyote maishani mwake, na wala hakuwa na mpango huo, muda wote huo alikuwa akihangaikia masomo yake tu ikiwemo ku-reseat mitihani ya form 4 mara 2 na kurudia kidato cha pili mara moja. (Wakati huo namfahamu alikuwa na miaka 30). Nilitaka kufahamu nini kilikuwa nyuma ya machungu hayo mpaka akawa hataki mahusiano na mtu yeyote? Akanieleza.. " Mama yangu alikuwa muaminifu sana kwa baba yangu, kiasi ambacho baba hakutakiwa kumtilia shaka mama hata kidogo, walizaa watoto wawili na wakiishi kwa amani sana, baadae baba alipata mwanamke mwengine na kuanza nae mahusiano, akaanza kuiona familia kama mzigo na kuanza kumdharau mama, mama alipitia kipindi kigumu miaka mingi sana mpaka baba alipoamua kumuoa huyo mke mwengine, ndo katika kipindi hiki ambapo mama yangu nae akapata ujauzito wangu, baba akakataa kabisa kuitambua hii mimba akidai kuwa mama atakuwa amechepuka kwa sababu yeye alikuwa hajafanya nae mapenzi muda mrefu sana, juhudi za kuwasuluhisha ziligonga mwamba na kupelekea mama kuachika. So kuanzia mimba yangu mpaka nazaliwa, mama alikuwa anapambana mwenyewe kuhakikisha naishi..na maisha yenyewe ya kijijini huko urangini ilikuwa shida sana.. (Alipofika hapa akaanza kulia). Ikabidi nianze kubembeleza sasa, ila baadae alinyamaza na kuendelea.. Kiufupi aliishia kwa tabu sana, alinyanyaswa sanaa na alishanusurika na matukio kadhaa ya kutisha ikiwemo kubakwa wakati akiishi kwa ndugu. Tangu akiwa mdogo, mama yake alimsisitiza kuwa hupaswi kumuamini mwanaume, hao ni washenzi kupindukia, hawana utu, tengeneza future yako hadi ieleweke ila wanaume wote wako sawa, hata ukiwa na future yako ni lazima baadae watakusumbua tu..!! Kwahyo yeye akatoka na msimamo wake kuwa hahitaji kabisa mwanaume maishani mwake... Kufikia hapa nikawa nishajua sasa naongea na mtu wa aina gani na natakiwa kwenda nae vipi..!! To make it short, niliweza kumshawishi Zulfa tuwe katika mahusiano, na kwakweli kutokana na ugeni wake na umri aliokuwa nao, alizama katika mahusiano mzima mzima. Nashukru Mungu niliweza kumbadilishia mtazamo wake juu ya wanaume na akaonyesha kwa vitendo hasa. Maisha yangu ya chuo yalianza kunyooka kisawa sawa kutokana na Care ya Zulfa, aliniamini kupita maelezo (nakiri wazi kuwa sijawahi kuaminiwa kwa kiwango hiki). Boom likitoka nakabidhiwa kadi na kuambiwa tu "tumia vizuri".. Mimi ndo nikawa mpangaji wa matumizi ya kile kiasi cha boom.. Lakini Zulfa alikuwa mtu wa maono hasa, alikuwa na akili iliyopevuka tayari.. Akanishauri tulime alizeti huko kwao, kwahiyo tukawa tunachukua kiasi kwa ajili ya matumizi yetu, kiasi kingine tukaanza kulima..naam...na pale chuo tukaanzisha vibiashara vidogo vidogo ambavyo yeye ndo alikuwa main supplier..vipafyum vya kike na vihand bag.. Maisha yakawa yanaenda vizuri kabisa, hatukaukiwi..japo nilizitumia pesa nyingi tu kukamuana na Nai..!!.

Naomba nipate break kidogo... Nitarudi baadae baadae hivi, ngoja nikapate Alqasuus...!!

Sent using Jamii Forums mobile app
ANOTHER LEGENDARY STORY .....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom