Let the CCM fans reply...And, How CCM underdeveloped Tanzania?
Let the CCM fans reply...And, How CCM underdeveloped Tanzania?
...Katika eneo la Mashariki ya Kati, kuna nchi mbili ambazo, kama zina maendeleo ya kiuchumi au kufanikiwa kijamii, ni kutokana na misaada na namna walivyoitumia. Nchi hizo ni Israel na Jordan.
...Inakadiriwa kuwa, mpaka kufikia mwaka 2008, msaada wa Marekani kifedha kwa Israel, ulikuwa USD 114 Bn.
...Nadhani, issue kubwa hapa ni jinsi ambavyo misaada inatumika. Je, fedha hizi hufika au hufanya kazi zilizolengwa? Je, ubadhirifu kwenye miradi inayofadhiliwa kwa fedha hizi ni wa kiasi gani na unadhibitiwa vipi? Je, miradi hii inafaida kwa jamii na nchi?
...Aidha tukumbuke kuwa, misaada si lazima iwe ya fedha. Inaweza kuwa ya kujifunza utaalamu fulani, kupewa teknolojia fulani, n.k.
...Wanaofurahia kusitishwa kwa misaada hii na wale wanaobeza, hawajui kitu kuhusu misaada, au wanaongozwa na ushabiki wa kisiasa. Watakaoathirika ni wananchi waliokuwa wakifaidika na miradi ya afya, elimu, maji na umeme, ambayo kwa namna moja ama nyingine haikuweza kufadhiliwa na Serikali.
...Misaada, iwe ya aina yeyote ile, ikitumiwa vizuri huleta maendeleo kwa jamii na kuchangia kukua kwa uchumi.
Hawajui watendalo indeed.Nilisoma kitabu hiki mara ya kwanza 1974.Oh,kilibadilisha mtazamo wangu kuhusu nchi za magharibi na misaada yao kabisa.Sidhani kama vijana wa kileo wameshawahi hata kukisoma kitabu hiki let alone kukisikia.Ndio maana hawaoni ubaya wa misaada ya wanyonyaji hawa waliojificha kwenye jina la wafadhili.Siku hizi wanaitwa partners of develoment!What a shame.Hawa sio partners ni adui zetu.
View attachment 333820
Ukisoma kitabu hiki utajua namna Ulaya ilivyoididimiza Afrika!
Na bahati mbaya mpango huo bado haujaisha!
Tunaoshabikia misaada hatujui tutendalo!
View attachment 333824
Nakuwa optimist sana kwa falsafa ya hapa kazi tu ya Bw. Magufuli hasa kwa kiburi alichokionesha kwa Mmarekani na umarekani wake na misaada yake ya kinafiki, sasa ifike hatua, nasi tuombwe misaada. Nilifuatilia vizuri sana wakati alipokuja Obama. Katika hotuba ya kumkaribisha, the then Tanzanian President, the so-called Mzee, His Excellency Dr Kikwete, alikuwa anainyenyekea sana misaada na kuiomba iendelee, yaani hadi aibu.
Tanzania tunaweza, kikubwa tunatakiwa tuwe wazalendo.
hivi vitu tumevisoma sana t6angu mashuleni.......View attachment 333820
Ukisoma kitabu hiki utajua namna Ulaya ilivyoididimiza Afrika!
Na bahati mbaya mpango huo bado haujaisha!
Tunaoshabikia misaada hatujui tutendalo!
View attachment 333824
hakuna taifa litakalotusaidia bila lenyew kuwa linafaidika pia, si marekan si watu wa ulaya wala wachina....shida hapa ni kwamba pengine masharti yanayotolewa na europe na hawa america yanakuwa yanatishia chama kama demokrasia au uhuru wa kujieleza yanakuwa yanatishia baadhi ya watawala kubaki madarakan ndo mana viongozi wa africa hapa tunakuwa wakali sana..ndo mana nchi zetu nying za zinaipenda china kwakuwa yeye hufuata interest zake tu habari za mnafungana mnapigana ye hana habari nazo.............View attachment 333820
Ukisoma kitabu hiki utajua namna Ulaya ilivyoididimiza Afrika!
Na bahati mbaya mpango huo bado haujaisha!
Tunaoshabikia misaada hatujui tutendalo!
View attachment 333824
Matatizo mengine ya kwetu wenyewe kutolipa kodi kusaini mikataba isiyo na tija kwa taifaMkuu, kuna watu wanashabikia ujinga wakidhani kufanya hivyo watapata faida yoyote!
Hiii nimeipendaAnd, How CCM underdeveloped Tanzania?
...Nadhani hapa tafsiri ya neno msaada au maana yake, ndio itagomba.Mkuu, hivii katika akili za kawaida Israel unailinganisha na Tanzania? Nashindwa kuamini moja kwa moja kusema kwamba Israel imeendelea kwa asilimia kadhaa za msaada wa Mmarekani, yawezekana Mmarekani ndiye alieyeendelea kwa expense ya Israel. Kwa nini nasema hivyo? Israel na waisrael ambao wengi wao ni wayahudi ni watu waliobarikiwa sana vipaji katika Nyanja tofautitofauti ikiwa ni pamoja na kijeshi, kisayansi na hata kisiasa. Kama huwa unafuatilia vizuri, marekani hadi kuitwa superpower katika anga la kijeshi na kivita ni juhudi za Myahudi. Mfano, Albert Einstein aligundua bomu muhimu kabisa katika historia ya Marekani ambalo ndilo lililotumika kuipiga Hiroshima tarehe 6 August 1945 na siku tatu baadaye bomu lingine la aina hiyohiyo lililotengenezwa na mtaalamu huyohuyo ndilo pia likatumika kuipiga Nagasaki. Ni baadhi ya silaha ambazo ziliipa jina kubwa Marekani ambazo ni juhudi za Kiyahudi. Hali kadhalika kuna wataalamu kibao wa kiyahudi katika afya na idara zingine za Marekani, pamoja na usalama wa Taifa pia, yaani CIA na FBI.
...Naona tafsiri yako ya neno msaada ni tafauti na ile inayofahamika, au ambayo iko kwenye hoja.Mkuu, pia umesema kwamba, msaada si lazima uwe wa kifedha, bali unaweza kuwa wa kitaalamu ikiwa ni pamoja na kupewa teknolojia Fulani. Kama ni hivyo, hata Afrika basi ina mchango na msaada mkubwa kwa Marekani. Inasadikika kuwa, kuna wataalamu wengi kutoka Ethiopia na Botswana, na hizi zote ni nchi za kiafrika, sasa je, na sisi tusitishe misaada kwa Marekani? Najua jibu hapa ni kwaba hatutaweza kwa maana huko wataalamu wetu wanalipwa shavu zuri kuliko katika nchi zao. Sasa kumbe na hata sisi tungekuwa tunawalipa vizuri wataalamu wetu na kuwathamini, basi nafikiri wangebaki na kama wangebaki, basi naamini wangeliendeleza Taifa. Lakini je, kuwalipa vizuri na kuwathamini inatosha kuwa-brainwash wasikimbie? wanahitaji pia kuwa katika utawala bora wenye demokrasia ili wafurahie maisha yao kwenye nchi yao. Haya, kila leo tunasikia na kuona madaktari wanaandamana kudai waongezwe mishahara, na baadhi yao wanaoonekana ni spokenmen hutolewa meno bila ganzi, je watakuwa na hamu ya kukaa nchini kwao? Go back in memory kwa alichokipata Dr Ulimboka, nafikiri kama wewe ni mzalendo mkuu, ungetoa hadi machozi kwa walichomfanyia.
...Tuko pamoja!Mkuu, huwa naamini sana katika nadharia za kifalsafa na ni kwa namna gani wazee wa zamani waliendelea. Mfano, mwanafalsafa Goran Hyden (1943) yeye anaamini, "...development is a result of human efforts...". Lazima kwa namna moja ama nyingine utakubaliana na mimi kuwa, nchi yoyote huendelea kwa juhudi za watu wake wenyewe. Sasa je, ni watu wa aina gani? Ni raia wa kawaida na viongozi kwa pamoja Hyden ndio anaowazungumzia. Raia tunao na tena ni wavumilivu na wachapa kazi wanaofanya kazi kama recruits, lakini viongozi hatuna.
..."hapa ni kazi tu" si falsafa, ni msemo maarufu.Nakuwa optimist sana kwa falsafa ya hapa kazi tu ya Bw. Magufuli hasa kwa kiburi alichokionesha kwa Mmarekani na umarekani wake na misaada yake ya kinafiki, sasa ifike hatua, nasi tuombwe misaada. Nilifuatilia vizuri sana wakati alipokuja Obama. Katika hotuba ya kumkaribisha, the then Tanzanian President, the so-called Mzee, His Excellency Dr Kikwete, alikuwa anainyenyekea sana misaada na kuiomba iendelee, yaani hadi aibu.
...Tafsiri rasmi ya uzalendo ni patriotism. Tatizo lililopo kwenye uzalendo/patriotism ni pale ambapo wananchi hawaoni kama Serikali inawajali, kusimamia na kulinda maslahi yao. Hapa kuna kundi kubwa halitakuwa na uzalendo, maana hawaiungi mkono Serikali.Tanzania tunaweza, kikubwa tunatakiwa tuwe wazalendo.
Mkuu shikamoo!Danganyikeni ninyi sio mimi. Tumekuwa wavivu na wezi halafu tunazingizia watu wengine. Vitabu kama hivyo vinamfanya mwafrika azidi kudumaa kimawazo badala ya kusonga mbele. Kuna mataifa kama waisrael walipata shuruba isiyosemekana na leo wana maendeleo ije kuwa sisi?